Jumamosi, 26 Ramadan 1442 | 2021/05/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hatari za Muundo Mpya Mpana wa Usalama wa Pakistan

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Wiki chache zilizopita, Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan kwenye Mazungumzo ya Usalama ya Islamabad: Pamoja kwa Mawazo 2021 alisisitiza haja ya muundo mpya wa usalama unaojulikana kama muundo mpana wa usalama. Alisema, "Watu wanadhani kwamba ikiwa tutaimarisha tu vikosi vya jeshi na usalama, ingetosha kwa usalama wa kitaifa. Usalama wa Kitaifa leo unajumuisha mambo mengi ambayo yamepuuzwa katika miongo iliyopita, ikiwemo usalama wa hali ya hewa, usalama wa chakula na ustawi wa kiuchumi”. [1]

Maoni:

Khan aliungwa na Bajwa ambaye alizungumza juu ya haja ya kupanua fahamu ya usalama wa kitaifa kuwa "kutoa mazingira mazuri ambayo kwayo matarajio ya usalama wa binadamu, maendeleo na ukuaji wa kitaifa yanaweza kutekelezwa". [2] Kuondoka kutoka katika usalama wa jadi unaozingatia serikali kujumuisha usalama ambao sio wa jadi ni juhudi ya Bajwa-Khan kurekebisha usalama wa kitaifa wa Pakistan kulingana na uchumi wa kijiografia badala ya siasa za kijiografia.

Wakati wa Vita Baridi, usalama wa jadi — ambapo ukiritimba wa mamlaka ya dola uliotegemewa na jeshi ulitoa usalama wa ndani na nje — uliathiri uhusiano baina ya dola. Wasiwasi mkuu wa usalama wa jadi ni ulinzi na uzuiaji, na kusambaza tena nguvu kati ya dola kufikia usawa (amani) na kupunguza vita. Tofauti nyingine ni kwa dola kuongeza nguvu ya kutosha kutawala mfumo wa kimataifa na kuushinda udhaifu. Zaidi ya hayo, uelewa wa Magharibi wa usalama wa jadi umetokana na mtindo wa Westphalian wa karne ya 17 na utaifa wa karne ya 19. Usalama wa dola unategemea nguvu za kijeshi ambazo zinapanuka hadi kwenye mipaka iliyowekwa ya dola. Amani hupatikana kupitia mizani ya mfumo wa mamlaka na utaratibu wa kimataifa ni wa uwingi.

Fahamu ya Kiislamu ya usalama inatofautiana na wazo la Kimagharibi la usalama wa jadi. Katika Uislamu, usalama unahusu kulinda utukufu wa Sharia ndani ya mipaka ya dola ya Kiislamu, na nje kati ya dola ya Kiislamu na dola zisizo za Kiislamu. Usalama wakati wote lazima uwe mikononi mwa Waislamu. Ndani, usalama unajumuisha ulinzi wa haki kwa raia wote - bila kujali Waislamu na wasio Waislamu. Kwa kuwa mipaka ya dola haikufungwa kuwa maalumu, usalama unaendelea kubadilika ili kuhakikisha utukufu wa Sharia. Nje, usalama unahusu kuwezeshwa kwa upanuzi wa Uislamu kupitia da'wah na jihad. Mfumo kwa kiulimwengu wa Kiislamu sio ya uwingi wala hautumii mizani ya mfumo wa mamlaka ili kutimiza amani. Katika Uislamu, ulimwengu umegawanyika katika Dar Islam na Dar Harb. Amani inapatikana kupitia kujisalimisha kwa Sharia au kupitia utekelezaji wa mikataba inayoongozwa na hukmu za Sharia kwa dola ambazo si za Kiislamu.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisimamisha Dola ya kwanza la Kiislamu mjini Madina — ambapo usalama ulihakikisha utekelezaji wa sharia, hata wakati mipaka ilipo badilika. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alihakikisha kuwa usalama unatosha kutekeleza sheria za Kiislamu na kulinda haki za raia na ushindi wa Khaybar na Makka, na pia pamoja na mikataba iliyofanywa kati ya makabila ya Kiarabu yanayoishi karibu na Himaya ya Kirumi. Abu Bakr na Omar (Mwenyezi Mungu awawie radhi) hawakufanya mikataba na Warumi na Wafursi ili kunali usawa katika eneo hilo. Kinyume chake, serikali changa ya Kiislamu mjini Madina ilipigana na dola mbili hizo kuu kwa wakati mmoja ili kuhakikisha utukufu wa mfumo wa kiulimwengu wa Kiislamu. Makhalifa ambao waliendelea baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) walifuata Sunnah yake kuhusiana na usalama.

Baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti mnamo 1991, wasomi wa Kimagharibi walitilia shaka sifa za usalama wa dola na badala yake, walitetea usalama wa binadamu unaoungwa mkono na ushirikiano kama njia ya kuandaa uhusiano kati ya dola tofauti tofauti. Mnamo 1994, UN ilitangaza nguzo mbili kuu za usalama wa binadamu: uhuru kutokana na hofu na uhuru kutokana na uhitaji. [3] Uhuru kutokana na hofu kimsingi unazingatia uzuiaji wa vurugu na hivi majuzi umeamua kutoboa ubwana wa dola ili kulinda raia. Hii imezaa fahamu ya uingiliaji wa kibinadamu na jukumu la kulinda (R2P). Uhuru kutokana na uhitaji unahusu kupeana nafasi ya ufikiaji wa huduma zinazowezesha uhifadhi wa maisha kama vile elimu na huduma ya afya. Kwa kuongezea, UN iliainisha sehemu kadhaa muhimu za usalama wa binadamu, ambazo ni pamoja na usalama wa kiuchumi, usalama wa chakula, usalama wa afya, usalama wa mazingira, usalama wa kibinafsi, usalama wa jamii na usalama wa kisiasa. [4]

Kwa uhalisia usalama wa binadamu (usalama usio wa jadi) sio jumla kwa wote kama unavyoshikiliwa na wafuasi wake. Umejengwa juu ya Uliberali wa Kimagharibi na unakuza maadili ya kisekula. Bajwa-Khan wanataka kupanua usalama wa kitaifa wa nchi hiyo ili kujumuisha usalama wa binadamu ambao utafanya masuluhisho huria na maadili ya Kimagharibi sehemu muhimu ya muundo mpana wa usalama wa Pakistan. Kwa mfano, usalama wa kiuchumi unatilia mkazo sana sera huru mamboleo zilizowekwa na Itifaki ya Washington. Amerika na India zitatumia sera hizi kuingilia wazi uchumi wa Pakistan kwa kisingizio cha ujumuishaji wa kieneo.

Katika Uislamu hakuna fahamu wa usalama wa binadamu uliotabiriwa juu ya uliberali. Uislamu hulinda maisha ya mwanadamu, akili, utu wa kibinadamu, mali ya kibinafsi, dini, na tabaka kwa raia wake. Sharia ya Kiislamu inatosha zaidi kuhakikisha haki za wanadamu wote, bila kujali mahali na wakati. Kwa mfano, kujumuisha kwa Pakistan usalama wa chakula kama sehemu ya muundo mpana wa usalama kunakusudiwa kupunguza uhaba wa chakula. Lakini, hili ni jeraha la kujitakia. Hapo zamani, Pakistan ilisafirisha vyakula vikuu ili kupata pesa za kigeni kushughulikia deni la nje. Hili limeharamishwa na Uislamu. Kwa kuongezea, Pakistan ina mamilioni ya hekta za ardhi ya kilimo isiyolimwa inayomilikiwa na mabwenyenye. Chini ya Uislamu, ardhi ya ukulima isiyolimwa inapaswa kuchukuliwa na dola kulisha idadi ya watu inayokua ya Pakistan.

Vivyo hivyo, Bajwa-Khan wanataka kujumuisha usalama wa kiuchumi kama sehemu ya muundo mpana wa usalama. Hii inamaanisha kuibadilisha Pakistan kuwa kitovu cha uchumi na kujumuisha ujirani kupitia sera za kiuchumi mamboleo. Sera kama hizi husababisha kutegemeana, humomonyoa ubwana wa kiuchumi, na ni faida kwa uchumi wenye nguvu. Ujerumani inafaidika sana na EU, huku nchi ndogo kama Ureno, Ugiriki, Italia na Uhispania zinaendelea kuumia kiuchumi. Wakati huo huo, Amerika na Ulaya zinafaidika zaidi kutokana na utandawazi, ambao huja kwa gharama ya ulimwengu wa tatu. Jaribio la Pakistan la kutekeleza miradi ya CPEC limeendeleza waziwazi uchumi wa China. Ikiwa Pakistan ingekuwa kitovu cha eneo, India itafaidika zaidi. Chini ya Uislamu, uchumi umehifadhiwa kwa kuharakisha ukuaji wa viwanda katika hatua ya vita ili kutosheleza na kuepuka utegemezi kwa nchi ambayo inaweza kuwa adui katika siku zijazo. Mgogoro wa Covid-19 unaonyesha kwa usahihi jambo hili — nchi zinaondoa minyororo yao ya usambazaji ili kuzihamisha ufuoni na hivyo kudhamini kujitosheleza.

Jamii ya kimkakati ya Pakistan lazima ipinge muundo mpya wa usalama kwa usalama wa kitaifa wa nchi hii. Jamii ya kimkakati lazima ifanye kazi kufichua makosa katika mipango ya Bajwa-Khan na kuhakikisha kuwa usalama wa kitaifa wa Pakistan unalingana na Uislamu ambao unalinda ubwana wa Ummah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti

Marejeo

[1] The Express Tribune, (2021). PM launches advisory portal on national security, [Online] The Express Tribune. Available at: https://tribune.com.pk/story/2289885/pm-launches-advisory-portal-on-national-security
[2] Bajwa, Q. (2021) Read: Full text of Gen Bajwa's speech at the Islamabad Security Dialogue. [Online] Dawn. Available at: https://www.dawn.com/news/1613207
[3, 4] United Nations Development Programme, (1994).HUMAN DEVELOPMENT REPORT 1994. Publisher (New York: Oxford University Press). Available at: http://hdr.undp.org/sites/default/files/reports/255/hdr_1994_en_complete_nostats.pdf

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu