Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 15/01/2021

Vichwa vya Habari:

Abdel Fattah El-Sisi wa Misri Asihi Usaidizi Zaidi kwa ajili ya Ujenzi Mpya wa Gaza

Waziri Mkuu wa Pakistan Azindua Sera ya Usalama wa Kitaifa

UAE Yawekeza Saini kwamba Nchi za OIC Zaiona Kashmir kama Sehemu Muhimu ya India: Wataalamu

Maelezo:

Abdel Fattah El-Sisi wa Misri Asihi Usaidizi Zaidi kwa ajili ya Ujenzi Mpya wa Gaza

Ukanda wa Gaza unahitaji "zaidi" ya dolari milioni 500 ambazo Cairo ilizitenga kwa ajili yake mnamo Mei 2021 kwa ajili ya ujenzi mpya, alisema Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi. Wakati wa kushiriki kwake katika Kongamano la Vijana Ulimwenguni katika jiji la Sharm El-Sheikh nchini Misri, alionyesha matumaini kwamba miradi ya ujenzi mpya ambayo makampuni ya Misri yanahusika ingekamilika “haraka iwezekanavyo kwa ajili ya ndugu zetu katika Ukanda wa Gaza.” El-Sisi alizitaka kampuni zinazofanya kazi huko kuajiri Wapalestina badala ya wafanyikazi wa kigeni. Pia alitoa wito kwa nchi wafadhili kutoa "msaada mkubwa" kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Kipalestina katika Mashariki ya Karibu. Rais Abdel Fatah al-Sisi alitangaza mwezi Mei kwamba Misri inatenga dolari milioni 500 kwa ajili ya ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza, na kwamba makampuni ya Misri yatashiriki katika kazi hiyo. Mapema mwezi Mei, mashambulizi ya anga ya Israel yalisababisha uharibifu wa zaidi ya makaazi 200 katika Ukanda wa Gaza na taasisi 31 za elimu, zikiwemo shule, vyuo na vituo vya mafunzo ya ufundi stadi. Kulingana na Umoja wa Mataifa, Wapalestina 40,000 walikimbia makaazi yao - haswa kutoka Kaskazini hadi Kusini - huku 2,500 wakipoteza makaazi yao. Vilevile, vifo 213, wakiwemo watoto 61 na wanawake 36, vilirekodiwa pamoja na majeruhi 1,442. [Chanzo: Arab News; Egypt Today]

Ni mara ngapi Misri imeingia katika ujenzi upya baada ya dola ya Kiyahudi kuharibu Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Palestina? Gaza haihitaji kujengwa upya bali ukombozi wa kudumu kutoka kwa dola ya Kiyahudi. Suluhisho pekee ni ukombozi kupitia Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Waziri Mkuu wa Pakistan Azindua Sera ya Usalama wa Kitaifa

Waziri Mkuu Imran Khan mnamo siku ya Ijumaa alizindua waraka wa kwanza kabisa wa sera ya usalama wa kitaifa nchini Pakistan - unaolenga usalama wa binadamu na kiuchumi. Hati hiyo iliidhinishwa na baraza la mawaziri la shirikisho mnamo Disemba 28 baada ya kuunga mkono Kamati ya Usalama wa Kitaifa. Mnamo Ijumaa, toleo la umma la hati asili ya kurasa 110 ilitolewa baada ya kuonyeshwa kurasa 50. Akihutubia sherehe za uzinduzi mjini Islamabad, Khan alisema kuwa "sera inayojumuisha wote itatoa mwelekeo wa taifa" katika nyanja mbalimbali za usalama wa taifa. Waziri Mkuu alisema kuwa usalama wa nchi unahusishwa na usalama wake wa kiuchumi na sera hiyo mpya itasaidia kuhakikisha ukuaji wa umoja nchini kinyume na usalama wa kijeshi wa mwelekeo mmoja ambao umebakia kipaumbele kwani "mageuzi ya Pakistan yalifanyika katika hali isiyo salama sana. Mazingira na nchi yalikabiliwa na migogoro na jirani zaidi ya ukubwa wa Pakistan,” Waziri Mkuu alisema. "Sera ya Usalama ya Kitaifa 2022-26 inazingatia maono ya serikali yangu, ambayo inaamini kuwa usalama wa Pakistan unategemea usalama wa raia wake. Mtazamo huu unaozingatia raia kwa usalama wa wa taifa unatanguliza mshikamano wa kitaifa na ustawi wa watu, huku ukihakikisha haki za kimsingi na haki za kijamii bila ubaguzi," waziri mkuu wa Pakistan alisema. Sera hiyo inalenga kufikia ukuaji shirikishi na kulinda watu walio katika mazingira magumu kwa kuibadilisha Pakistan kuwa dola ya ustawi na mipango iliyoanzishwa na serikali ya Imran Khan, ikijumuisha bima ya afya kwa wote yenye thamani ya rupia milioni 1 kwa mwaka kwa familia za kipato cha chini, mpango wa hifadhi ya jamii wa Ehsaas, mikopo ya nyumba ya gharama nafuu na mtaala mmoja wa kitaifa. Mshauri wa usalama wa kitaifa wa Pakistan Dkt Moeed Yusuf alisema kuwa "Mtazamo wa Pakistan kwa usalama wa taifa ni mpana, makini, na thabiti na unalenga kuhakikisha usalama wa raia wetu walio hatarini zaidi. Usalama wetu wa kitaifa unatafuta kutambua njia za kupanua rasilimali za kiuchumi kama vile Pakistan inaweza kuimarisha usalama wake wa jadi na usio wa jadi. Mbinu ya busara zaidi ni "kuweka usalama wa kiuchumi katika msingi" na kuhamisha "gawio la uchumi imara ili kuimarisha ulinzi wetu na usalama wa binadamu. Hii ndio ruwaza ambayo sera ya usalama wa taifa inajitahidi kuifuata.” [Chanzo: : Gulf News]

Uchumi utawezaje kuwa nguzo kuu ya waraka mpya wa usalama, wakati Pakistan imedhoofisha pakubwa ubwana wa kiuchumi kwa kutafuta msaada kutoka kwa IMF? Mswada wa uhuru wa maamuzi wa SBP ni mfano mmoja wa IMF inavyoshinikiza udhibiti wa uchumi wa Pakistan, jambo ambalo linakejeli sera ya usalama wa kitaifa.

UAE Yawekeza Saini kwamba Nchi za OIC Zaiona Kashmir kama Sehemu Muhimu ya India: Wataalamu

Katika kile ambacho kinaweza kuleta uwekezaji mkubwa na kuunda nafasi za kazi huko Jammu na Kashmir, kampuni saba za serikali na za kibinafsi zinazomilikiwa na UAE zimejitolea kuwekeza katika J&K. Wakati wa ziara ya LG Manoj Sinha huko Dubai wiki iliyopita, makubaliano yalitiwa saini na LuLu Group, Al Maya Group, MATU Investments LLC, GL Employment Brokerage LLC & Noon Group katika sekta mbalimbali. Pia, DP World itajenga bandari ya ndani ya J&K. Mkataba wa maelewano (MoU) wa uwekezaji wa $-100 milioni na Century Financial pia ulitiwa saini. Akihutubia katika Mkutano wa Wawekezaji na Viongozi wa Biashara katika EXPO Dubai, LG Manoj Sinha alisema, "Uhusiano kati ya India na UAE umekomaa vya kutosha kwa miaka na kuwa 'Washirika wa Kimataifa' wa kudumu katika karne ya 21. Hizi ni zile nyakati katika safari ya Jammu na Kashmir ambapo fursa ziko nyingi." "Kwa sababu ya sera za uwazi na urahisi wa kufanya biashara, tuliweza kupata mapendekezo ya uwekezaji yenye thamani ya ₹45,000 crore na ziada ya ₹18,300 crore katika sekta ya ardhi na nyumba," alisema Lt Gavana, na kuongeza, "Hali ya usalama imeimarika kwa kiasi kikubwa na tunapokea watalii milioni 1.4 kwa wastani kila mwezi, hali inayoonyesha wazi mazingira mazuri ya biashara kustawi.” "Ninawaahidi kasi isiyokuwa ya kawaida katika kusafisha mapendekezo na nyaraka zinazohitajika, usaidizi usio na kifani kutoka kwa serikali na mazingira dhabiti ambayo hayajawahi kushuhudiwa ili kupata fursa zinazokuwa kwa kasi katika eneo la Muungano. Ninawahakikishia kuwa serikali itakuwa mwezeshaji, mshirika, mtoa huduma, mshiriki na mkuzaji katika kila hatua ili kuhakikisha mazingira endelevu, yenye uwiano, ya kimaendeleo na yenye ushindani kwa sekta kuu za jadi na sekta zinazoendeshwa na teknolojia ya zama mpya,” Sinha aliongeza. Wataalamu wameitaja kuwa ni ustadi mkubwa katika nyanja za kidiplomasia na vile vile za kisiasa. DGP wa zamani, ambaye alihudumu katika J&K, aliiambia News18, "Hii ni hatua kubwa kidiplomasia kwani nchi muhimu ya OIC UAE inawekeza katika eneo la muungano na hii ina maana kwamba wanatambua kuwa madai ya India ni halali. Pia, ni kikwazo kikubwa kwa Pakistan kwani nchi hiyo jirani imekuwa ikihamasisha kundi la OIC huko Kashmir. Lakini sasa nchi za OIC zimeanza kuitambua Kashmir kama sehemu muhimu ya India. Endapo uwekezaji wa UAE utaongezeka, basi Wasaudi wanaweza kufuata." [Chanzo: News 18]

Kuhalalisha umiliki wa India wa Kashmir na UAE hakushangazi. Katika miaka kadhaa iliyopita, nchi za Ghuba zimetafuta na kudumisha kichangamfu maslahi ya kibiashara na dola ya Kiyahudi, Myanmar na China. Ijapokuwa nchi hizo zimekuwa mstari wa mbele kuwakandamiza kikatili Waislamu wa Palestina, Myanmar na Xinjiang.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu