Jumapili, 25 Shawwal 1447 | 2026/04/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Mahouthi Wawakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa Kufichua Mkataba wa Trump!

Mnamo Ijumaa, 21/11/2025, kundi la Mahouthi katika Jimbo la Ibb liliwakamata wanachama wawili wa Hizb ut Tahrir, ndugu: Osama Muhammad Mas’ad Al-Wurafi (umri wa miaka 19) na Ibrahim Muhammad Mas’ad Al-Wurafi (umri wa miaka 15) kufuatia usambazaji wao wa toleo lililotolewa na Hizb ut Tahrir lenye kichwa: “Trump Anawaongoza Wafuasi Wake miongoni mwa Watawala katika Ardhi za Waislamu Kwenye Mkataba wa Fedheha na Aibu, Wakiinamisha Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza Hashem chini ya Usimamizi na Ukoloni!” Toleo hili lilisambazwa nchini Yemen na nchi nyingi za Waislamu.

Mauaji Mapya Yatekelezwa na Umbile Halifu la Kiyahudi katika Kambi ya Ain Al-Hilweh!

Katika muktadha wa kile ambacho Amerika inaendesha katika suala la amani na uhalalishaji mahusiano nchini Lebanon na eneo hili—ambapo kiuhalisia ni kusalim amri na kujisalimisha—umbile halifu nyakuzi la Kiyahudi, pamoja na silaha za Marekani, risasi za Ulaya, mikono ya Kiyahudi, na ushirika rasmi wa Waarabu, lililipua uwanja wa michezo na klabu ya michezo katika kambi ya Ain al-Hilweh katika mji wa Sidon kusini mwa Lebanon mnamo Jumanne, 18/11/2025. Mashahidi kumi na tano waliauwawa katika shambulizi hili la kikatili, na makumi ya watoto na raia walijeruhiwa, katika shambulizi baya linalothibitisha uhalifu wa umbile la Kiyahudi na uadui wake dhidi ya Waislamu.

Kauli za Patriarch Bechara Al-Rahi Kuhusu Wakristo katika Eneo Hili Mshikamano wa Kudumu kwa Fahamu ya Marekani na Kimagharibi ya “Walio wachache”, iliyo ngeni kwa Watu wa Eneo Hili na Historia Yao!

Katika mahojiano yake na chaneli ya Lebanon Al-Jadeed katika kipindi cha “Huyu ni Mimi” na mwandishi wa habari Samar Abu Khaleel, kauli za Patriarch Bechara Al-Rahi zinaambatana na ziara ya Papa Leo XIV katika eneo hili, ikiwa ni pamoja na Lebanon, hasa kuhusu suala la kubadilisha utawala wa Syria na kauli yake: “Wakristo wanaondoka Syria leo kwa sababu dola iliyopo ni dola ya Kiislamu! Ingawa haikuwa hivyo wakati wa utawala uliopita...” Na msimamo huu ni uthibitisho wa msimamo uliopita wa Patriarch mwenyewe; ambapo alisema mwaka wa 2011 wakati wa ziara yake nchini Ufaransa chini ya Sarkozy: “Kukiri kwamba makosa na ukiukwaji wa sheria uliotokea nchini Syria hakubatilishi ukweli kwamba Rais Bashar Al-Assad alikuwa ameanza mageuzi, na angepaswa kupewa nafasi”!

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu