Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
| H. 10 Jumada I 1447 | Na: H 1447 / 024 |
| M. Jumamosi, 01 Novemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Kukamatwa kwa El Fasher Ndio Mwisho wa Mpango, Au Bado Kuna Mishale Zaidi Yenye Sumu Kwenye Ala?
(Imetafsiriwa)
Sudan imeshuhudia mabadiliko makubwa katika vita vyake, ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya miaka miwili, huku Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vikichukua udhibiti wa El Fasher, ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan katika eneo la Darfur magharibi mwa Sudan. Hii imeimarisha udhibiti wao katika eneo hilo. Mapigano sasa yamejikita katika eneo jirani la Kordofan.
Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya raia 36,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wamehamishwa kutoka El Fasher tangu Jumapili iliyopita kutokana na mapigano. Wamepitia ukiukwaji mwingi, ikiwa ni pamoja na mauaji yanayotokana na kitambulisho, uchomaji moto, ubakaji wa wasichana na wanawake, uporaji, na utekaji nyara kwa ajili ya fidia. Wengi wamekimbilia Tawila, mji ulio umbali wa kilomita 70 ambao tayari unahifadhi karibu watu 650,000 waliohamishwa, na kuzidisha hali ya kibinadamu katika mji huo, ambao umekuwa kimbilio la mwisho salama kwa wakaazi kote Kaskazini mwa Darfur. Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu janga la kibinadamu huko El Fasher kufuatia tangazo la Burhan la kujiondoa kwa jeshi. Ulisema kwamba Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vimefanya ukatili mpya huko, huku video zikiwaonyesha wanachama wao wakitekeleza mauaji ya halaiki ya raia na wafungwa kutoka jeshi na vikundi washirika. Mtandao wa Madaktari wa Sudan, shirika la kibinadamu, uliishutumu RSF kwa kuwaua wagonjwa na wenzao katika hospitali pekee inayofanya kazi huko El Fasher. Serikali ya Sudan, ambayo imeanzisha mji wake mkuu wa muda huko Port Sudan mashariki ya mbali mwa nchi badala ya Khartoum, ilisema kwamba vitendo vya RSF ni sawa na mauaji ya halaiki, ikidai kuwa wamewaua takriban raia 2,000 tangu walipochukua udhibiti wa mji wa El Fasher. Wale wanaojaribu kukimbia mji huo pia wamekabiliwa na unyanyasaji, ikiwemo ubakaji, uporaji, na utekaji nyara kwa ajili ya fidia. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF alisema kwamba karibu watoto 130,000 huko El Fasher, ambao wamenaswa kwa zaidi ya siku 500, wako katika hatari ya ukiukwaji mkubwa, ikiwemo mauaji, ulemavu, utekaji nyara, na unyanyasaji wa kijinsia. Alisisitiza katika taarifa mmoja kwamba hakuna mtoto aliye salama huko, kutokana na uhaba wa chakula, maji, na dawa, na hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili.
Kama kawaida, Baraza la Usalama lilionyesha wasiwasi wake kuhusu ukatili ulioripotiwa kufanywa na RSF dhidi ya raia na kutoa wito kwa pande zote kwenye mzozo huo kuzingatia mara moja makubaliano ya kusitisha mapigano. Baraza hili hili, ambalo halikuwepo wakati wote wa vita, hata kujiepusha na kulaani na kukosowa, kwa sababu dola kubwa au zenye ushawishi ndani yake ndizo zinazochochea mzozo nchini Sudan.
Enyi Watu wa Sudan: Mzozo nchini Sudan na kwengineko utaendelea kutumika kama kichochea kwa ajili ya matarajio ya kimataifa na mzozo wao, pamoja na mipango yao miovu, uingiliaji kati, na upatiaji silaha wa makundi yanayopigana ili kufikia udhibiti kamili juu yao? Wanawake na watoto wenu wamekuwa wakiteseka kwa zaidi ya miaka miwili kutokana na mzozo huu wa umwagaji damu, ambao unatumikia maslahi ya Magharibi na washirika wake tu katika kudhibiti hatima ya Sudan, nchi ambayo wameitamani kwa muda mrefu kwa eneo lake la kimkakati na rasilimali. Ni kwa maslahi yao kuichana na kuigawanya. Kuchukua kwa RSF mji wa El Fasher ni kiungo chengine katika silsili hii ya matukio, ambayo kwayo Amerika inatafuta kuchonga eneo la Darfur, kuimarisha ushawishi wake nchini Sudan, na kuondoa ushawishi wa Uingereza huko.
Suluhisho haliko katika serikali ya kidemokrasia wala katika serikali ya kijeshi, bali ni katika kuondoa ushawishi wa Magharibi mkoloni kafiri katika aina na madhihirisho yake yote na wafuasi wake. Suluhisho ni katika kuuleta Uislamu madarakani, chini ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
[إِنْ يَنْصُرْكُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ وَإِنْ يَخْذُلْكُمْ فَمَنْ ذَا الَّذِي يَنْصُرُكُمْ مِنْ بَعْدِهِ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُون]
“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Aal-i-Imran: 160]
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |



