Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu la Swali
Aina ya Vima

Kwa: Hamed Shaheen
(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalamu alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,

Namuomba Mwenyezi Mungu uwe mzima na afya njema ewe Amiri wetu mheshimiwa,

Swali langu ni kuhusu vima. Swali ni kuhusu vima ambavyo Hizb inavipata katika kuanzisha tena maisha kamili ya Kiislamu. Je, kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kunapata "kima cha utu" kwa sababu ni kitendo kinachookoa wanadamu ikiwa kitafikiwa, au kunapata "kima cha kiroho" kwa sababu kuanzisha tena maisha kamili ya Kiislamu kumejengwa juu ya msingi wa kisheria (sio wa kighariza) unaohusiana na utawala wa Uislamu na faradhi ya utiifu kwa Khalifa, nk.? Barak Allahu fiik.

Pia, je, kima cha kiroho kinahusiana tu na ibada na sio kitu chengine chochote?

Jibu:

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullah wa Barakatahu,

Kwanza: Kabla ya kujibu, ni muhimu kufafanua vipengele viwili vinavyohusiana na vina:

* La kwanza ni kwamba kima ni dhamira ya kitendo na si matokeo yanayopatikana kutokana na kufanya kitendo. Kima kinaweza kuwa cha kiroho, lakini matokeo ni yanayoonekana au yasiyoonekana. Kwa mfano, unajitahidi na nia yako ni kima cha kiroho, lakini matokeo ya kitendo hiki ni matokeo yanayoonekana, kama vile ufunguzi wa nchi au ngome ... Na unaswali na nia yako ni kufikia kima cha kiroho na matokeo yake ni yasiyoonekana ikiwa swala katika hali hiyo haitokani na njia, bali ni njia ya kisheria isiyokuwa ya dua, hivyo matokeo yatakuwa ni kupata malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Imeelezwa katika Fahamu za Hizb ut Tahrir (Mafaahim): “... Kwa mfano, dua ni kitendo kinachopata kima cha kiroho, na jihad ni kitendo cha kimada ambacho kinapata kima cha kiroho, lakini dua, hata ikiwa ni kitendo cha kimada, kinapata matokeo yasiyoonekana, ambayo ni malipo, hata kama dhamira ya mwenye kuswali ni kufikia kima cha kiroho, tofauti na jihad, ni kupigana na maadui na ni kitendo cha kimada kinachopata matokeo yanayoonekana kama kuteka ngome au mji au kuuawa kwa adui na kadhalika, hata kama nia ya mujahid ni kufikia kima cha kiroho...”

Ama dua katika kesi nyingine, “ambayo hakuna njia halali,” inaweza kufikia matokeo yanayoonekana. Imeelezwa katika jibu la swali la tarehe 25 Oktoba 2014: “…Hakuna chochote kilichotajwa katika Fahamu (Mafaahim) kuhusu dua katika hali nyingine, bali ni zile zilizojumuishwa katika Hadith jumla ambayo Ahmad aliijumuisha katika Musnad yake: Kutoka kwa Abu Al-Mutawakkil, kutoka kwa Abu Saeed, kwamba Mtume (saw) amesema:

«مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَدْعُو بِدَعْوَةٍ لَيْسَ فِيهَا إِثْمٌ، وَلَا قَطِيعَةُ رَحِمٍ، إِلَّا أَعْطَاهُ اللَّهُ بِهَا إِحْدَى ثَلَاثٍ: إِمَّا أَنْ تُعَجَّلَ لَهُ دَعْوَتُهُ، وَإِمَّا أَنْ يَدَّخِرَهَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ، وَإِمَّا أَنْ يَصْرِفَ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهَا»

“Hapana Mwislamu yeyote atakaye omba dua ambyo hakuna ndani yake uovu, wala kukata kizazi, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa kwayo mambo matatu: ima amharakishie aliloliomba, ima atamuekea aliloliomba kesho Akhera, au Amwondolee shari mithili ya jema aliloliomba.” Wakasema: Basi tuzidishe, akasema: «اللَّهُ أَكْثَرُ» “Mwenyezi Mungu ndiye zaidi.” Yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu humjibu muombaji kwa moja katika mambo matatu, mojawapo ni «إِمَّا أَنْ تُعَجَّلَ لَهُ دَعْوَتُهُ» “ima amharakishie aliloliomba.” Ni matokeo ya kuonekana.”

* Pili ni kwamba somo la kima linahusiana na nia ya mtu binafsi, yaani, ni mtu binafsi:

1. Katika Mafaahim, vima vimeunganishwa na dhamira ya mtu binafsi (cha kibinadamu kwa maana ya mtu au mfanyikazi) [katika ukurasa 30-34] ikisema yafuatayo:

“... Kuhusu nia ya kazi, kila mfanyikazi lazima awe na nia ya kazi inayofanywa. Nia hii ni thamani ya kazi. Kwa hiyo, ilikuwa hakuna budi kwamba kila kazi iwe na thamani ambayo mtu hutilia maanani wakati wa kufanya kazi hiyo, vyenginevyo itakuwa tu bure bilashi...”

Kwa hivyo, Muslim hana budi kufanya kila awezalo ili kufikia thamani iliyokusudiwa ya kila kazi anayoifanya wakati wa kuitekeleza na kuifanya kazi hii, ili kuchangia katika ustawi na mwinuko wa jamii, na wakati huo huo kudhamini ustawi na utulivu wa nafsi yake...

Ndiyo maana ni makosa kwa vima hivi kukadiriwa na mwanadamu. Bali, vima lazima vitathminiwe na Muumba wa mwanadamu, Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, ni muhimu kwa Shari’ah kubainisha vima hivi kwa mwanadamu na kubainisha muda wa kuvitekeleza, na kwa hivyo mtu anavichukua...

Kwa njia hii, vima hupatikana katika mujtamaa kadiri unavyohitaji kama mujtamaa maalum. Mujtamaa huu unapimwa kwa viwango vyake. Kwa msingi huu, lazima afanye kazi ili kufikia vima hivi, kuzalisha jamii ya Kiislamu kulingana na mtazamo wa Uislamu wa maisha.] Mwisho

2. Hii ina maana kwamba thamani ya kazi ni dhamira ambayo kwayo mfanyikazi aliifanya kazi hiyo, kwa hiyo thamani ni dhamira ya kazi hiyo, na mwenye kusudi la kazi hiyo ni mwanadamu, yaani mtu anayetambulika, kama Muhammad, Zainab, Fatima na Khaled, anapofanya kitendo anachokusudia kufikia thamani maalum ya kazi yake. Ikiwa Muhammad alifanya biashara, anakusudia kupata faida ya kimada, ambacho ni kima cha kimada, na iwapo Zainab ataswali, anakusudia kufikia thamani ya kiakhlaqi, ambayo ndicho kima cha kiroho... Na ikiwa Fatima ni mkweli, basi anakusudia kufikia thamani ambayo ni thamani ya kiakhlaqi. Na ikiwa Khaled anamsaidia mwenye shauku, basi anakusudia kufikia thamani ambayo ni thamani ya utu... Hivyo, kima ni nia ya mtu binafsi kufanya kazi hiyo, yaani mtu anayeifanya kazi hiyo kwa nia ya kupata thamani ni binadamu "mtu binafsi".

3. Hapa, kazi ya Hizb inajitokeza kudhibiti vima hivi miongoni mwa Mashababu (wanachama) wake, iwe vima hivi ni vya kiroho, kiakhlaqi, kiutu au kimada, ili vima hivi viwe kwa mujibu wa hukmu za Shariah, na Hizb hutumia njia zinazohitajika kuzidhibiti kama vile uongofu au dalili kwa mujibu wa hukmu za Shariah, na kama uongofu na dalili haudhibiti Mashababu basi adhabu ya kiidara lazima itumike ili kuhakikisha kwamba Mashababu wanatekeleza vima hivi kwa mujibu wa amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu...

Kadhalika, kazi ya dola ni kusimamia vima hivi kwa mujibu wa hukmu za Shariah, na Muislamu kama mtu binafsi (kama mtu au mfanyikazi) hana chochote isipokuwa kufanya kazi katika kuvifikia vima hivi kwa mujibu wa amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu. Katika aina zote, kima cha kiroho, cha kiakhlaqi, cha kiutu na cha kimada.

Hili ni jukumu la serikali na dori yake katika kudhibiti upataji wa vima wa mtu binafsi kwa mujibu wa hukmu za Shariah, iwe kima ni cha kiroho, akhlaqi,  utu au cha kimada... Na njia zinazohitajika hutumika kuvidhibiti, kama vile mwongozo au dalili kwa mujibu wa hukmu za Shariah, na iwapo muongozo na dalili hazipatikani kusahihisha ukiukaji wa Shariah katika utekelezaji wa watu binafsi wa vima hivi basi adhabu inahitajika, ili kuhakikisha kwamba watu binafsi wanavitekeleza vima hivi kwa mujibu wa amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu...

Pili, sasa nitajibu swali lako:

1. Mbebaji Da'wah ambaye anafanya kazi ya kuregesha maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah, anakusudia katika kazi yake kupatikana kima cha kiroho ili kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume Wake (saw), na matokeo ya kazi yake itakuwa ni matokeo yanayoonekana kama vile izza, ushindi, tamkini, ufunguzi na kueneza kheri pale ambapo Khilafah imemakinika.

[وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِنَ اللَّهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ]

“Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!” [As-Saf 61:13].

2. Nia ya kupata kima ni suala la mtu binafsi, yaani linalohusiana na watu binafsi. Kwa hiyo, mtu ana nia ya kufikia kima cha kiroho, cha kiakhlaqi, cha kiutu au cha kimada ... Ni nia ya mtu binafsi. Ama Hizb, kutokana na kazi yake, ni kuwadhibiti Mashababu wake ili matendo yao yasiwe ya bure bilashi, bali wafanye kazi ili kufikia vima hivi kwa mujibu wa hukmu za Shariah. Kadhalika, kazi ya dola ni kudhibiti utambuzi wa vima hivi kwa watu binafsi katika mujtamaa kwa mujibu wa hukmu za Shariah.

Natumai kuwa jibu hili litatosheleza, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi na Mwenye Hekima.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

06 Rabii’ al-Akhir 1444 H

Sawia na Oktoba 31, 2022 M

Link ya jibu hili kutoka ukurasa wa Amir wa Facebook.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu