Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 582
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Vichwa Vikuu vya Toleo 582
Vichwa Vikuu vya Toleo 582
Mwaliko wa kushiriki katika kisimamo cha izza kilichoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia ili kuadhimisha kumbukumbu ya mapinduzi chini ya kauli mbiu “Mapinduzi Yanaendelea... Kuelekea Khilafah Rashida,” mnamo Jumatano, 14 Januari 2025, katika Barabara ya Al-Thawra.
Kutokana na utaifa, ukabila na kuanzishwa kwa dola za kitaifa na mipaka yake katika ardhi za Waislamu, kitambulisho cha Waislamu kimeharibika na kutengana, ambapo Ummah wa Kiislamu hapo awali uliunganishwa katika udugu mmoja na ndani ya Dola moja ya Kiislamu, badala yake ukagawanyika katika dola za kitaifa zaidi ya 50 na vitambulisho vya kitaifa kufuatia kuvunjwa kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab, 1342, mikononi mwa Mustafa Kamal, “baba wa udhalifu”.
Tulipokuwa Umma mmoja tofauti na mwingine wowote, dola yetu iliweka Rayah (bendera) yake juu ya maeneo yote; ilikuwa mlinzi, kimbilio, na kizuizi dhidi ya yeyote ambaye angeweza hata kufikiria kumshambulia Muislamu mmoja. Waislamu walikuwa mwili mmoja, wakisaidiana kwa ushindi, msaada, na kuimarishana. Iwapo kiungo kimoja kingelalamika, mwili uliobaki ungejibu kwa kukesha na homa. Kisha maadui walielewa kwamba umoja huu na dola hii ndio sababu ya nguvu ya Umma wa Kiislamu na ngao yake ya kinga. Kwa hivyo walianza kulenga ngao hiyo, wakijaribu kuivua, wakifanya juhudi kubwa kwa miaka mingi mirefu hadi walipofikia lengo lao, kwa masikitiko, na kuivunja Dola ya Khilafah mnamo 1924, wakiuchana Ummah wa Uislamu vipande vipande ili kuizuia kurudi katika hali yake ya zamani.