Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 588
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Vichwa Vikuu vya Toleo 588
Vichwa Vikuu vya Toleo 588
Vichwa Vikuu vya Toleo 587
Mwezi mtukufu wa Ramadhan unatukumbusha kwamba Uislamu ulikuja tu kubadilisha ulimwengu na kutatua matatizo ya wanadamu kulingana na muongozo wa Mwenyezi Mungu (swt) na kwa ruwaza iliyowasilishwa katika Quran na Sunnah. Tunaposhuhudia dhulma, ukandamizaji, na misiba mingi na matatizo yanayoukumba ulimwengu wa Kiislamu na wanadamu kwa jumla, ni wazi kabisa kwamba tunahitaji sana ruwaza sahihi ya mabadiliko iliyo wasilishwa na Uislamu.
Enyi Waislamu, nawakumbusha haya yote katika siku hizi ambapo uvamizi wa kikatili wa Mayahudi dhidi ya Ukingo wa Magharibi pamoja na Gaza unaendelea, kisha uvamizi wa Mayahudi ukaenea hadi Lebanon na Syria… ambapo waliranda wakiwa huru katika nchi za Kiislamu bila kukutana na upinzani wowote wa kweli. Badala ya watawala kuhamasisha majeshi ya Waislamu kupigana na umbile la Kiyahudi, kuwafukuza wale walio nyuma yake na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa... badala yake, tunawaona watawala hawa wakisaini makubaliano baada ya makubaliano nalo, na hata mtawala dhalimu Trump anawakusanya pamoja ili kuwadhalilisha, bila aibu yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, au waumini!