- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ili Kupata Mabadiliko Halisi, Achaneni na Demokrasia na Itisheni Nusra kwa ajili ya Khilafah
(Imetafsiriwa)
Habari:
Vikao vya mahakama moja ya wilaya ya Islamabad 17 Agosti 2022 iliidhinisha kuwekwa rumande kwa siku mbili kwa kiongozi wa PTI, Shahbaz Gill, kwa ombi la polisi wa mji mkuu. Hakimu pia alielekeza afisa wa upelelezi, kupanga uchunguzi wa matibabu wa Bw. Gill, na kuwasilisha ripoti kwa mahakama hiyo.
Maoni:
Bw. Shahbaz Gill ni Mkuu wa Majeshi wa Imran Khan, Waziri Mkuu wa zamani na mwenyekiti mwanzilishi wa chama cha Pakistan Tahreek-i-Insaf (PTI). Amekuwa mmoja wa wafuasi wa Imran Khan. Bw. Gill anajulikana vyema kwa lugha ya matusi dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa, chama cha Pakistan Democratic Alliance (PDM). Alikamatwa mnamo 9 Agosti 2022, kwa matamshi yake, ambapo alidai kuwa alichochea cheo na faili ya jeshi, kukataa maagizo ya amri ya kijeshi ya Pakistan, ambayo inatawala Pakistan kivitendo.
Tangu kukamatwa kwa Bw. Gill, ni dhahiri kabisa kwamba PTI na mwenyekiti wake mwanzilishi, Imran Khan, wako chini ya shinikizo kubwa. Tangu kukamatwa huku, PTI inajitenga na msimamo wa Bw. Gill. PTI imepunguza wazi usemi wake dhidi ya "wasio na upande wowote," ndani ya uongozi wa kijeshi.
Udhibiti unaoendelea wa chama cha kisiasa sio jambo geni katika siasa za Pakistan. Ingawa, vyama vyote vya kisiasa nchini Pakistan vinaunga mkono Amerika, mara kwa mara vinanyoosha mbawa zao, zaidi ya dori ambayo uongozi wa kijeshi umevifafanulia. Wakati wowote chama chochote cha kisiasa kinapofanya hivyo, uongozi wa kijeshi, kwa baraka za Amerika, hukata manyoa yake, kwa ima kukomesha utawala wao, au kuondosha uongozi wao mkuu, au kuulazimisha uongozi wao kwenda uhamishoni. Hii imetokea kwa chama cha Pakistan People’s Party (PPP) na Pakistan Muslim League-Nawaz (PML-N), mara nyingi. Kwa hivyo historia inarudiwa leo nchini Pakistan, kwa mara nyingine tena. Wakati huu mlengwa ni PTI.
Katika Demokrasia, hakuna chama cha kisiasa kinachoweza kwenda kinyume na matakwa ya Marekani, kwa sababu uongozi wa kijeshi mtiifu kamili kwa Washington. Hata kama chama kitaingia madarakani kwa wingi wa thuluthi mbili, hakitawahi kutenda bila ya kujali maslahi ya Marekani. Huko nyuma tuliona kung'olewa kwa tawala ambazo zimekuwa na theluthi mbili ya kura kwenye bunge la taifa. Kwa hivyo, yeyote anayefikiri kwamba chama chao cha kisiasa kinaweza kupata kura nyingi katika Demokrasia, kupata uhuru kutoka kwa wakoloni, kwa bahati mbaya amekosea sana.
Ili kuleta mabadiliko halisi, lazima tuachane na Demokrasia, ambayo daima ni farasi wa Amerika, bila kujali mwendeshaji wake. Ni lazima tufuate Njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa ajili ya mabadiliko. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alifanya kazi katika ngazi tatu, kuleta mabadiliko ya kina, umati, wenye ushawishi na watu wenye nguvu. Mjini Makkah, daraja tatu hazikukubaliana na Uislamu. Badala yake watu wenye nguvu walimpa ofa Mtume (saw) kushiriki katika mfumo wao wa kikafiri, ambao aliukataa kata kata. Kinyume chake, mjini Madina, watu wenye nguvu walitoa Nusrah yao ya usaidizi, kupitia Ahadi (Bay’ah) ya Pili ya Aqabah, ikiruhusu utabikishaji kamili wa Uislamu, bila ya kulegeza msimamo au utabikishaji wa hatu kwa hatua.
Kwa hiyo nchini Pakistan au katika sehemu nyengine yoyote ya ulimwengu wa Kiislamu, mabadiliko halisi, utabikishaji kamili wa Uislamu, unaweza kutokea tu wakati watu wenye nguvu, majeshi, watakapotoa Nusrah kwa wale watakaoisimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Hebu na tuachane na Demokrasia na tuombe kutoka kwa majeshi Nusrah yao kwa Hizb ut Tahrir.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan