Jumatatu, 05 Ramadan 1444 | 2023/03/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uislamu na Waislamu Wataendelea Kuteseka Bila kujali Nani Ameshinda au Ameshindwa kwenye Uchaguzi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wakenya mara kwa mara wanatazama mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kawaida na kujaribu kutafakari ishara mchanganyiko kuhusu ni nani anayeweza kuwa Rais wao mpya. Naibu Rais William Ruto na kinara wa Upinzani Raila Odinga wanafuatana unyo unyo. (The Star, 13/8/2022).

Maoni:

Hivi sasa Kenya kama shamba la wakoloni inazama katika taharuki ya kisiasa kutokana na kuchelewa kutangazwa kwa mshindi wa urais. Mawakala wa kisiasa wanaowakilisha miungano shindani ya kisiasa wanatupiana tuhuma za wizi wa kura. Uhalisia juu ya uongozi wa Kenya yaani miundo ya kisiasa na kijeshi imefungwa minyororo na bwana mkoloni Uingereza. Kwa hivyo, sera zake za ndani na nje zinachorwa jijini London na kutekelezwa jijini Nairobi. Hivyo basi, uchaguzi ni mapambo tu ya kisiasa yanayotumiwa na bwana wa kikoloni kuwapa nguvu wasimamizi wa shamba lake.

Kwa hivyo, ni jambo la kushangaza kwa Waislamu kusherehekea kushinda au kushindwa kwa mgombea fulani haswa katika ngazi ya urais. Kwa kuwa, kuanzia mwanzo, chaguzi hizi za kidemokrasia ni haramu kwetu Waislamu kushiriki katika ngazi yoyote ile yaani kuanzia ngazi ya Wadi hadi Urais. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِ﴿

“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu” [Yusuf: 40]. Uharamu huu unatokana na ukweli kwamba tunachagua watu wa kwenda kutuwakilisha katika kutunga sheria na utawala kinyume na maamrisho ya Shari’ah ya Kiislamu.

Baya zaidi watawala hao mawakala wa kikoloni wanaapishwa kuwa maadui wa wazi wa Uislamu na Waislamu. Uadui wao unathibitishwa na sio tu matamshi yao bali na vitendo vyao. Wanapitisha na kutabikisha sheria na sera zilizoidhinishwa na wakoloni zinazolenga Uislamu na Waislamu kwa kisingizio cha kupiga vita misimamo mikali na ugaidi. Mfano mzuri ulikuwa mwaka wa 2008 wakati Raila Odinga - Waziri Mkuu wa wakati huo na William Ruto - wakati huo akiwa Waziri wa Kilimo na baadaye Elimu wote walikuwa sehemu ya serikali ya mseto iliyoongozwa na marehemu Rais Mwai Kibaki. Ilikuwa ni chini ya uongozi wao ambapo Sheria ya Kupambana na Ugaidi ilipitishwa na kuimarishwa zaidi katika miaka iliyofuata chini ya uangalizi wao.

Ripoti za hivi punde zinathibitisha kwamba kuna ongezeko la idadi ya Waislamu wanaohangaishwa na kukabiliwa na mauaji yaliyokiuka sheria. Isitoshe, wengine wanaangamizwa kiuchumi na vyombo vya usalama vya dola kufunga akaunti zao za fedha na utajiri wao kuekewa vikwazo! Baya zaidi kwa Waislamu, ni kuzinduliwa kwa makao makuu ya Kitengo cha Polisi wa Kupambana na Ugaidi (ATPU) jijini Mombasa mnamo tarehe 20 Julai 2022. Jumba hilo la kisasa la ATPU lenye thamani ya Sh81 milioni lilifadhiliwa na serikali ya kikoloni ya Uingereza. Fauka ya hayo, Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Jane Marriott, alisema Kenya ni mshirika mkuu wa usalama wa Uingereza katika Afrika Mashariki. Pia alisema ugaidi ni mojawapo ya matishio makubwa zaidi yanayoikabili Kenya na Uingereza, na kwa hivyo, ili kupambana na tishio hili, Uingereza itaendelea kufadhili juhudi za Kenya za kupambana na ugaidi kwa Sh1 bilioni kila mwaka! (The Star, 20/7/2022).

Inasikitisha kuona Waislamu wakijifanya mithili ya mbuzi wanaowakaribia ‘mbwa mwitu’ kuliwa, kwa jina la kuwasherehekea wanasiasa wa kidemokrasia ambao ndiyo sababu ya maisha yao mabaya. Kwa upande mwengine, kuufumbia macho muongozo wa Kiislamu, unaolingania kushikamana imara na Shari’ah ya Kiislamu yaani kutoridhika chini ya utawala wa Kikafiri unaoongozwa na Makafiri. Hakika, Waislamu wanaoishi katika tawala za kidemokrasia ni vipofu; ISIPOKUWA ikiwa wanafanya kazi usiku na mchana ili kuondoa hali halisi iliyopo na kuibadilisha kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu, Khilafah itakayosimamishwa tena kwa njia ya Utume.

Khilafah ndio tumaini letu pekee la kweli, ngao na mlinzi wa Uislamu na Waislamu, mali yetu, damu yetu na heshima yetu. Kukosekana Khilafah kumetufanya sisi Waislamu kuwa mayatima, ambao kila mjinga anaweza kuwakejeli! Ni lazima tukumbuke kwamba matumaini yetu ya maisha ya amani na mafanikio katika dunia hii ya mapito na akhera yako katika Khilafah. Kwa hiyo, ni lazima tuwe sehemu ya Hizb ut-Tahrir na kuongeza juhudi zetu maradufu kama Umma Mmoja unaolingania Dola Moja inayoongozwa na Khalifah Mmoja. Utukufu wa ardhi zetu utaregeshwa na maadui wa Uislamu na Waislamu watapigwa vita na wamwagaji damu za Waislamu watalipizwa kisasi InshaAllah. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ﴿

“Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.” [3. Aali-Imran: 9]. Dunia nzima iko katika machafuko, kiongozi wa ulimwengu, Amerika anayeitwa kinara wa demokrasia inakaribia kuporomoka. Musichelewe kuchukua fursa hii nzuri ya kufanya kazi kwa ajili ya Khilafah ijayo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu