Alhamisi, 02 Jumada al-awwal 1447 | 2025/10/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Muungano na Amerika hauruhusiwi kwa Pakistan, wala Muungano na India hauruhusiwi kwa Afghanistan

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri wa Ulinzi wa Pakistan Khawaja Asif mnamo Jumatatu (20 Oktoba 2025) alitupilia mbali madai ya Afghanistan kwamba Islamabad inatenda kwa niaba ya Marekani ili kuunda mabadiliko ya serikali jijini Kabul, akielezea madai hayo kama “upuuzi mtupu”. Islamabad imesema kwa muda mrefu kwamba India, hasimu wake wa muda mrefu, inafanya kazi pamoja na Afghanistan kusaidia Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP), ambayo inajulikana kama Taliban ya Pakistan, na wanamgambo wengine dhidi ya Pakistan. New Delhi inakanusha madai hayo. (Arab News)

Maoni:

Kando na kauli ya Waziri wa Ulinzi, ni wazi kwamba watawala wa Afghanistan wameituhumu Pakistan kwa kufanya kazi kwa niaba ya Marekani, kwa sababu ya muungano wa kiuchumi na kijeshi wa Islamabad na Washington. Kwa upande mwingine, ni wazi kwamba watawala wa Pakistan wamewatuhumu watawala wa Afghanistan kwa kuchukua hatua kwa upendeleo wa India, kwa sababu ya muungano wa Kabul na New Delhi.

Mapigano ya umwagaji damu kati ya Pakistan na Afghanistan, na usitishaji wao dhaifu wa mapigano, ni mzozo mkubwa kati ya Waislamu ambao unaweza kutatuliwa tu kwa kumregelea Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا]

“Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.” [Surah An-Nisaa: 59]. Hivyo tunapata nini tunapomregelea Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw)?

Kwanza, hairuhusiwi kufanya miungano na dola zinazo za kivita. Uhalisia wa Amerika ni kwamba ni dola ambayo inapigana na Waislamu mfululizo, na kusaidia umbile la Kiyahudi katika uvamizi wake wa Palestina na mauaji ya halaiki mjini Gaza. Ama India, inaikalia kimabavu Kashmir na inapiga vita Uislamu chini ya mamlaka yake. Hairuhusiwi kufanya mkataba wa kudumu na dola hizo zilizo za kivita, kivitendo. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Mumtahina 60:9].

Pili, hairuhusiwi kusimamisha mapigano kwa njia ya kudumu, na kuweka makubaliano ya kudumu ya kusitisha vita (hudnah), kwa sababu hii inasitisha Jihad, ambayo lazima iendelee hadi Siku ya Kiyama. Usimamishaji wa kudumu wa vita pia unazuia kuenea kwa Uislamu, hadi Mwenyezi Mungu (swt) aufanye Uislamu utawale juu ya mifumo mengine yote ya maisha. Amesema Mwenyezi Mungu (swt): [وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّهِ] “Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Anfal 8:39], na Mtume (saw) amesema, «وَالْجِـهَـادُ مَاضٍ مُنْذُ بَعَثَـنِي اللَّهُ إِلَى أَنْ يُقَاتِلَ آخِـرُ أُمَّـتِي الدَّجَّـالَ» “Jihad lazima iwe yenye kuendelea tangu aliponitumiliza Mwenyezi Mungu, mpaka mwisho wa Ummah wangu utakapopigana na Dajjal.” [Imepokewa na Abu Dawud kupitia Anas]

Tatu, hairuhusiwi kwa dola ya Waislamu kufanya makubaliano ya kijeshi na dola zengine, kama vile makubaliano ya ulinzi wa pande zote mbili, makubaliano ya usalama wa pande zote, na uwezeshaji wowote wa kijeshi unaohusiana na hilo, kama vile kukodisha kambi za kijeshi, viwanja vya ndege, au bandari. Pia hairuhusiwi kuomba msaada (isti’aanah) kutoka kwa dola za kikafiri na majeshi yao, wala kuchukua mikopo na misaada kutoka kwa dola hizi. Makubaliano haya yameharamishwa na Uislamu. Uislamu umemharamisha Muislamu kupigana chini ya bendera ya ukafiri, au kwa ajili ya ukafiri, au kwa niaba ya dola ya kikafiri, au kumpa kafiri mamlaka juu ya Waislamu au juu ya ardhi ya Uislamu.

Mtume (saw) amewaharamisha Waislamu kutafuta msaada (isti’aanah) kutoka kwa dola za kikafiri, kwa kuwa aliharamisha kutafuta nuru kutoka kwenye moto wa washirikina, kama alivyosema, «لاَ تَسْـتَضِـيئُوا بـِنَارِ الْمُشْرِكِينَ» “Msitafute nuru kwenye moto wa washirikina”. [Imepokewa na Ahmad]. Moto ni kinaya cha vita. Mtume (saw) pia amesema, «فَإِنَّا لاَ نَسْـتَعِينُ بـِمُـشْـرِكٍ» “Hakika sisi hatuombi msaada kwa mshirikina”. [Sahih Ibn Hibban].

Enyi Waislamu wa Pakistan na Afghanistan!

Jueni kwamba bwana wa serikali mbili za India na Pakistan ni bwana Marekani, na Marekani ndiye anayeziamuru na kuzikataza serikali zote mbili kufanya kile kinachotumikia maslahi yake. Kujipanga na au kushirikiana na India au Pakistan kunamaanisha kuanguka katika mtego wa Marekani. Sisi pia hatukubali serikali jijini Kabul kuendelea kuamiliana moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na bwana huyo huyo. Ikiwa hili litaendelea, itakuwa ni ulaji njama dhidi ya Ummah na maslahi yake, sawa na kutii usalimishaji wa kambi ya Bagram unaoitishwa na mfalme wa Marekani, Trump.

Enyi Waislamu wa Pakistan na Afghanistan kwa jumla na hasa maulamaa wao!

Ni juu yetu sote kuwataka watawala wa Afghanistan wakate mahusiano yote na India. Ni juu yetu sote kuwataka watawala wa Pakistan wakate mahusiano yote na Marekani. Ni juu yetu sote kudai utekelezaji wa Dini katika mambo yetu yote. Ni Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume ndiyo itakayounganisha Ummah mzima, na rasilimali zake nyingi, kama dola moja yenye nguvu, itakomboa ardhi zetu zinazokaliwa kwa mabavu na kuwalazimisha maadui zetu kurudi nyuma.

Enyi Maafisa na Wanajeshi wa Jeshi la Pakistan na Mujahidina wa Afghanistan!

Vunjeni upanga wowote utakaoinuliwa dhidi ya Muislamu mwengine. Elekezeni panga zenu zote kwenye Dola ya Kibaniani, umbile la Kiyahudi na mkuu wa makruseda, Amerika. Zichunguzeni nafsi zenu na jiepusheni na masanamu ya ukabila na utaifa, kwani yanakufanyeni kuni za moto wa Jahannam. Azimieni kujisalimisha kikamilifu kwa Dini ya Uislamu, bila ya kutoa visingizio vya kusitisha hukmu yoyote ya Shariah. Toeni nusrah yenu (msaada wa kijeshi) kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Khilafah Rashida itawaunganisha nyote kama kikosi kimoja cha kijeshi ili kuwatia hofu maadui na kuponya nyoyo za waumini.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu