- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Kongamano la Istanbul “Gaza iko katika Mshiko wa Mauaji ya Halaiki, Mitego, na Usaliti.”
Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa tatu ya Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa, mnamo Jumapili sawia na tarehe 04/10/2026 Hizb ut Tahrir Wilayah ya Uturuki iliandaa kongamano katika jiji la Istanbul chini ya kichwa: “Gaza iko katika Mshiko wa Mauaji ya Halaiki, Mitego, na Usaliti.”
Kongamano hilo lilifanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Nini Hatun huko Esenyurt, huku likiwa na hadhira kubwa na yenye shauku. Kongamano hilo lilionyesha mawasilisho ya maarifa muhimu na masuluhisho yaliyopendekezwa yanayolenga kulibakisha suala la Gaza mbele ya umakini wa umma na kuwakumbusha Waislamu, haswa wanazuoni na wanafikra, majukumu yao kuelekea hilo.
Programu, iliyoongozwa na Ibrahim Kahya, ilianza kwa kusomwa aya kutoka Quran Tukufu, na kufuatiwa na uwasilishaji wa video inayoangazia dhulma na ukatili unaotokea Gaza. Kisha, Muhammad Amin Yildirim, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Uturuki, alitoa hotuba ya ufunguzi.
Yildirim alisisitiza kwamba kadhia ya Gaza na Palestina sio kadhia ya kibinadamu au ya kimaadili tu, bali kimsingi ni kadhia ya Kiislamu, akisisitiza umuhimu mkubwa wa kuishughulikia kwa mtazamo huu. Alisema: "Gaza na Palestina sio ardhi takatifu inayoshirikiwa na dini tatu, kama baadhi ya sauti za kupotosha zinavyotangaza, wala si mahali ambapo Waislamu na Mayahudi wanatakiwa kuishi pamoja kwa msingi wa kile kinachoitwa suluhisho la dola mbili kwa uwongo na kwa uzushi. Badala yake, ardhi hii ni ardhi iliyobarikiwa iliyoshuhudia Safari ya Isra na Miraj, na inakumbatia Msikiti wa Al-Aqsa, Qibla chetu cha kwanza. Kuilinda Palestina, kuikomboa kutokana na uvamizi, na kuilinda kwa njia ambayo haimfanyi mtu yeyote kusubutu kuitamani au kuidhuru baada ya hapo ni wajibu wa kidini kwa Umma wa Kiislamu."
Kufuatia hotuba ya Mehmet Emin Yıldırım, Mehmet Mışeniç, Mwenyekiti wa Chama cha Mshikamano wa Palestina (FIDDER), alipanda jukwaani. Baada ya kusisitiza umuhimu wa kuweka kadhia ya Gaza mbele ya ufahamu wa umma, Mışeniç alisema: "Watu wanaweka matumaini yao kwa Gaza kwenye mpango unaoitwa wa amani uliotolewa na Trump, Farauni wa zama zetu na mfano halisi wa uovu. Tangu kile kinachoitwa kusitisha mapigano, misaada ya kibinadamu haijaruhusiwa kuingia Gaza katika kiwango kinachohitajika. Kile ambacho Gaza inahitaji zaidi leo ni usaidizi mkubwa. Watu wote wa Gaza wanaishi katika mahema. Lakini naweza kusema kwa fahari kwamba ndugu zetu mujahidina huko Gaza hawajasalimu amri, na hawatasalimu amri kamwe. Licha ya shinikizo la nje na usaliti wa ndani, upinzani utaendelea kwa sababu ni suala la imani isiyoyumba nyoyoni mwao."
Baada ya Mışeniç, mwanahabari na mwandishi Ahmet Faruk kutoa hotuba yake. Na baada ya kulinganisha ukombozi wa Salahuddin dhidi ya Al-Qudsi kutoka matekani na kuanguka kwake chini ya uvamizi, Farol alisisitiza hitaji la suluhisho msingi, akisema, "Uhalisia tunaokabiliana nao leo haupaswi kamwe kutufanya tukate tamaa. Kama Umma wa Kiislamu, lazima tufanye kazi kwa dhati kurudi kwenye mfumo wa Mungu na kusimamisha Khilafah. Khilafah itakaposimamishwa, Mwenyezi Mungu akipenda, Amerika na umbile la Kizayuni watapiga magoti mbele ya Waislamu."
Kufuatia hili, mwanaharakati na mwandishi Erdal Elbiyuk alichukua nafasi, akiwasilisha mifano ya kuvutia ya vikwazo vilivyowekwa na biladi za Kiislamu katika njia ya misafara ya misaada inayojaribu kuvunja kuzingirwa kwa Gaza. Alisema: "Mateso na dhulma inayoipata Gaza ni matokeo ya vitendo vya watawala wa nchi hamsini na saba za Kiislamu. Kwenye kichwa 'Gaza ndani ya Mshiko wa Mauaji ya Halaiki, Mitego, na Usaliti,' tunapaswa pia kuongeza neno 'kujisalimisha.' Watawala hawa wana tabia kama Mayahudi linapokuja suala la kuruhusu msaada kufika Gaza; wamejisalimisha kwa karibu kwa Israel. Tunashuhudia usaliti kila mahali, na usaliti huu unawapa ndugu na dada zetu mateso sawa na yale wanayopata kutoka kwa umbile lenyewe la Kiyahudi."
Hotuba ya mwisho ya kongamano hilo ilitolewa na Dkt. Abdul Rahim Shen, mwandishi na mtafiti wa sheria za Kiislamu. Dkt. Shen alitoa shukrani zake kwa mujahidina waliotekeleza Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, ambayo ilitikisa ulimwengu na kuwakumbusha Waislamu tena kuhusu kadhia ya Palestina.
Wakati wa hotuba yake, ambayo ilikuwa imejaa mifano yenye nguvu na maana kubwa, Dkt. Shen alitoa uchambuzi muhimu wa kisiasa na kutoa kauli zifuatazo: "Kimbunga cha Al-Aqsa kilimkasirisha sana kafiri Trump, mhandisi wa usawazishaji mahusiano. Kwa hivyo, aliamuru umbile la Kizayuni, analolidhibiti, kufanya mauaji ya halaiki. Kile kinachoitwa kusitisha mapigano kilitekelezwa tu ili kunyamazisha Gaza. Kuhusu watawala wanafiki katika nchi za Kiislamu, ambao hawakuweza kuchukua hatua yoyote ya kuruhusu hata tone moja la maji kuingia Gaza, wote walichukua hatua, kwa amri ya Trump, kuhakikisha mafuta yanapita kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz. Watawala hao wamejichukulia jukumu la kuwanyang'anya silaha ndugu zetu, na kutengeneza njia ya kuanzishwa kwa utawala wa mamlaka nchini Palestina. Huu ndio mzunguko mbaya wa usaliti."
Kwa kuegemea aya kutoka Quran Tukufu, Dkt. Shen aliwasilisha uchambuzi mfupi wa matukio huko Gaza, akifichua kile alichokielezea kama usaliti unaofanywa na serikali za nchi za Kiislamu. Pia aliwakumbusha wanazuoni wajibu wao wa kusema ukweli na kutouficha.
Katika kumalizia maelezo yake, Dkt. Shen alinukuu hadith ya Mtume ikisema kwamba Kiyama hakitafika hadi Waislamu na Mayahudi wapingane.
Alielezea imani yake kwamba majeshi ya Ummah wa Kiislamu, yatakapoungana chini ya bendera ya Khilafah, yatalishinda umbile la Kizayuni na kukomesha uwepo wake katika ardhi zilizobarikiwa zinazozunguka Msikiti wa Al-Aqsa. Kwa mtazamo huu, alisisitiza umuhimu wa Waislamu kushikilia kwa nguvu matumaini ya ukombozi na ushindi.
Programu hiyo ilimalizika baada ya Dkt. Abdul Rahim Shen kumaliza kutoa hotuba yake.
Mjumbe wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Katika Wilayah ya Uturuki
Jumapili, 22 Rabi’ ul-Akhir 1448 H – 04 Oktoba 20226 M

- Sehemu ya Amali ya Kongamano -
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/uturuki/5450.html#sigProIddef8ef0500

Alama Ishara
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies

Kwa Maelezo Zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki:
Tovuti Ramsi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki
Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki
Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki
Tovuti ya Jarida la Kokludegisim




