Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mamlaka ya Dayton mjini Ramallah na Mamlaka ya Lebanon Zinakwenda Ndani ya Ajenda ya Marekani ili Kuondoa na Kumaliza faili ya Kambi!
(Imetafsiriwa)

Tangu mwanzo wa matukio katika Kambi ya Ain al-Hilweh mwishoni mwa Julai 2023, Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Lebanon alitoa toleo mnamo 31/7/2023 lenye kichwa: Hali ya Kikanda, uchoraji mipaka ya ardhi! Kuweka matayarisho katika kambi ya Ain al-Hilweh kwa ajili ya vita na operesheni za usalama” Miongoni mwa yale yaliyotajwa ndani yake ni kwamba "uamuzi ulifanywa ili kujumuisha mambo yaliyotawanyika ya harakati ya Fatah ndani ya kambi na kuregesha udhibiti kwa Mamlaka ya Dayton, ambayo inashikilia uratibu wa usalama "takatifu ", juu ya kambi. Hili linafanywa na watu ambao wanaahidi utiifu kamili kwa mamlaka hii, ambayo imeegemea wazi kwa Marekani”.

Chama hicho kilionyesha katika taarifa yake kwamba kuna uamuzi wa kisiasa wa Mamlaka ya Lebanon unaozuia kuingilia kati kwa vikosi vya usalama vya Lebanon kusimamisha vita, taarifa hiyo ilisema: "Vikosi vya usalama vya Lebanon, vinajulikana kwa kuingilia kati kusitisha mapigano hayo ndani ya masaa kadhaa, vinaonekana vikiruhusu hali hiyo kuongezeka kwa kiwango kamili. Hili linaambatana na majaribio ya kisiasa ambayo yameshindwa kushughulikia uzito wa hali hiyo. Hili linazua shaka juu ya asili ya ziara ya Majed Faraj, mikutano yake, na kile kilichojadiliwa wakati wake”.

Matukio haya mapya katika kambi ya Ain al-Hilweh mnamo Alhamisi usiku, 7/9/2023, yanathibitisha kile chama kilichoamini zaidi ya mwezi mmoja uliopita. Imethibitishwa kuwa mamlaka ya Lebanon inahusika katika yale yanayotokea ndani ya kambi leo. Vyenginevyo, tunawezaje kuuelezea uwezeshaji wa mamlaka ya Lebanon wa kuingia kwa silaha nzito za kisasa kambini kwa faida ya moja ya pande husika kwenye mapigano yaliyowakilishwa na Mamlaka ya Dayton na mikono yake, Usalama wa Kitaifa na Harakati ya Fatah, na uhamisho wa chembe kutoka kwa kambi zengine kwa uangalizi kamili wa mamlaka hii? Ingawa inakataza kuingia kwa mfuko wa simiti kwa shughuli za ukarabati au ujenzi isipokuwa kwa idhini ya usalama ambayo ni ngumu kuipata! Je! Tunawezaje kukielezea kimya cha mamlaka hii kuhusu kile kinachotokea na kufeli kwake kutoa idhini kwa vikosi vya usalama kulazimisha kusitisha mapigano, hadi wakati wa kuandika taarifa hii. Hii ni licha ya kulenga vituo viwili vya jeshi la Lebanon karibu na kambi hiyo na kujeruhiwa askari, ambao baadhi yao walijeruhiwa vibaya mnamo usiku wa 11/9/2023?!

Kilicho cha hakika na ukweli hadharani ni kwamba Mamlaka ya Dayton huko Ramallah imetekeleza mpango huu kupitia mkono wake wa kijeshi kambini, Huduma yake ya Usalama wa Kitaifa, na kupitia harakati ya Fatah, kundi kuu katika mamlaka hii! Kumbuka kwamba hapo awali tuliwaonya viongozi wa harakati hiyo juu ya kile Mamlaka ya Dayton, ambayo iliuza Palestina, ikauza lengo lake, na kukabidhi mamlaka yake kwa Marekani na Mayahudi! Walakini, kuna msisitizo kati ya baadhi ya viongozi hawa juu ya kuregelea sheria ya Mwenyezi Mungu (swt) kuhusu uharamu wa (kumwaga) damu, na sio kutii lugha ya akili!

Kwa hivyo, matukio haya yamekuwa wazi kwa kila mtu, kijana na wazee, kambini na nje yake, kwamba kinachotokea ni njama chafu, ambayo lengo lake ni kutengua na kumaliza faili ya kambi kulingana na uamuzi wa kisiasa wa Marekani wa kuchora mpaka wa ardhi ya Lebanon na umbile la Kiyahudi ambalo linainyakua ardhi iliyobarikiwa ya Palestina! Na kumaliza hali ya uadui kati ya umbile Kiyahudi na Lebanon! Vyenginevyo, je ni kutoka kwa Sharia au akili kuharibu mitaa yote kwa kisingizio cha kuleta washukiwa?! Isipokuwa huu ndio mradi unaohitajika, uharibifu wa kimfumo, ambao ulianzishwa na upande mmoja, na ambao pande zengine zilifuata bila mwongozo!

Kwa watu wetu katika kambi ya Ain al-Hilweh, tunasema:

Kinachotokea kwenu leo ni mwenendo dhahiri katika hali ya kisiasa katika kanda hii, ya kwanza yake ikiwa ni kuendelea kumaliza hali yoyote ya kijeshi ambayo angali inaleta tishio, hata ikiwa ni kidogo tu, kwa umbile la Kiyahudi na kwa tawala ambazo zinalinda umbile la Kiyahudi kutoka pande zake. Ya pili, ni mwendelezo wa hali zilizotangazwa za uhalalishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi, haswa baada ya Lebanon kuwekwa kwenye njia ya kuhalalisha mahusiano tangu kukamilika kwa uchoraji mipaka ya bahari na sasa mipaka ya ardhi! Ziara ya Mshauri wa Rais wa Marekani wa Usalama wa Kawi Ulimwenguni, Amos Hochstein, mnamo 30/7/2023, haiko mbali na sisi, ambayo alithibitisha: "Uwezo wa kufanya kazi sasa juu ya suala la kuchora mipaka ya ardhi"! Ziara hiyo iliambatana na ziara ya Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Amir-Abdollahian mnamo 30/7/2023! Ili picha hiyo iwe kamili kwa vyama vyote, haswa Chama cha Iran na wale wanaodai upinzani, kuhusiana na sifa za uchoraji ardhi, ikiwemo umuhimu wa kuvunja na kumaliza hali ya kambi nchini Lebanon, haswa kusini mwake, sambamba na maslahi ya kampuni za gesi na mafuta!

Enyi watu wa Lebanon kwa jumla, na Waislamu haswa:

Vibaraka wa Mamlaka ya Lebanon wanaendeshwa na Marekani, baadhi yao moja kwa moja na wengine kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Hawajali usalama wenu au riziki yenu isipokuwa kwa kiwango ambacho hudumisha "Shamba la Lebanon" umbo dhaifu ambalo hutoa ustawi wao. Wao ni wale waliouza dini yao kwa ajili ya dunia yao na dunia ya maadui zenu, kwa gharama ya maisha yenu, ya watoto wenu, na fahari ya nchi hii na watu wake.

Kwa hivyo, msitegemee chochote isipokuwa baya zaidi kutoka kwao, msidanganyike na taarifa zao za kushambulia Mayahudi au Marekani. Tumewaona wakitangaza (taarifa) dhidi ya mabenki, kwa mfano, na hadi sasa hakuna benki hata moja iliyofungwa. Tumeziona taarifa zao kuhusu kupigwa bomu bandari ya Beirut, kwa hivyo wakajigawanya kama "wanaounga mkono na wanaopinga" na suala hilo lilimalizwa kwa tamthilia chafu! Hivi ndivyo wanavyofanya na kambi ya Ain al-Hilweh. Wao huchochea zana za migogoro na kushinikiza moto wa ugomvi ndani ya kambi, licha ya mabomu kuanguka kwenye vichwa vya watu katika kambi ya Ain al-Hilweh na maeneo yake ya karibu.

Hii ndio hali ya Waislamu leo mashariki na magharibi mwa dunia: njama, umwagaji damu, kuhamishwa makao na udhalilifu, tangu kuanguka kwa dola ya Kiisilamu na kukoloniwa kwetu na Magharibi kafiri. Hatutakuwa na uwepo wa kweli na ikhlasi hadi tutakaporegesha tena njia yetu ya kwanza katika Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Dola, ambayo ni mchungaji wa kweli wa mambo ya wale wanaobeba uraia wake, iwe ni Waislamu au wengineo. Inawapa njia za staha za kuishi, huhifadhi damu yao, kulinda heshima yao, na inaregesha matukufu yao. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt), ambaye hujibu dua za wale wanaohitaji, kwamba hili litatokea hivi karibuni.

[أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ أَإِلَهٌ مَّعَ اللهِ قَلِيلاً مَّا تَذَكَّرُونَ]

“Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia.” [An-Naml: 62].

H. 27 Safar 1445
M. : Jumanne, 12 Septemba 2023

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu