Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 548
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Taarifa ya mwisho ya Mkutano wa Waarabu, ulioandaliwa na mji mkuu wa Iraq, Baghdad mnamo tarehe 17 Mei 2025, ilisisitiza haja ya kuleta misaada ya kibinadamu mjini Gaza. Watawala wa Waislamu, Waarabu na wasiokuwa Waarabu, wamezuia majeshi ya Waislamu kupigana na Mayahudi, kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu. Mtume ﷺ ametuambia kuwa kupigana na Mayahudi na kuwashinda kunaleta malipo makubwa.
Trump alianza ziara yake nchini Saudi Arabia mnamo Mei 13, 2025, ikifuatiwa na Qatar mnamo Mei 14, 2025, akihitimisha safari yake nchini Imarati mnamo Mei 15, 2025, na kuhitimisha ziara yake mnamo Mei 16, 2025. Kisha aliandamanisha ziara hii kwa udanganyifu wake kwamba hatazuru umbile la Kiyahudi, kuwakejeli wajinga wanaodai kuwa uungaji mkono wa Trump kwa umbile la Kiyahudi umetikiswa! Hii ni licha ya ukweli kwamba umbile la Kiyahudi lilipanua mashambulizi yake kwenye Ukanda wa Gaza baada ya Trump kuondoka katika nchi hizo tatu.
Hatimaye, Dhalimu Trump Anahitimisha Ziara yake katika Kanda hii!
Trump alitangaza kwa mshangao jana, Jumamosi, katika chapisho kwenye jukwaa lake la Ukweli wa Kijamii (Truth Social platform), kwamba "Baada ya usiku mrefu wa mazungumzo yaliyopatanishwa na Marekani, ninafurahi kutangaza kwamba India na Pakistan zimekubali kusitishwa kwa mapigano kamili na mara moja, "na kuzisifu nchi zote mbili kwa kutumia busara na akili kubwa." (Al Jazeera, 11/5/2025) ... ni upi ukweli katika uhasama na mzozo huu? Je, Mkataba wa Maji wa Indus ni nini haswa ambao India imeusitisha kwa muda? Je, Marekani inahusika katika kuanzisha shambulizi hilo na pia kulisitisha?
Kisimamo cha Nusra Mbele ya Bunge la Lebanon kwa ajili ya Waislamu waliowekwa Kizuizini kilicho andaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon.
Vyanzo vya kimatibabu vimeandika kuuawa shahidi kwa Wapalestina wasiopungua 42 kutokana na ulipuaji mabomu wa umbile la Kiyahudi katika Ukanda wa Gaza tangu alfajiri ya Jumatatu, 12 Mei 2025. Uvamizi huo ulianza tena jioni baada ya kusimama kwa saa kadhaa, ambapo mwanajeshi mmoja aliyekamatwa wa umbile la Kiyahudi aliachiliwa huru.
Mabadilishano ya makombora kati ya Pakistan na India yanaendelea katika njia nyingi za kusitisha mapigano huko Kashmir baada ya India kushambulia kwa mabomu maeneo tisa ndani ya Pakistan usiku wa Mei 6, ambayo ilisema ni "miundombinu ya kigaidi iliyohusika na shambulizi la silaha huko Kashmir" mwezi uliopita. Suluhisho la kivitendo la kusonga mbele haliwezi kuwa mzozo mdogo, lakini lazima liwe ukombozi wa kina wa maeneo yanayokaliwa kimabavu.