Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  7 Safar 1444 Na: Afg. 1444 H / 03
M.  Jumamosi, 03 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kifo cha Kishahidi cha Mowlavi Ansari ni Muendelezo wa Mauaji ya Ajabu ya Mitandao ya Kijasusi!
(Imetafsiriwa)

Mowlavi Mujib-ur-Rahman Ansari, mzungumzaji fasaha na khatibu wa Msikiti wa Gazargah, aliuawa shahidi katika mlipuko mmoja pamoja na watu 17, huku makumi ya wengine wakijeruhiwa ndani ya Msikiti wa Gazargah wa mkoa wa Herat. Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan inalaani vikali kabisa shambulizi hili la kikatili na kitendo cha kigaidi, ikilizingatia kuwa ni kinyume na ubinadamu na mafundisho ya Shariah. Mwenyezi Mungu (swt) akubali kuuawa kishahidi mashahidi hao, awape afueni ya haraka waliojeruhiwa, na awape subira na/au ujira mwema jamaa zao.

Sio mara ya kwanza tangu tushuhudie mauaji ya wanazuoni wanaoheshimika, viongozi na wazee wenye ushawishi wa Ummah huu, haswa katika kipindi cha miaka 20 ambapo Afghanistan ilikuwa chini ya ukaliwaji na uvamizi wa kimabavu -  huku msururu wa mauaji yaliyolengwa wasomi na viongozi wenye ushawishi yakiongezeka. Wavamizi na mitandao yao ya kijasusi walikuwa wakitekeleza mauaji ya ajabu katika ardhi hii ili kuwatenga, kuwakashifu, na kuwaua wale waliokuwa maarufu miongoni mwa watu na walionekana kuwa kikwazo dhidi ya mipango na njama za wavamizi - kama vile mauaji ya kishahidi ya Mowlavi Ansari ni mwendelezo wa vitendo hivyo vya kijasusi.

Ukaliaji kimabavu kwa kweli ulishindwa nchini Afghanistan, lakini wavamizi bado hawajatulia. Maadui wa Uislamu wanakusudia kutekeleza mashambulizi yao madhubuti dhidi ya maadili ya Kiislamu, serikali ya sasa, wanazuoni na viongozi mashuhuri wa jamii hii kwa kutumia mbinu tofauti ili kutoa changamoto na kuishinikiza Imarati ya Kiislamu ya Afghanistan (IEA) kwa upande mmoja, na kuwamaliza wale wanaowaona kuwa kizingiti katika njia yao kwa upande mwingine. Kwa hivyo, Imarati ya Kiislamu lazima itambue kwamba ukoloni wa Magharibi na washirika wao wa kieneo wana nyuso nyingi - wao [maadui] wakati mwingine huonekana na mikono iliyojaa misaada ya kifedha kama mashirika ya kibinadamu, wanaharakati wa kiraia, vyombo vya habari huku pia wakiwezesha maandamano, kutoa mashinikizo ya kisiasa, na kubeba shughuli za kijasusi zisizojulikana na mauaji yanayolenga.

Tulikuwa tayari tumefichua njama hizo za adui na kuwatahadharisha viongozi wa jamii juu ya vitendo hivyo mara kadhaa; leo, tunarudia kwa mara nyingine tena ukweli kwamba nchi za Magharibi daima hutumia siasa za pande nyingi na ngumu katika kuamiliana na Waislamu. Kwa sasa wanaonekana wakizungumzia juu ya misaada ya kibinadamu na haki za binadamu, lakini kwa kweli, wanazuia kuundwa kwa serikali yenye nguvu na imara ya Kiislamu nchini Afghanistan na eneo hili. Kwa hivyo, tunapaswa kutambua kwamba ni kupitia kushikamana kwa karibu na Ummah na kutabikisha kikamilifu Uislamu pekee, ndipo tutakapo weza kuepuka fitna za ndani, kuangamiza njama za kigeni, kuwaadhibu wahalifu na kuhakikisha kwamba mali na maisha ya Waislamu yanalindwa. Hatupaswi kuchukulia jambo hili kuwa la kawaida kwamba kuunda tu kitambulisho thabiti vha Kiislamu na kufufua jamii iliyotulia pekee ndiko kutatuwezesha kusimama dhidi ya maadui zetu wa kigeni mithili ya ngome ya chuma kuvunja mipango na hila zao mbovu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu