Jumamosi, 26 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kimbunga cha Al-Aqsa kiko Hai na Kinaendelea

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wapatanishi watia saini makubaliano ya Trump ya kusitisha mapigano Gaza. (Oktoba 13, 2025).

Maoni:

Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa haikuwa tukio la muda mfupi ambalo lilimalizika kwa makubaliano ya mhalifu Trump na dola ya kikafiri nyuma yake, Marekani, muungaji mkono rasmi wa umbile la Kiyahudi. Badala yake, Kimbunga cha Al-Aqsa kilikuwa ni cheche iliyowasha moto ndani ya nyoyo za Waislamu, na kuzifungua akili na nyoyo zao. Waliona unyonge na uovu wa watawala wao wasaliti, na wakatambua unafiki wa wale wanaodai kuwa ni na ubinadamu, na wanaotetea haki za wanawake na watoto. Wakawa na hakika kwamba sheria za kimataifa, na mikataba si chochote ila ni silaha inayotumiwa na makafiri, dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Operesheni hii imefichua kwamba kile ambacho Magharibi kafiri inachokihofia na kuwa na wasiwasi nacho zaidi ni Waislamu kwenda kinyume na matakwa ya Magharibi. Kwa hiyo wamefanya kazi kwa bidii, kwa nguvu zao zote na silaha zao, na kwa vitisho vyao, ukatili na uhalifu wao wote, kuiangamiza Gaza na kuua wanawake na watoto mbele ya macho ya ulimwengu, kwa lengo moja akilini, ambalo ni kukinyonga kiungo hiki kilicho hai ndani ya mwili wa Umma, bila kuzingatia kanuni za hadhara yao wenyewe, ambayo itatoweka hivi karibuni, in shaa Allah.

Kuamka kwa Ummah kunaiogopesha jamii ya kimataifa, na Khilafah ndio wasiwasi wake mkuu. Uthabiti, subira, na Imani katika Mwenyezi Mungu (swt) iliyodhihirishwa na Gaza, licha ya vitisho na mauaji, inaiogopesha zaidi, na inaifanya kutambua kwamba kinachotokea ni hadithi ya izza. Kusimama dhidi ya nguvu imara ni zama kipekee katika njia ya historia.

Ni lazima tutambue kikamilifu kwamba vita dhidi ya Waislamu havitakoma, na kwamba kafiri haoni amani isipokuwa kwa kutokuwepo Uislamu. Kwa hiyo, watafanya kazi kwa mipango na mbinu zote za kutuvuruga na kutukatisha tamaa kwa vita, vitimbi na njama, ili tubaki kuwa Umma uliochanika bila ya azimio. Jambo la faradhi zaidi leo hii ni kufanya kazi kwa bidii ili kujiondolea mfumo huu wa kimataifa na zana zake, kuzikanusha, na kujitolea mhanga katika njia ya kuunganisha Ummah, na kusimamisha Khilafah ya Pili kwa Njia ya Utume, ambayo itahifadhi haki za Waislamu na kulipiza kisasi kwa maadui zao.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sadiq al-Sarari – Wilayah Yemen

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu