Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mashambulizi ndani kabisa ya Lebanon!

Yako wapi Mamlaka ya Kisiasa na Vyombo vyake kuhusiana na Stahiki zake?! Je, Uvumilivu wa Kimkakati wa Mhimili Bado haukwisha?!
(Imetafsiriwa)

Mashambulizi ya mabomu ya Lebanon ya wale waliokasirikiwa - Mayahudi - yamekuwa ya mara kwa mara kila siku, na hata kuathiri miji mikubwa kama Sidoni, Tyre, na Nabatieh, baada ya kufungika kwenye vijiji vya mpakani, kuua na kujeruhi watu walio salama katika maeneo hayo na mijini. Tunamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, awakubalie mashahidi wao, awaponye majeruhi wao, na awaponye maumivu yao, hii ni pamoja na safari nzito za ndege za Kiyahudi na matembezi juu ya Lebanon, hadi kaskazini ya mbali ya Lebanon, bila kizuizi au hata kujaribu kuyazuia!

Ama kuhusu mamlaka ya Lebanon na vyombo vyake, vimekaa kimya sawa na kimya cha makaburi isipokuwa malalamiko kwa Baraza la Usalama, baraza lile lile linalofuatilia mauaji ya watu wa Gaza! Bila kufanya chochote, tofauti na lilivyofanya kwa Ukraine, kwa mfano! Lau baadhi ya nchi zilijaribu kuchukua hatua, Marekani inazikabili kwa "veto"! Licha ya hitilafu kati ya utawala wa Biden na Netanyahu na serikali yake ya Kiyahudi yenye msimamo mkali, inapokuja suala la uwepo na kuendelea kwa umbile hili nyakuzi, na suala hilo linaingizwa kwenye damu ya Waislamu, Marekani inakanyaga maadili yote ambayo inayadai na kuulingania ulimwengu kushikamana nayo, ambayo ni, kiasili yao, maadili ya uongo na duni.

Mamlaka hii ya Lebanon na vyombo vyake, ambayo inafanya vyema tu katika kuongeza kodi, kuongeza faini, na kujadidisha mamlaka, unaiona mamlaka hiyo hapa, ikifanya kazi kwa njia ambayo uamuzi wake unatanguliza kodi bora zaidi na wapangaji faini! Je, hili si kweli kwa utawala wa Lebanon na mamlaka yake, kama vile tawala za eneo lenye mafungamano na nchi za Magharibi, zinashughulika na watu wake na adui wake kwa mujibu wa kanuni ya "simba yuko juu yangu wakati mbuni yuko vitani"! Iko wapi mamlaka hii ambayo haifikirii kujihami hata kwa mifumo midogo ya ulinzi hewani?!

Ama kuhusu mhimili wa kile kinachoitwa upinzani, na kile ilichokiita kuhusiana na umoja wa medani, kabla ya Kimbunga cha Al-Aqsa tangu 2021, ilikuja na maneno mawili mapya "udhibiti wa mshtuko" na "uvumilivu wa kimkakati", baada ya neno la zamani "jibu kwa wakati na mahali muwafaka"! Ni mshtuko gani ambao huwezi kuudhibiti, ambao unahitaji kuingia vitani kwa nguvu kamili?! Halafu je uvumilivu huu wa kimkakati haujaisha bado?! Wakati na mahali sahihi itakuja lini?! Au ukweli ni ule alioueleza Sheikh Naim Qassem, Naibu Katibu Mkuu wa Chama, mnamo Februari 15, 2024 wakati wa hafla ya ukumbusho: “Tunajibu kwa njia ya uwiano, na chaguo letu ni kuinusuru Gaza huku tukiendelea kumzuia adui msaada huu na makabiliano haya machache ndio tumeyaona yana faida na manufaa...”?!

Imedhihirika kuwa uamuzi ulichukuliwa katika ngazi ya kikanda, inayowakilishwa na Iran, kwa kuafikiana na uamuzi wa kimataifa, unaowakilishwa na Marekani, kutekeleza hali hii ya uwiano na hali hii mpya ya kile kinachoitwa kuzuia na kiasi kidogo cha makabiliano.! Hii inaeleza kwa nini mzigo wa Lahian na Hochstein unasalia kufunganywa kuja Lebanon kila kukicha! Ili kuweka uwiano, makabiliano machache, subira ya kimkakati, na masuluhisho ya mazungumzo, kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alivyosema katika taarifa zilizochapishwa na Idhaa ya Al-Manar ya Hezb, mnamo tarehe 2/7/2024: “Serikali ya Bwana Raisi inaamini kwa uthabiti njia ya diplomasia na mazungumzo, na haijawahi kujitenga na meza ya mazungumzo, na kamwe haitaweza! Hali ilipozidi kuwa mbaya na shimo lilipofunguliwa kwenye ukuta na Mayahudi, watu wa Gaza waliachwa peke yao, wakikabiliana na watoto wao, wazee na silaha zao nyepesi - mashini ya maangamivu makubwa iliyoungwa mkono na nchi za Magharibi ili kuhifadhi uvamizi ya umbile la Kiyahudi, ambalo lilitikiswa katika eneo hilo mikononi mwa kikundi kidogo, Katibu Mkuu wa Chama, Bwana Hassan Nasrallah, alijitokeza, siku thelathini baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, mnamo tarehe 11/3/2024, akiridhika kwa kupiga Mashamba ya Shebaa wakati huo, na kuyaita: "Ujumbe wa mshikamano pamoja na Gaza"! Muhimu zaidi, alidokeza kwa kusema: “Vita vyetu havijafikia hatua ya ushindi kwa muondoano. Bado tunahitaji muda kuwa wa kweli, lakini tunashinda kwa pointi...”! Baada ya chaguo maarufu na lililopigiwa debe hapo awali kati ya wale waliokuwa wakiitisha mhimili huu ilikuwa "kuliondoa umbile hilo ndani ya dakika saba" na "vita vikubwa vilivyosubiriwa kutokana na umoja wa medani," hadi msemaji wao akasema. : “Funganyeni mizigo yenu mrudi Palestina”!

Haya yote yametia moyo umbile la Kiyahudi na jeshi lake dhaifu kuendelea katika udanganyifu wao, kwa kulenga shabaha zaidi, na kutangaza hili hadharani! Uhamasishaji uliofanywa na chama wakati wa mapinduzi ya Kiarabu, kuunga mkono kile ilichokiita vita vyake vya mapema dhidi ya ugaidi, ungekuwa sawa au kidogo kama ilivyokuwa kwa Mayahudi, na kwa ajili ya Palestina, kauli mbiu hiyo ambayo imekuwa ikinyanyu kukulia kwa miaka! Hata hivyo, ilitosha kwa yale aliyoyaeleza Katibu Mkuu wa Chama katika hotuba yake ya tarehe 11/3/2023, katika taarifa yake ya muhtasari wa hali mhimili huu ulipofikia: “Vita hivyo ni vita vya uthabiti, subira, uvumilivu, kufikia mafanikio, na kukusanya mafanikio...”, Na njia ya mazungumzo ndiyo kipaumbele cha watu hawa, kama ilivyoelezwa katika maana ya maneno ya Sheikh Naim Qassem na kauli yake: “Hatuna mjadala kuhusu mustakabali wa kusini mwa Lebanon kutoka pande zake mbili, kutoka upande wa Palestina na kutoka upande wa Lebanon, isipokuwa baada ya uchokozi kamili dhidi ya Gaza kusimama”!

Enyi Waislamu nchini Lebanon; Kutoka kwa Ali bin Abi Talib, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe pamoja naye, kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«الْمُسْلِمُونَ تَتَكَافَأُ دِمَاؤُهُمْ وَيَسْعَى بِذِمَّتِهِمْ أَدْنَاهُمْ وَيَرُدُّ عَلَيْهِمْ أَقْصَاهُمْ وَهُمْ يَدٌ عَلَى مَنْ سِوَاهُمْ، أَلَا لَا يُقْتَلُ مُسْلِمٌ بِكَافِرٍ وَلَا ذُو عَهْدٍ فِي عَهْدِهِ»

Maisha ya Waislamu wote ni sawa; walio wa hali ya chini zaidi wao wanaweza kudhamini ulinzi wao, walio mbali zaidi wanaweza kuwazuia wengine wasivunje ulinzi ambao wametoa, * nao ni kundi moja dhidi ya wengine. Muislamu asiuwawe kwa ajili ya kafiri, wala asiuwawe aliyepewa ahadi akiwa yuko ndani ya ahadi yake.” “Basi msiseme: Kwa nini tuingie vitani pamoja na watu wa Palestina? Au: Hatuwezi kuhimili matokeo ya vita! Wajibu wenu ni mmoja na damu yenu ni moja, mbele ya wale wanaokalia kimabavu shubiri moja ya ardhi ya Kiislamu, popote walipo.

Enyi Waislamu nchini Lebanon; Nyinyi na sisi tuko kwenye njia panda, kwani dori ya watawala wa madhara ambao wameketi kwenye mipaka ya Sykes-Picot, wakilizunguka umbile la Kiyahudi, au karibu nalo, au mbali zaidi, imekuwa wazi kwenu na inaonekana wazi, na wanamiliki makombora ambayo kwayo tunasikia tu majina yao yanayosikika! Wao ndio asili, na Mayahudi ni kivuli kwao. Ikiwa asili itatoweka, kivuli kinaondoka! Wanalinda umbile la Kiyahudi na kuhakikisha ulinzi wake, na hata kulipatia chakula na msaada wa kijeshi, hadharani na faragha. Wanatangaza kususia bidhaa na makampuni yanayounga mkono umbile la Kiyahudi, na kutoka chini ya meza, na hata juu yake, wanalipatia mafuta, makombora, na mavazi ya kijeshi, ambayo yanawapa joto huku wanaua ndugu zenu, kwa mabomu, njaa, baridi na dhulma! Wanakuacheni katika dhiki yenu, nyoyo zenu zikiwaka dhidi ya ndugu zenu, na munaanguka katika tashwishi zenu na kile walichotaka kwenu, udanganyifu kwamba hamuna uwezo wa chochote! Hakika, nyinyi, Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda, nyinyi ni mwenye uwezo na munaweza!

Je, watoto wenu hawako jeshini kuanzia askari, maafisa na makamanda?! Je, munawaruhusu vipi kufumba macho na warudi majumbani mwao wakitingisha mikia ya kuvunjika moyo na kujitiisha?! Je, vyeo na medali hizi zimekusudiwa kujionyesha?! Je, kinachokatwa katika riziki zenu kwa ajili ya majeshi haya yanayoundwa kwa watoto wenu, ni ili kunenepesha tumbo la mtawala, wasaidizi wake na walinzi wake? Ilhali watoto wenu wanauawa, si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali kwenye vizingiti vya vibaraka hawa wasaliti, ambao hawamuonei haya Mwenyezi Mungu, Mtume wake, na waumini!!

[أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ * اعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ]

“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu. Jueni kwamba Mwenyezi Mungu huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Tumekubainishieni Ishara ili mpate kuzingatia.” [Al-Hadid:16-17]. Nyoyo zao zitaishi lini kama sio leo?! Kwa kiasi hiki cha umwagaji damu, na mashambulizi dhidi ya wanaume na wanawake huru kutoka kwa watu wa Gaza, Palestina, Lebanon, na kila sehemu iliyofikiwa na mkono wa khiyana ya Mayahudi!!

Enyi Waislamu nchini Lebanon; Wachocheeni watoto wenu wasonge ili kuwanusuru watu wao, na Hizb ut Tahrir iko pamoja nanyi, ndani yenu na miongoni mwa watoto wenu. Endapo watawala wakisimama mbele yao, hebu na wawatupe chini. Wakati huo huo, msibweteke na kukaa kimya kwa muda mrefu, mkililia watu wa Gaza na machungu yanayowapata! Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amekukatazeni kuwa wanyonge katika kupigana na watu, maadui zake, Mwenyezi Mtukufu, ambao licha ya maumivu yao, hawatarajii kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu isipokuwa hasara, adhabu na uchungu duniani na kesho Akhera - wanakupigeni kwa mkono mmoja na wana nia ya kukuueni!

[وَلَا تَهِنُوا فِي ابْتِغَاءِ الْقَوْمِ إِن تَكُونُوا تَأْلَمُونَ فَإِنَّهُمْ يَأْلَمُونَ كَمَا تَأْلَمُونَ وَتَرْجُونَ مِنَ اللهِ مَا لَا يَرْجُونَ وَكَانَ اللهُ عَلِيماً حَكِيماً]

“Wala msifanye ulegevu kuwafukuzia kaumu ya maadui. Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyo umia nyinyi. Nanyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu wasio yataraji wao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.” [An-Nisa:104].

H. 10 Sha'aban 1445
M. : Jumanne, 20 Februari 2024

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu