بسم الله الرحمن الرحيم
Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir Wilayah ya Tunisia
Mustakabali wa Vizazi vya Vijana nchini Tunisia...
Pazia la Sheria Fisadi na Mfumo wa Elimu Uliofeli Yaonyesha Mgogoro wa Kimfumo
(Imetafsiriwa)
Wizara ya Wanawake na Watoto ilitangaza matokeo ya ripoti ya takwimu juu ya arifa za hali zilizo hatarini za watoto na kuwatishia watoto kwa sheria ya miaka 2020 na 2021, iliyowakilishwa na uzinduzi wa jukwaa la ulinzi wa watoto ambalo hutoa uwezekano wa arifa ndogo, baada ya kupokea arifa zaidi ya 20,000 mwaka 2022, akinyooshea kidole cha lawama kwamba vitisho vingi ambavyo mtoto huanikwa kwavyo na kuarifiwa viko katika mazingira ya familia kwa kiwango cha asilimia 60 ya arifa zote, na kuongeza kuwa asilimia ya arifa zinazohusiana na uzembe wa wazazi na kushindwa kwao kutunza na kuelimisha zilifikia asilimia 50.9 mwaka 2021.
Katika mwezi wa sasa wa Januari 2023, Wizara ya Elimu ilifanya mchakato wa mashauriano ya ndani katika ngazi ya mifumo ya elimu kuhusu kutoa usomaji muhimu na mapendekezo ya kuhakiki mfumo wa nidhamu shuleni ulioainishwa katika Waraka Na. 91/93 wa 1991, kutokana na mabadiliko ya sheria jumla na mabadiliko yaliyoshuhudiwa na taasisi za elimu, ambazo zilionyeshwa hasa na kutofaulu kwa mfumo wa nidhamu katika kurekebisha tabia ya wanafunzi katika mazingira ya shule.
Mazingira ya shule yanashuhudia kuongezeka kwa kiwango cha ukatili unaoelekezwa na wanafunzi kwa waelimishaji, ambao umefikia hatua ya majaribio ya mauaji.
Na sisi katika Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia tuna wasiwasi katika kusema yafuatayo:
1- Kutokuwa na ulinganifu katika njia ya miundo na taasisi za serikali kunaonyesha ukosefu wa usawa wa kifikra unazisukuma kutokana na mfumo wa kisiasa kutokuwa na msingi thabiti wa kifikra unaozingatia kanuni moja, na tunaifafanua hapa kwa ujasiri na imani katika kanuni ya Uislamu wa kweli ambao hauwezi kubadilishwa kwa suluhisho la kimsingi kwa tatizo la kujenga vizazi vichanga.
2- Imeelezwa katika Kanuni Jumla za Mfumo wa Nidhamu waraka wa 91, “Uhuru sio mnyoofu kwani ni fahamu ya kinadharia isipokuwa itofautishwe na matamanio ya hamu, na sio nyoofu kwani ni thamani ya kimaadili isipokuwa tu itofautishwe na aina zote za ulegevu na kutojali.” Na hapa tunaona baraka na matokeo ya nukta kianzio hii potovu ya kifikra kwa kuzingatia fahamu ya Kimagharibi ya uhuru katika mfumo wetu wa kifikra na kielimu, ambayo ilitupeleka moja kwa moja kwenye ugomvi wa matamanio, kuanguka kwa akhlaqi, ulegevu na uzembe, pamoja na kile ambacho waelimishaji wanateseka kwacho kila siku katika taasisi za elimu cha unyanyasaji na dhulma za kimaneno na kimwili kutoka kwa mwanafunzi bila msaada wowote, ambapo Wizara ya Wanawake haisikii firimbi ya onyo.
3- Dori ya Wizara ya Wanawake iliamuliwa na wakoloni kupitia mashirika ya kimataifa kama vile UNICEF, ambayo inaunda ramani ya kifikra inayotokana na kubomoa muundo wa familia na kuuchafulia sura kama kiota cha asili kwa mtoto chini ya safu ya tuhuma na takwimu zilizotiwa chumvi ili kuunda mfumo unaoruhusu upitishaji wa kanuni na sheria zaidi zinazotufanya sisi sote kuwa wahalifu. Hili linadhihirika kwa kuwa wito wa kurekebisha uchapishaji wa mfumo wa nidhamu unahitimishwa kwa onyo kwamba mapendekezo lazima yahusu jarida la haki za mtoto na nususi za sheria zilizotolewa na UNICEF, katika pambano la wazi kwa maadili ya watu wa nchi hii, maadili ya Uislamu.
4- Sera ya kuwadunisha waelimishaji - kwa miaka mingi - iliyotekelezwa na serikali, ilizuia misheni yao kwa kikundi la sheria tasa ambazo kimsingi ziliwanyima haki zao za kuheshimiwa na kuthaminiwa. Leo, Wizara ya Wanawake inaendelea kushambulia umbile la familia na mamlaka ya wazazi ndani yake chini ya anwani ya kirongo: "Watoto wako chini ya tishio" na "Watoto wako hatarini." Hili linakuja kama mwendelezo wa mbinu ya kushambulia mamlaka ya mchungaji yaliyoidhinishwa na Uislamu: mchungaji katika dola, mchungaji shuleni, mchungaji katika familia, ambayo mfumo wa kisekula huyaita kwa maneno kama vile wima, mfumo dume, na mamlaka ya baba mkuu, kwa kupotosha na uzushi.
5- Uhusiano wetu na kile ambacho vizazi vya vijana vinaishi kwacho katika familia na kile wanachoishi kwacho katika mazingira ya shule hutokana na imani kwamba nidhamu ya tabia ya watoto wetu na uboreshaji wa maadili, matendo na mahusiano yao ni matokeo ya kupandikiza fahamu angavu, kutoka katika chimbuko la Shariah ya Mwenyezi Mungu na hukmu zake, ambazo zinaweza kutekelezwa tu kwa kupatikana kwa utashi wa kisiasa unaoegemezwa juu yake, yaani Dola ya Khilafah ambayo huhakikisha kuundwa kwa mazingira ya kisheria yanayofaa kwa ajili ya kuenea kwa Fikra za Kiislamu kama msingi wa tathmini na uamuzi, na hivyo juhudi za familia na taasisi ya elimu zinaweza kuja pamoja chini ya mfumo halali wa kisiasa ili kuunda vizazi kama anavyotaka Mwenyezi Mungu Mtukufu.
H. 7 Rajab 1444
M. : Jumapili, 29 Januari 2023
Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Tunisia