Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Youm-e-Istehsal Kashmir (Siku ya Unyonyaji)

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri Mkuu Imran Khan na Mkuu wa Wanajeshi (COAS) Jenerali Qamar Javed Bajwa mnamo Alhamisi walitoa wito kwa India juu ya kuendelea kwake na "uzingiraji katili wa kijeshi" na "dhulma isiyo na kifani" katika Kashmir iliyokaliwa. Kukemea kwao kulijiri wakati ambapo nchi ilitekeleza Youm-e-Istehsal Kashmir (Siku ya Unyonyaji) kutimiza miaka miwili tangu New Delhi ilivue bonde hilo uhuru wake wa maamuzi. (https://www.dawn.com/news/1638926)

Maoni:

Siku nyingine tena imeongezwa kwenye jumla ya siku zinazotakiwa kuzingatiwa kuhusu Kashmir wakati utawala wa Imran Bajwa unapotekeleza Youm e Istehsaal mnamo 5 Agosti 2021, juu ya India kuendelea na uzingiraji katili wa kijeshi mnamo 5 Agosti 2019. Inatokea katika wakati ambapo Wahindi washirikina wameipoteza Kashmir kisiasa na kisaikolojia na kile kilichobakia mikononi mwa Modi, ni ukandamizaji wa kinguvu kupitia vikosi zaidi ya milioni moja vya India na bado hawajawezi kuwatuliza Waislamu wa Kashmir waliodhulumiwa.

Hapa utawala wa Imran Bajwa unapuuza kwa makusudi baadhi ya hoja kama kumsaidia Modi kwa kupiga soga tupu, serikali lazima izingatie kuwa hata ikiwa mtu atasimamisha harakati za kuvuka mpaka hadi mpaka za mujahideen kwa kupitia misako na kukomesha kila msaada wa fedha wa Jamaa za watu wa Kashmir wanaoishi Pakistan, mtu hawezi kuchukua nchi yoyote au mahali popote ikiwa watu wanaoishi huko hawataki hata kwa shubiri moja kumkubali mkandamizaji, pili ikiwa serikali ya Imran Bajwa kikweli inataka Kashmir iwe huru kutoka kwa ukandamizaji wa India basi mtu ni lazima atambue ukweli kwamba hakuna mkandamizaji atakayetoa uhuru kama zawadi; lazima mtu auchukue kwa nguvu, ambayo kwa sasa serikali hii inaifuta kwa makusudi, licha ya kuwa na nguvu ya kufanya hivyo kama tulivyoichukua AJK mnamo 1948. Na tatu kama ndugu wa Kiislamu ni jukumu letu la Kiislamu kuwasaidia ndugu zetu na dada zetu Waislamu na kumkomesha mkandamizaji kwa nguvu. Na hata ikiwa serikali hii inatii kile kinachoitwa UNO, UN inawakuruhusu kuwasaidia watu wa Kashmir kwa kila njia lakini kwa amri ya Amerika, serikali ya Pakistan imeyafunga majeshi badala yake kuwatumia dhidi ya Waislamu wenye ikhlasi nchini Pakistan wanaolingania utekelezaji wa Khilafah. Na mwisho kabisa sasa China pia inahusika katika eneo hilo kwa hivyo sasa wachezaji walioko wameongezeka kwa hivyo ikiwa serikali hii ina ikhlasi basi wana machaguo ya kutosha ya kivitendo ya kuyafanya na kuikomboa Kashmir badala yake kukaa kimya cha mhalifu na kujifanya kama tu watazamaji inapokuja wakati wa kutoa jibu linalofaa kwa Modi kwa sababu tu Amerika ndivyo inavyotaka. Na kwa kusema tu kwamba Wahindi wananyanyasa, Wahindi wanaleta machafuko nchini Pakistan kupitia Afghanistan, Wahindi walikuwa nyuma ya APS au uwasilishaji hati kwa UNO hakutasaidia jambo hilo kwani ukandamizaji unaweza kukomeshwa tu kwa nguvu sio kupitia miito au kuomba msaada, sisi sote tunajua ni kipi wanachoweza kupata ombaomba katika ulimwengu huu.

Imekuwa zaidi ya siku 730 za uzingiraji katili wa India kwa Kashmir na katika kipindi hiki uonevu wa Washirikina unafikia mipaka yake. Maelfu ya ndugu na dada wa Kiislamu wameuawa mashahidi, maelfu ya dada zetu wamechafuliwa heshima yao, ulimwengu mzima unashuhudia unyama huu wote lakini bado unampendelea dhalimu na kwa wakati kama huo badala ya kuchukua hatua za kivitendo za kuikomboa Kashmir serikali hii imeongeza siku nyingine kwa kusherehekea. Miito, midahalo na mazungumzo hayatafanya chochote isipokuwa kuongeza ukandamizaji wa kikatili wa utawala wa Modi. Katika mpangilio wa ulioko sasa, India imezindua dhidi ya Pakistan: vita vya kisaikolojia, vita vya kisiasa, vita vya kizazi cha nne na vita vya kijeshi, na je tunafanya kujibu? Tunalegeza hata msimamo wetu wa kimsingi, badala yake katika nyakati za hivi karibuni serikali hii imelazimisha simulizi kwamba maswala kama Kashmir yanaweza kutatuliwa tu kupitia mazungumzo. Ni simulizi ya batili; hakuna suala kama hilo katika historia lililotatuliwa kupitia mazungumzo mwisho wa siku ni upanga ndio unaotatua suala hilo. Hata nchini Afghanistan, Amerika ililazimika kufanya mazungumzo na wapiganiaji uhuru wakati Amerika iliposhindwa vita virefu zaidi katika historia mikononi mwa mujahedina wachache.

Utawala ulioko sasa hauwezi kufanya chochote dhidi ya washirikina kwa sababu wameifunga mikono yetu kwa makusudi kupitia kujihusisha katika IMF, mpango wa Benki ya Dunia na kuweka shinikizo bandia kwa taifa kwa ajili ya FATF kwa faida za kidunia. Kashmir inaweza tu kukombolewa kupitia Jihad pekee ikiongozwa na vikosi vyetu vya Wanajeshi simba wanaotamani kukata vichwa vya washirikina hao. Ni chini ya Khilafah pekee majeshi yetu ndipo yatapokwenda huko Srinagar na kuikomboa Kashmir kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt).

Katika wakati ambapo udhalimu ni ufisadi kamili na wahasiriwa hawawezi kufanya chochote hawana usaidizi, nusra kutoka kwa Mwenyezi Mungu (sw) inakuja, hakuna ushindi mkubwa na mabadiliko makubwa yaliyokuja bila ya kipindi hiki, ambapo udhalimu huhisi kwamba mimi ndiye bwana na ninaweza fanya kila kitu na masikini wanasema hakuna aliyeko wa kutusaidia. Masikini hawawezi kufanya chochote isipokuwa kuinua mikono yao "YA ALLAH," nusra itakuja katika kipindi hiki na ndugu na dada zangu wapenzi wakati ni wao. Huu ndio wakati wa kuinua kiwango chetu na kufanya kazi kwa bidii zaidi ya hapo awali ili kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mohammad Adil

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu