Jumamosi, 04 Rajab 1446 | 2025/01/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  13 Muharram 1444 Na: Afg. 1444 H / 02
M.  Alhamisi, 11 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Ameuawa Shahidi katika Mkoa wa Ghazni
(Imetafsiriwa)

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo. [33:23]

Abdul Aziz Mohammadi ambaye alikuwa mwanachama mkuu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan katika mkoa wa Ghazni, ameuawa shahidi na watu wasiojulikana wenye silaha usiku wa Jumanne. Aliteswa vibaya sana na kupigwa risasi kikatili machoni huku mikono, miguu na macho yake yakiwa yamefungwa alipokuwa akielekea nyumbani kwake kutoka kwa mpango wa Dawah.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inauona ukatili na unyama huu haramu kuwa ni kitendo cha ajabu cha ugaidi na mauaji, na inatangaza kwamba kulinda maisha ya Waislamu ni moja ya wajibu msingi wa serikali ya Kiislamu ambao utahakikishwa kupitia kutabikisha Uislamu. Hivyo basi, huu ni wajibu wa serikali ya Kiislamu kulinda maisha, mali, heshima na matukufu ya Waislamu kwa kutabikisha mfumo wa Kiislamu, na kujikomboa kutokana na mzigo wa majukumu katika maisha haya ya dunia na Akhera. Kwa vyovyote vile, Waumini wana agano na Mola wao Mlezi wa kuyatoa mhanga maisha yao na mali zao na vipenzi vyao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na katika njia ya Uislamu, kurahisisha njia kwa ajili ya utawala wake wa kiulimwengu. Hizb ut Tahrir, katika miaka 70 ya mapambano yake ya kisiasa na kifikra, imethibitisha kwamba ina imani thabiti katika lengo lake (Kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida kwa kubeba mapambano ya kisiasa na kifikra kiasi kuwa hakuna vikwazo, pingu wala aina yoyote ya mateso na vitendo vya kuhofisha vinavyo weza kutikisa na kupotosha imani yake, wala haitafanya hivyo katika siku zijazo. (In Sha Allah)

Abdul Aziz alikuwa mmoja wa wabebaji Dawah wanyofu na wachangamfu aliyejitolea maisha yake kwa kupambana bila kuchoka kwa ajili ya kuhuisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamishwa dola ya Khilafah. Alibaki mwaminifu kwa agano lake na Mwenyezi Mungu (swt).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Afghanistan inatoa rambirambi kwa wanachama wote wa Hizb ut Tahrir, wapiganaji wa Kiislamu na Waislamu wote kuhusiana na tukio hili la kusikitisha. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) akukubali kifo chake cha kishahidi, na awape subira na ujira familia yake na jamaa zake, na awadhalilishe wauaji wake kwa njia ya kufedhehesha.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu