Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Manifesto za Vyama: Hali ni ileile Kamwe Haitobadilika kwani Uislamu Umetupiliwa Mbali!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mbio za kumsaka raisi wa serikali ijayo zimeshika kasi ikiwa tayari wagombea wa wadhifa wa urais, walioidhinishwa na tume ya usimamizi wa uchaguzi wakizindua rasmi manifesto zao kwa ajili yakupata kura za uchaguzi wa Mwezi Agosti 09. Raila Odinga anayewania kwa mara ya tano kiti cha urais, alizindua manifesto yake mapema mwa mwezi Juni ambayo kimsingi imejikita katika mabadiliko ya kiuchumi kwa kupitia uenezwaji wa viwanda. Akiahidi kuwa kila Gatuzi katika magatuzi yote 47 kuweko na kiwanda cha uzalishaji. Mpinzani wake wa karibu naibu rais William Ruto ambaye kwake ni mara ya kwanza kugombea urais alizindua manifesto yake mnamo Juni 30. Manifesto yake nayo imejikita kwa misingi mitano ikiwemo: kufufua uchumi wa nchi kupunguza gharama za maisha, kuimarisha hali za vijana. Profesa Wajackoya ameteka masikizi takriban pembe zote za nchi pale alipotaja kwenye manifesto yake kwamba atahalalisha bangi!

Maoni:

Manifesto za vyama vya kisiasa ni ada ya zamani ambapo huweka mkataba wake na wapiga kura. Kama zilivyokuwa manifesto za vyama vya kisiasa vya miaka ya nyuma, manifesto zilizozinduliwa hazina chochote kipya katika Aidilojia. Wanasiasa wa Kidemokrasia ama vyama wana hulka ya kutoa ahadi zisizo kuwa na sura wazi bali hujaza masuala ambayo serikali zote zilizopita hazikuweza kuzitekeleza. Kwa mfano utawala wa sasa unaoondoka wa Jubilee kwenye manifesto yake uliahidi kubuni nafasi za kazi milioni 1.3 kila mwaka kwa vijana wasokuwa na kazi lakini wapi! Ilikuwa ni ahadi tupu. Uhalisia wa mambo ni kwamba Kampeni za Demokrasia zinadhaminiwa na mabwenyenye mabepari wanaohonga wapiga kura kama chambo na kuwapata mawakala wa kisiasa ambao wakichaguliwa wafanye kila wawezavyo kulinda maslahi yao.

Kuhusu suala la uhalilishwaji wa bangi, hii inaonesha bayana jinsi itikadi ya Kisekula ilivyozalisha wanasiasa wanaotukuza maovu na fikra za kihuni. Kwa kutenganisha Dini na Maisha, usekula umesheheni wanasiasa wanaopelekwa na matamanio na wala sio sharia za Mwenyezi Mungu (Swt).

Yeyote atakayeshinda uchaguzi huu kwa hakika hatobadilishi kimsingi hali ngumu anayokabiliana nayo raia wa kawaida. Hii ni kwa sababu uongozi katika Demokrasia ni urongo na tamaa tu ya kukidhi maslahi ya kibinafsi wala sio kujali maslahi ya watu. Serikali itakayoundwa itajifunga na sera za unyonyaji za mfumo wa Kikoloni wa kirasilimali. Seuze ya hayo, hizi chaguzi za Kidemokrasia hufichua urongo na utapeli uliojikita kwenye kutoa ahadi tupu na kudai kwamba upigaji kura ndio njia ya ya kufikia maendeleo na mabadiliko na mustakabali mwema.

Kwa kuwa manifesto zote hizi zimeweka Uislamu mbali katika ajenda ya mabadiliko, hii ina maanisha kuwa hali itabaki hiyo hiyo wala haitobadilika. Uislamu una mengi ya kutekelezwa kikamilifu na una njia halisi ya kufikia mabadiliko ya kikweli ambayo dunia nzima lazima ijukumike kuufanyia kazi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari  Hizb ut-Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu