Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 563
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Vichwa Vikuu vya Toleo 563
Vichwa Vikuu vya Toleo 563
Katika hatua inayotarajiwa, kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, Mohamed Hamdan Dagalo, alikula kiapo cha kikatiba kama mkuu wa Baraza la Rais la kile kinachoitwa serikali sambamba huko Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini, mnamo Jumamosi, 30/8/2025. Makamu wa Rais, wajumbe wa Baraza la Rais, na Waziri Mkuu pia walikula kiapo.
Sisi katika Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan, tunafuraha kuwaalika ndugu zetu wanahabari, wanasiasa, na wale wenye hamu na mambo ya umma kuhudhuria na kushiriki katika kikao cha kila mwezi cha kadhia za Umma, ambapo mwezi huu kichwa chake ni: Mpango wa Amerika wa Kuitenganisha Darfur... Na Jinsi ya Kuutibua.
Miaka minne iliyopita, mnamo 31 Agosti 2021, uvamizi wa kijeshi wa miongo miwili wa Afghanistan na vikosi vya Amerika na NATO ulimalizika, kwani mwanajeshi wa mwisho wa Amerika aliondoka nchi humu usiku wa manane. Hii ilikuwa hasa kwa sababu ya mhimili wa Wamarekani kuelekea Indo-pacifiki, kupunguza kasi ya maendeleo ya China. Nchi za Kiislamu, hususan Mujahidina wa Afghanistan walikuwa wamewaumiza kichwa Wamarekani na kukengeushwa na mkakati huu mpya. Tunatoa pongezi zetu kwa mafanikio haya ya kihistoria na siku kuu kwa Waislamu wote, hasa kwa watu wa Afghanistan, wabebaji Dawah, na Mujahidina.