Jumanne, 19 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Shambulizi la Muafghani jijini Washington na Maeneo Yaliyofichwa ya Siasa
(Imetafsiriwa)

Habari:

Shambulizi la silaha jijini Washington, D.C. wiki moja iliyopita—ambapo Rahmanullah Lakanwal, raia wa Afghanistan, anatuhumiwa kuwafyatulia risasi Walinzi wawili wa Kitaifa wa Marekani—lilitokea karibu na kituo cha Metro cha Farragut Magharibi, mita mia chache tu kutoka Ikulu ya White House, eneo ambalo kwa kawaida linalindwa na baadhi ya tabaka kali zaidi za usalama. Kutokana na ufyatuaji risasi huo, Sarah Bäckström, mlinzi wa Kitaifa wa miaka 20, aliuawa na Andrew Wolf alijeruhiwa vibaya.

Maoni:

Ripoti za vyombo vya habari zinaonyesha kwamba hapo awali alihudumu nchini Afghanistan kama sehemu ya kitengo cha operesheni kinachohusishwa na CIA, na kwamba baada ya kuhamishiwa Marekani alipambana na masuala ya kisaikolojia, kutengwa, na shinikizo la kifedha—matatizo ambayo pia yameripotiwa miongoni mwa mali zengine za ujasusi za Marekani. Hata hivyo, utata mkubwa zaidi unabaki: Je, licha ya kukosa idhini ya kubeba silaha, aliwezaje kusafirisha bunduki kutoka jimbo la Washington hadi mji mkuu? Ni nani—au ni utaratibu gani—uliomwezesha kusafiri kwa zaidi ya masaa 30 akiwa na silaha, katika mojawapo ya mazingira salama zaidi nchini Marekani? Na kwa nini shambulizi hilo halikutokea katika jimbo lake la makaazi, bali hasa katika kitovu cha kisiasa cha nchi? Maswali haya yanaunda sehemu muhimu ya mjadala unaoendelea.

1. Uwezekano wa Kuhamisha tena Mali za Ujasusi za Marekani kwenda Afghanistan Chini ya Pazia la “Kuwarudisha Nyumbani Wahamiaji Haramu”

Mgogoro unaotokana na shambulizi hili unaweza kuipa Marekani kisingizio cha kurekebisha shughuli zake za ujasusi kuhusu Afghanistan. Tangu kupoteza ufikiaji wa moja kwa moja kwa vyanzo vya kibinadamu ndani ya nchi baada ya 2021, ongezeko lolote la wasiwasi wa usalama unaohusiana na wahamiaji wa Afghanistan linaweza kuhalalisha mipango ambayo inaonekana kuhusisha “kusimamia wahamiaji haramu,” lakini ambayo kusudi lake lililofichwa ni kurudisha mali shirika za ujasusi au zinazoweza kutumiwa nchini Afghanistan.

Muundo huu una kielelezo: hapo awali, Marekani imetumia faili za uhamiaji, “kurudi kwa khiyari,” au kupelekwa kwa watu waliolengwa ili kujenga upya mitandao yake ya ujasusi. Leo, mazingira ya kisiasa na vyombo vya habari ni kwamba hali mithili ya hiyo—iliyotekelezwa kimya kimya na bila tangazo rasmi—inaonekana kuwa ya kuwezekana, hasa kwa kuzingatia historia ya Lakanwal na unyeti wa kesi zinazofanana. Msingi wa kisiasa wa hatua kama hizo unaonekana kuchukua umbo.

2. Uwezekano wa Upatilizaji wa Hali Baada ya Tukio wa Dola ya Kiyahudi

Huku kukiwa na maandamano ya kiulimwengu kuhusu mwenendo wa dola ya Kiyahudi katika vita vya Gaza, inanufaika na tukio lolote linalohusisha wahamiaji au Waislamu ambalo linaweza kutumika kuimarisha sera za kupinga uhamiaji Magharibi. Kupunguza uwepo au ushawishi wa jamii za wahamiaji na Waislamu barani Ulaya na Marekani kutapunguza shinikizo la kisiasa kwa dola ya Kiyahudi. Inaamini kwamba maandamano yaliyoenea Magharibi dhidi ya mauaji ya halaiki mjini Gaza yanachochewa na Waislamu na wahamiaji. Katika muktadha huu, Israel inaweza kuwa na dori katika matukio kama hayo, kwani kesi ya Lakanwal na matokeo yake—mazingira magumu ya uhamiaji na hofu iliyoongezeka kwa wakimbizi Waislamu—inawiana na maslahi yake.

3. Matumizi Wazi ya Kisiasa ya Trump ya Tukio Hilo

Jibu la Donald Trump na harakati za kihafidhina nchini Marekani limekuwa la moja kwa moja na lisilopingika. Mara moja alitunga shambulizi hilo kama ushahidi wa “hatari ya uhamiaji” na kutoa wito wa kutathmini upya haraka uandikishaji wa wakimbizi. Wakati huo huo, mamlaka za uhamiaji, zikinukuu masuala ya usalama, zilizuia zaidi uhakiki wa kesi za utafutaji hifadhi kwa Waafghanistan na raia wa mataifa mengine.

Ikikabiliwa na kupungua kwa umaarufu, Trump anatumia tukio hili kufufua simulizi inayolenga usalama, kuhamasisha kambi yake ya kihafidhina, na kwa mara nyingine tena kuhalalisha sera za kupinga uhamiaji.

Kwa wengi nchini Marekani, tukio hilo linapunguzwa hadi kuwa suala la uhamiaji pekee, na makundi fulani yameligeuza kuwa chombo cha chuki dhidi ya Uislamu. Hata hivyo ukweli ni kwamba Lakanwal ni zao la miaka mingi ya kushiriki katika misheni hatari na za siri zilizonasibishwa na CIA nchini Afghanistan—misheni zilizomfanya kuwa mtu aliyeathiriwa na vita na vurugu muda mrefu kabla ya kuwa mhamiaji.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yousef Arsalan
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu