- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
Angazo la Amali za Kimataifa za Hizb ut Tahrir
katika Kumbukumbu ya Kuvunjwa Khilafah
1447 H – 2026 M

Katika mwezi mtukufu wa Rajab wa mwaka huu, 1447 H (2026 M), tunakumbuka kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, vibaraka wa wakoloni makafiri. Dola hii ilianzishwa na Bwana wa Mitume, Muhammad (saw), na Maswahaba zake Watukufu (ra). Mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) uliondolewa mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na 3 Machi 1924 M, mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal. Kumbukumbu hii ya kusikitisha inarudi kwetu huku mauaji ya halaiki yanayofanywa na umbile la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza yakiendelea, kama vile mauaji ya kikatili yanayofanywa katika Ukingo wa Magharibi. Ukatili huu umesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa, na kutoweka kwa zaidi ya wanaume na wanawake Waislamu 230,000 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, wengi wao wakiwa wanawake, watoto, na wazee. Zaidi ya hayo, vita visivyo na maana na vya umwagaji damu vinavyoendelea nchini Sudan vinaendelea kuchukua maisha ya Waislamu wasio na hatia huko, vikitumikia maslahi ya makafiri wa Amerika, ambayo yalichochea mzozo kati ya vibaraka wake wa kutenganisha Darfur na Sudan, kama vile ilivyoitenganisha Sudan Kusini hapo awali.
Kwa sababu hizi zote, Hizb ut Tahrir inaandaa amali kubwa za umma katika nchi ambazo inafanya kazi ili kuwaamsha Waislamu na kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii na hizb ili kusimamisha Dola ya Kiislamu (Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume). Dola hii pekee ndiyo inayoshikilia ufunguo wa izza ya dunia na wokovu Akhera, na ndiyo pekee inayoweza kuikomboa ardhi na watu wake kutokana na makafiri wahalifu!
Sisi, katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, tutatoa taarifa kamili ya amali hizi kwenye ukurasa huu, tukimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume.
Ijumaa, 13 Rajab 1447 H sawia na 2 Januari 2026 M

(Hotuba ya Amiri)
Hivi Punde!

Ujumbe kutoka kwa Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Mohammad)
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Kumbukumbu ya Miaka 105 ya Kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah
Hivi Punde!

Ujumbe kutoka kwa Dada Rana Mustafa
Mwanachama wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Maadhimisho ya Miaka 105 ya Kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah
Hivi Punde!

Alama Ishara za Kampeni
| #ReturnTheKhilafah | #TurudisheniKhilafah |
| أقيموا_الخلافة# | #EstablishKhilafah |
| #YenidenHilafet | خلافت_کو_قائم_کرو# |



MATOLEO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Fuatilia kwa Lugha Nyenginezo
![]() |
|





