Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Amani ya Kudumu Inaweza Tu Kupatikana huko Balochistan kupitia Kuung'oa Mfumo wa Wakoloni na Kusimamisha Khilafah Rashida

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 14 Novemba 2024, Naibu Msemaji Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alitangaza, “Tunalaani vikali shambulizi la Brigedi ya BLA Majeed la Novemba 9 katika kituo cha reli.” (https://www.state.gov/briefings/department-press-briefing-november-14-2024/)

Maoni:

Machafuko katika jimbo la Balochistan si jambo geni. Yamedumu tangu uhuru wa Pakistan kutoka kwa Raj wa Uingereza. Watu wa Balochistan wana malalamiko ya kina, yaliyoachwa bila kutatuliwa na utawala wa kikoloni wa Uingereza na watawala ambao ni vibaraka wa wakoloni wa Magharibi. Mfumo wa wakoloni ulipangwa kuwatiisha Waislamu, badala ya kuangalia mambo yao. Unawanyima haki na unadumisha udhibiti kupitia nguvu za kijeshi.

Katika miaka ya hivi karibuni, Balochistan imeshuhudia mfululizo wa matukio ya vurugu, ikiwa ni pamoja na milipuko ya kujitoa muhanga iliyolenga raia, vikosi vya usalama na raia wa China. Wimbi hili la mashambulizi lilianza Agosti 2018, na mauaji yaliyolenga wahandisi wa China, na kufuatiwa na shambulizi kwenye ubalozi mdogo wa China mnamo Novemba 2018, na shambulizi la bomu katika hoteli ya Gwadar mnamo Mei 2019. Mnamo Aprili 2022, Brigedi ya Majeed ya Jeshi la Ukombozi la Balochistan ilifanya shambulizi la bomu la kujitoa muhanga katika taasisi ya China katika Chuo Kikuu cha Karachi.

Mashambulizi yameendelea hadi 2024, na matukio kama vile shambulizi la msafara huko Balochistan mnamo Machi 26, na shambulizi la wahandisi wa Kichina karibu na Bandari ya Gwadar mnamo Agosti 13, yote yakilenga kuhujumu Ukanda wa Uchumi wa China na Pakistan (CPEC). Mnamo tarehe 26 Agosti, 2024, Jeshi la Ukombozi la Balochistan lilianzisha mashambulizi yake makubwa zaidi kuwahi kutokea, na kuua watu wapatao 73 na kulenga vituo vya polisi, njia za reli, na magari. Hivi majuzi, shambulizi kwenye kituo cha reli cha Quetta liligharimu maisha ya raia wasio na hatia.

Mashambulizi haya yameongezeka tangu Marekani na India kuunda muungano wa kukabiliana na China. Dola zote mbili zinaunga mkono vuguvugu la kujitenga huko Balochistan. Usaidizi huu unaonekana kulenga kuhusisha jeshi la Pakistan ndani ya migogoro ya ndani, kupunguza umakini wake kwenye mpaka na India, haswa katika Jammu na Kashmir. Katika mkakati wake wa kukabiliana na kuinuka kwa China, Marekani imetumia vibaya harakati za utaifa huko Balochistan. Katikati ya mizozo yake ya mpaka na China, India imejaribu kudhoofisha maslahi ya China, kuwiana na malengo ya Marekani. Kwa hivyo, Pakistan imeingizwa katika mzozo wa ndani, haswa huko Balochistan, na zaidi ya wanajeshi 80,000 wametumwa kukabiliana na vikundi vinavyotaka kujitenga.

Serikali inayotawala nchini Pakistan ilipaswa kushughulikia suala la Balochistan, ambayo ni sehemu ya ardhi yake, kwa kuitendea haki, uadilifu na wema kwa mujibu wa Shariah, na kwa kutumia mali ya umma katika ardhi ya Balochistan kwa raia wote wa serikali, wakiwemo Wabaloch. Lakini badala yake, ililichukulia tatizo hilo kama suala la usalama, kwa kuua na kukamata, si kwa uangalizi mzuri kama ilivyo katika Uislamu. Mtume (saw) amesema, «الْإِمَامُ رَاعٍ وَمَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imam ni mchungaji na anawajibika kwa raia wake.” (Imepokewa na Al-Bukhari).

Kadhalika, makundi ya kisilaha ya Balochistan hayakupaswa kuwaruhusu maadui wa Uislamu, Marekani na India, kuwatumia wao vibaya dhidi ya Waislamu, wala yasingefanya kazi ya kulitenga na kuligawanya jimbo hilo, kwani hili ni jambo kubwa katika Uislamu, mhusika wake atachukuliwa kuwa na dhambi kubwa, kwani Waislamu ni Umma mmoja ambao hauwezi kugawanywa.

Umoja wa kweli wa watu wa Pakistan hautaregeshwa isipokuwa kwa kutekeleza hukmu za Uislamu, kueneza fikra ya udugu wa kweli wa Kiislamu, na kutekeleza fikra ya usawa baina ya Waislamu wote katika kunufaika na mapato ya mali ya umma kama vile gesi, madini, nk., hadi dhulma, umaskini, na kutengwa viondolewe kutoka kwa watu Waislamu wa Balochistan na Waislamu wengine. Uislamu umekataa na kuharamisha kabisa hisia za utaifa, na umeanzisha udugu miongoni mwa Waislamu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ وَاتَّقُوا اللهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ]

“Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.” [Al-Hujurat: 10]. Wakati huo huo, udugu huu wa Uislamu lazima uwasukume kufanya kazi pamoja na wanaofanya kazi ili kusimamisha dola yao moja, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, chimbuko la umoja wao, chimbuko la fahari yao, na ukweli wa udugu wao...na huo ndio ushindi mkubwa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zakariya Imran – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu