Jumatatu, 26 Shawwal 1447 | 2026/04/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Trump Awaongoza Wafuasi wake kutoka kwa Watawala katika Ardhi za Waislamu kwenye Mkataba wa Fedheha na Aibu, Wakiinamisha Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza Hashem chini ya Usimamizi na Ukoloni!

“Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha alfajiri ya Jumanne mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Ukanda wa Gaza baada ya kuidhinisha rasimu ya azimio lililowasilishwa na Marekani na kuunga mkono mpango wa amani wa Trump katika sekta hiyo, na Rais Trump aliisifu kura ya Baraza la Usalama kuhusu azimio la Gaza kama wakati wa kihistoria...” (BBC, 18/11/2025). Kuhusu Azimio Nambari 2803, lilichapishwa na vyombo vya habari na lilikuwa ni idhini ya mpango wa pointi 20 wa Rais Donald Trump wa kukomesha mzozo mjini Gaza, lililotolewa mnamo tarehe 29 Septemba 2025.

Waislamu Maskini Wanastahili Zaidi Uwekezaji wa Watawala Wapumbavu Kuliko Amerika

Mfalme Mtarajiwa wa Saudi Arabia alifanya ziara nchini Marekani mnamo Jumanne, 18/11/2025, ambapo alionyesha kiwango cha upumbavu wake katika kufuja utajiri wa Ummah, kiwango cha utiifu wake kwa bwana wake Amerika, pamoja na kiwango cha usaliti wake kwa Ummah wa Kiislamu, njama yake dhidi yake, na vita vyake dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) kwa kukubali kujiunga na Makubaliano ya Abraham, yaliyowekwa katika usaliti mwingine ambao unahakikisha njia iliyo wazi ya suluhisho la dola mbili.

Je, Watoto Wafungwa Katika Magereza ya Uvamizi ni Watoto au Wanaume?!

Taasisi za Palestina zinazohusika na masuala ya wafungwa, ikiwemo Klabu ya Wafungwa, zilisema kwamba zaidi ya watoto 1630 kutoka Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na al-Quds, na makumi kadhaa kutoka Ukanda wa Gaza wamekamatwa na uvamizi tangu mwanzo wa vita dhidi ya Gaza. Waliashiria kuuawa shahidi kwa mtoto mmoja ndani ya Gereza la Megiddo baada ya kukabiliwa na njaa, kunyimwa, na unyanyasaji. 350 kati yao bado wako katika magereza ya uvamizi, wakiwemo wasichana wawili, katika hali ngumu ambazo zinagongana kabisa na viwango vyote vya kimataifa vya ulinzi wa watoto. Wanakabiliwa na uhalifu wa mateso, njaa, na kupuuzwa kimatibabu, vilevile kudhulumiwa kijinsia, pamoja na kutengwa kwa pamoja na kunyimwa kutembelewa.

Ukosefu wa Masuluhisho ya Kudumu kwa Mgogoro wa Rohingya

Gazeti la ‘South China Morning Post’ liliripoti mnamo tarehe 10 Novemba kwamba Umoja wa Mataifa umeonya kwamba Kusini-mashariki mwa Asia kuna hatari ya “janga jengine la kibinadamu” ikiwa uvukaji wa bahari wa wakimbizi waliokata tamaa utaendelea bila kudhibitiwa. Vifo vya watu wasiopungua 21, wakiwemo watoto kadhaa, katika ajali ya boti karibu na pwani ya Malaysia vimeibua hofu ya kuongezeka tena kwa uvukaji hatari wa bahari wa wakimbizi wanaokimbia mzozo nchini Myanmar na hali mbaya katika nchi jirani ya Bangladesh. Kulikuwa na miili 12 iliyopatikana nchini Malaysia na tisa katika nchi jirani ya Thailand – kulingana na mkuu wa eneo wa shirika la bahari la Malaysia, Romli Mustafa.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu