- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Watawala wa Pakistan Wanatoa Kile Ambacho Marekani Imekuwa Ikikiota Siku Zote na Kuiondoa Katika Hatari Yake
(Imetafsiriwa)
Habari:
Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza mnamo Jumamosi, Mei 23, 2026, kwamba makubaliano na Iran yalikuwa karibu kukamilika, akisema, “Makubaliano yamejadiliwa kwa kiasi kikubwa, yanakaribia kukamilika.” Aliongeza kwamba alikuwa na “wito mzuri sana” na viongozi na maafisa nchini Saudi Arabia, Imarati, Qatar, Pakistan, Uturuki, Misri, Jordan, na Bahrain kuhusu Iran. Hii ilikuja saa chache baada ya afisa mmoja wa Iran kufichua kwa Al Jazeera kwamba mkataba wa maelewano ulikuwa umefikiwa na mpatanishi wa Pakistan, lakini kwamba Tehran ilikuwa ikisubiri majibu ya Marekani. Afisa huyo aliashiria kwamba Mkuu wa Jeshi la Pakistan Asim Munir alipangwa kutangaza mkataba huo wa maelewano jijini Tehran, lakini alikuwa ameondoka ili kufanya uratibu pamoja na Washington (Al Jazeera Net).
Maoni:
Amerika isingeweza kufikia makubaliano, au hata mfano wake, pamoja na Iran ambayo iliruhusu Marekani kuokoa aibu, kama isingekuwa kwa juhudi zisizochoka za watawala na makamanda wa kijeshi la Pakistan, hasa Waziri Mkuu Shehbaz Sharif na kamanda wa vikosi vya nyuklia vya Pakistan, Field Marshal Asim Munir. Walifanya kazi mchana na usiku, wakisafiri kwenda Tehran kutoa ujumbe wa Marekani, wakitumia ujanja pamoja na nguvu kuilazimisha Iran kukubali makubaliano yoyote na Amerika ambayo yangeiondoa katika hali ngumu ambayo ilikuwa imejitengenezea. Kwa hivyo, pazia linaangukia kwenye sura mpya ya usaliti, iliyorekodiwa katika historia ya utawala wa Pakistan, ambao daima umejiona kama kibaraka mtumwa na mtiifu wa bwana wake katika Ikulu ya White House, kutoka Zia-ul-Haq, kupitia ndugu wa Sharif, kisha wana wa Musharraf na Kayani, hadi kwa ndugu wa Sharif tena leo, pamoja na Asim Munir.
Ingawa vibaraka hawa ndani ya uongozi wa Pakistan wamepoteza aibu yote mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) na watumishi wake kwa kucheza dori hii ovu—kurudia walichofanya na Taliban nchini Afghanistan, na chini ya kivuli cha amani, wakiikabidhi Afghanistan, makaburi ya tawala za himaya, kwa Amerika kwa sahani ya fedha—sasa wanawapa ardhi ya Imam Muslim na Bukhari kwenye sahani hiyo hiyo kwa mkuu wa ukafiri na kiongozi wa muungano wa Makruseda, Amerika. Licha ya ushupavu wao na kutokuwa na haya, wasaliti hawa hawasubutu kukubali kwamba kwa kweli wanafanya kitendo kiovu. Badala yake, wanadai kufanya kitendo kizuri: kusimamisha vita visivyo vya haki na kupatanisha pande hizo. Wanaupa nguvu udanganyifu huu kwa msaada wa maulamaa wa serikali ambao wameendeleza uongo huu na kutenda dhambi kwa kushindwa kuwawajibisha watawala hawa, na kwa msaada wa vyombo vya habari vya mamluki na watu wenye ushawishi ambao wameuza Ummah wao duni thamani .
Ili kuweka wazi mambo kuhusu jambo hili muhimu, na ili wale wanaoishi waweze kuishi na dalili iliyo wazi, na wale wanaokufa waweze kufa na dalili iliyo wazi, tunasema: Maridhiano baina ya watu ambayo ni ya kusifiwa na ya lazima kwa Waislamu kuyafanya ni maridhiano kati ya waumini, kwa uwazi na uadilifu, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu (swt) Ambaye amesema,
[وَإِنْ طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا]
“Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni.” [Surah Al-Hujarat: 9]. Kwa hivyo, hukmu ya maridhiano kati ya watu ni kati ya waumini, na si kati ya waumini na makafiri; yaani, kujitahidi kupatanisha kati ya watu ni wakati mapigano ni kati ya makundi mawili ya waumini, na si kati ya kundi la waumini na kundi jengine la makafiri. Kinaya ni kwamba, huku serikali na wasemaji wake wakidai kutimiza wajibu wao wa Sharia wa upatanishi, wamepuuza kanuni hii kwa urahisi katika majaribio yao ya kupatanisha makundi ya Waislamu na Jeshi la Pakistan, na Taliban katika mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan. Badala yake, wameanzisha kampeni za kijeshi mfululizo kuwafuata na kuwaua Waislamu wa Taliban.
Hukmu ya Sharia ya Kiislamu inayotumika kwa mgogoro kati ya Amerika na Waislamu katika ardhi za Imam Muslim na Bukhari inapatikana katika hadith ya Mtume Muhammad (saw) ambaye amesema,
«انْصُرْ أَخَاكَ ظَالِمًا أَوْ مَظْلُومًا» “Mnusuru ndugu yako, iwe ni dhalimu au aliye dhulumiwa.” (Bukhari). Kwa hivyo, wajibu wa Sharia kwa watu wa Pakistan na Ulimwengu wote wa Kiislamu ni kuwanusuru ndugu zao wanaodhulumiwa.
Hali ya watawala wa kisiasa wa Pakistan na makamanda wa kijeshi ni kama ile ya watawala na makamanda wengine wa Waislamu katika nchi zote za Kiislamu; Kazi yao kuu ni kuwatumikia wakoloni makafiri, kuhujumu Umma wa Kiislamu katika kila mgogoro, na kuutelekeza Umma wa Kiislamu katika kila hali. Kama vile walivyowatelekeza watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina katika mapambano yao dhidi ya adui wa Mwenyezi Mungu (swt) na adui yao, Mayahudi, wamewatelekeza Waislamu nchini Iran. Kamwe hawatawamusuru Waislamu katika mgogoro wowote, wa zamani au wa sasa, wala kheri au uadilifu wowote hauwezi kutarajiwa kutoka kwao katika mustakabali. Kwa hivyo, wajibu wa Sharia unaowajibikia Umma wa Kiislamu ni kuwapindua watawala hawa na kuwabadilisha na Khalifa wa Waislamu ambaye atatetea Uislamu na Waislamu, akipigana pamoja nao na kutafuta ulinzi wao. Kufeli kutimiza faradhi hii ya Sharia kutaufanya Umma wa Kiislamu ubakie kutiishwa chini ya udhalilifu wa mkoloni kafiri. Kwa hivyo, Maulamaa na watu wenye ushawishi lazima watoe wito kwa hili, na kwa sababu hii, wanyoofu miongoni mwa watu wenye nguvu za kijeshi na ulinzi (أهل القوة والمنعة ahl ul-quwwah wal man'ah) katika majeshi ya Waislamu lazima watoe nusrah yao (نصرة msaada wa kijeshi) kwa Hizb ut Tahrir (حزب التحرير Chama cha Ukombozi) ili kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo italeta ushindi kwa Uislamu na Waislamu na kuunganisha Umma chini ya bendera ya Tawhid. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:
﴿إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنْفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ وَالْقُرْآنِ وَمَنْ أَوْفَى بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّهِ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُمْ بِهِ وَذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴾
“Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa” [Surah At-Tawbah: 111].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal al-Muhajir – Wilayah Pakistan



