Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari

H.  14 Rajab 1442 Na:
M.  Ijumaa, 26 Februari 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katika Kumbukumbu ya Karne Moja ya Kuvunjwa kwa Khilafah… Isimamisheni Enyi Waislamu

(Imetafsiriwa)

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote, Mola Mlezi wa viumbe vyote, Muumba wa mbingu na ardhi; Muumba wa wanadamu, mtumilizaji manabii na mitume, na muonyaji wa mataifa kupitia vitabu, Bwana wa hesabu, Pepo na Moto, anayetawala viumbe vyote.

Na rehema na amani zote zimshukie mwombezi wa Umma wa Kiislamu, na shahidi kwa hilo katika ubebaji ulinganizi kwa watu wengine wote, bwana wa viumbe Muhammad (saw) na jamaa zake na maswahaba zake kwa jumla.

Sisi hapa leo tuko mbele ya kumbukumbu nyengine ya kuvunjwa kwa Khilafah, lakini wakati huu inageuka ukurasa wake wa mia moja; Ndio maana lazima turudi nyuma kuangalia kile kilichokuwa katika karne hii yote tangu kutoweka kwa Khilafah. Miaka mia moja hii imekuwa katika pande mbili. Upande mweusi, wenye huzuni, na upande mwengine wenye kuchomoza na kutoa bishara njema, wenye kutia moyo matumaini ya kuendelea kutafuta na kufanya kazi. Ama upande wa giza wa enzi hii ulikuwa maarufu zaidi kati ya mambo mawili.

Ama kuhusu jambo la kwanza, ni kutelekezwa kwa utawala wa Uislamu, kwani Umma wa Kiislamu na nchi zake hawakuwahi kutoka katika utawala wa Uislamu wote kwa kipindi kimoja, kama ilivyotokea zama hizi. Leo, hakuna tena sehemu yoyote ulimwenguni ambayo iko chini ya kivuli cha utawala wa Uislamu hata kidogo; Hii ni huku Umma ukiwa una idadi ya karibu bilioni mbili! Badala yake, Waislamu wenyewe katika kipindi cha zama hizi, na kwa sababu ya ukali wa kushikamana kwao na kile alicho nacho kafiri Magharibi, walianza kushindana kujaribu aina tofauti tofauti za utawala wa kikafiri juu yao wenyewe, wakisahau kwamba Magharibi huyu huyu ndiye yule yule mkoloni kafiri ambaye alishirikiana nao na kuzikalia nchi zao. Na kutokana na ukali wa hali hii, ya kuwa mbali na dini ya Mwenyezi Mungu, hukmu za Uislamu, baada ya karibu miaka arubaini ya kuvunjwa kwa Khilafah, zilifikia ukingo wa kukunjika na kumalizika.

Ama jambo la pili ni majanga, ambayo Umma wa Kiislamu umepata kutokana na kukosekana kwa Khilafah. Licha ya ukweli kwamba Umma ulikuwa umepatwa na majanga mengi katika zama zake za awali, kutokuwepo kwa Khilafah katika kipindi cha miaka 100 iliyopita kumeruhusu kukusanyika misiba katika Umma wa Kiislamu ambayo haikuwahi kukusanyika kwa wakati mmoja. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«يُوشِكُ الْأُمَمُ أَنْ تَدَاعَى عَلَيْكُمْ كَمَا تَدَاعَى الْأَكَلَةُ إِلَى قَصْعَتِهَا»

"Mataifa yako karibu kukuitana dhidi yenu kama wale wanaokula wanavyoitana kwenye bakuli lao."

Misiba ya kimada bado inaendelea na haijasimama, Al-Aqsa iliyobarikiwa inachafuliwa na Mayahudi, na damu tukufu ya watu wa Iraq imemwagika kwa miongo kadhaa, Ash-Sham imevunjwa miji yake na kuhamishwa watu wake, Yemen imeangamizwa na mgonjwa mwenye njaa, Misri inavunja misikiti yake na watu wake hutumia siku zao kati ya umaskini na uonevu, na Libya imepasuliwa kati ya udhalilishaji wa vibaraka na moto wa wasaliti, Sudan ni maskini licha ya utajiri wake, Burma inatesa Waislamu mbele ya masikio na macho ya ulimwengu. Urusi na watawala wa Asia ya Kati wanaendelea kupigana na Uislamu na kuwatesa Waislamu, na Kashmir inamilikiwa na Mabaniani na kuwanyanyasa watu wake, na India inatekeleza udhalilishaji wa Waislamu ndani yake, na wao ndio wenye nchi hiyo, na China ya Kikomunisti inajaribu kufuta Uislamu kutoka kwa akili za Waislamu wa Uyghur kwa kuwalazimisha kufanya vitendo vilivyoharamishwa. Afghanistan inavutwa kwenye udhalilishaji wa mapatano, na Mali inachinjwa na Ufaransa. Mbali na majanga mengine yaliyowapata Waislamu wa Ufilipino, Algeria, Bosnia, Chechnya, Palestina, Lebanon, Eritrea, Somalia, Uzbekistan, Pakistan, Azerbajan, Afrika ya Kati, Sri Lanka, Bangladesh, Indonesia, India, Liberia, Thailand, Uhabeshi na kwengineno tangu kuvunjwa kwa Khilafah.  Kufeli kwa majeshi ya Waislamu kwa Umma wao kuliongeza mzigo wa majanga haya juu yake. Ambapo majeshi ya Uturuki, Pakistan, Misri, Algeria, Iraq, Indonesia, Hijaz, Syria na majeshi mengine ya Kiislamu yamewafelisha watu wa Umma wa Kiislamu. Wote hawa waliwafelisha Waislamu katika mazingira magumu zaidi, lakini badala yao walitoa silaha, vifaa na mafunzo yao kuwakandamiza Waislamu na sio wengine.

Ama misiba ya maadili, hakuna hata mmoja uliofifia hadi Magharibi mkoloni kafiri inatoe zana mpya na kuhuisha janga jipya. Kuanzia uhadaifu wa ukomunisti hadi kudharau sheria ya Kiislamu, mpaka kashfa ya ugaidi, wazo la Uislamu huria, mradi wa demokrasia ya Kiislamu, hadi kudhihiri kwa hofu ya Uislamu (Islamophobia). Kwa hivyo mashambulizi hayo dhidi ya Uislamu na Waislamu, imani zao, sheria zao na nabii wao yamekuwa ya mitindo leo katika jamii za kilimwengu kutoka mashariki ya mbali hadi magharibi mbali. Kutoka New Zealand, ambapo Waislamu bado wanahangaishwa baada ya mauaji yao, kupitia katika nchi za Ghuba ya Kiarabu, ambapo Waislamu wanaingizwa katika maadili ya hadhara ya Kimagharibi, na haya sio ya mwisho katika msururu, uhalalishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi, pamoja na Madina na Makka, ambazo zimezingirwa na uasherati wa Mamlaka ya Burudani, kuzifikia nchi za Kimagharibi za kikoloni za kikafiri, ambapo Ufaransa inawaongoza katika kampeni za kuudhalilisha Uislamu na nabii wake na kubuni sera za kuwatesa Waislamu katika maisha yao. Na usisahau nafasi ya mtandao wa ulimwengu, ambayo inadhibitiwa na kampuni za kirasilimali ambazo zimehakikisha, kwa niaba ya serikali za kimagharibi za kikoloni za kikafiri, kunyamazisha kila ukurasa au akaunti ambayo unaangazia uongozi wa kifikra wa Kiislamu. Vivyo hivyo, wakati Umma wa Kiislamu ulipohitaji wanachuoni wake, ambao wanaweza kuiangazia njia ya haki, wakati Magharibi ilikuwa ikitangaza sumu zake na kueneza kupotoka kwake, katika nyakati hizo ngumu, wanachuoni wa kiserikali, haswa viongozi wao katika majukwaa ya vyombo vya habari na wale wanaosimamia vikundi vya wasomi na fatwa waliundwa. Kwa hivyo waliruhusu riba, kupigana katika vikosi vya wapiganaji makafiri, wakaondoa pazia, wakijumuika katika hadhara ya Kimagharibi, na kushiriki katika utawala wa kikafiri. Bali, hakika baadhi yao walipiga vita kazi ya kurudisha utawala wa Uislamu, kwa hivyo kufeli kwao ikaongeza katika janga la kimaadili.

Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimiza nuru yake

Ama upande wenye kuchomoza bishara njema, ni kwamba licha ya nguvu na udanganyifu ambao makafiri Magharibi wamekusanyika dhidi ya Uislamu na Waislamu katika kipindi cha miaka 100 ili kuzuia Uislamu kurudi kwa uhai, Mwenyezi Mungu amewaaibisha na kuwathibitisha wenye ikhlasi katika Umma, na akawaafikia kwa kile kinachomridhisha. Wabebaji ulinganizi walikuwa na dhamira kali zaidi kuliko ujabari wa dola za wakoloni, walikuwa na nguvu zaidi katika imani kuliko maadui wa Uislamu na madhalimu, na walithibitisha ukweli zaidi kuliko wale ambao walikuwa na maradhi nyoyoni mwao. Hawakuruhusu Umma unyakuliwe kutoka mikononi mwao, na waliendelea kujitahidi kwa mwongozo wake na walitoa kafara kubwa kwa ajili hiyo. Utawashuhudia wengi wao, na wakiteswa na kuangamizwa katika pembe za dunia, na wakifukuzwa katika nyumba zao kama Waislamu wa kwanza walivyofukuzwa. Na kwa kuwa radhi za Mwenyezi Mungu ndizo zilizokuwa lengo lao na mwitikio ulioongezeka wa Umma ndio uliokuwa faraja yao, hivyo basi walikuwa na thabati na Umma pia ukawa na thabati pamoja nao. Na sisi hapa leo tuko mbele ya Umma ulilojaa maisha na uliojaa vijana wanyofu, unaotambua kuwa dini yake ni ya haki, na unaotafuta njia ya kufikia umoja wake. Unapewa bishara njema na Quran na Sunnah kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ataurudishia utukufu wake, kufungua nchi na kueneza hadhara yake.

Mwanzo wa hatua ya kuporomoka kwa hadhara ya  Kimagharibi

Kwa upande wa Magharibi mkoloni kafiri, imeanza hatua kuporomoka, kama vile Ujamaa wa Mashariki alivyoporomoka mbele yake. Ufaransa ilitangaza kifo cha fikra yake wakati alipoanza kugeuka dhidi ya itikadi yake ya kisiasa kutunga kanuni dhidi ya Uislamu. Kikosi cha Jumuiya ya Ulaya kilifichuka wakati kilipoimba katika bunge lake kusherehekea kujitenga kwa Uingereza kutoka kwake. Amerika iliongeza hali ya kutokuelewana kati ya nchi za Magharibi wakati ilipoondoa barakoa yake na kufunua sura yake ya kweli, na ikajichagua yenyewe rais ambaye hasiti kutangaza malengo ya matumizi ya nchi yake, na hajali kuhusu maneno ya kijeuri kwa washirika wake. Kwa hivyo, nchi kubwa zaidi Magharibi ikaachana na jukumu lake kama kiongozi wa maadili, bali Amerika ikawa mchochezi mkuu wa mzozo mbaya wa kiuchumi kati ya dola zake.

Kisha Mwenyezi Mungu akatuma virusi vya Korona kwenye ulimwengu huu ili kuitandika kwavyo hadhara ya Kimagharibi machoni ya kile inachokitukuza, ambacho ni uchumi, na janga la Korona limefanya uchumi wa mifumo ya kirasilimali kuwa mkali zaidi kuliko ilivyofanya katika miili ya wanadamu. Virusi vilipanda juu ya mgogo wa utandawazi. Mashine hiyo ya uchumi yenye ulafi ambayo serikali za kirasilimali ziliiunda ili kujishindia masoko ya ulimwengu. Mashine ya utandawazi ilizuia kufunga milango usoni mwa virusi hivi. Nchi zimekuwa zikisita kufunga mipaka yao kwa janga hilo kwa miezi kadhaa, hadi baada ya muda kupita. Na walipoanza kukabiliana na ugonjwa huo, Mwenyezi Mungu hakuwaongoza kwa njia sahihi ya kukabiliana na janga hilo, kana kwamba walikuwa wakiongozwa na hatima yao kwa miguu yao. Kwa hivyo, janga la Korona lilikuwa sababu ya ziada ya kuporomoka na kugawanyika kwa Magharibi. Kwa sababu yake, nchi za Jumuiya ya Ulaya zilianza kubadilisha misafara ya kibiashara ya baadhi yao ili kupata vifaa vya matibabu. Pia ni kwa sababu hiyo kwamba mzozo kati ya kampuni za kirasilimali huko Amerika juu ya kufungua na kufunga uchumi umeongezeka, na mzozo kati yao ulifikia hadi katika uchaguzi wa urais, ukigawanya jamii katika mgawanyiko mkali, na kufikia hatua ya wafuasi wa Trump kushambulia jengo la Congress, hekalu kubwa la demokrasia duniani. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿تَحْسَبُهُمْ جَمِيعاً وَقُلُوبُهُمْ شَتَّى

"Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali." [Al-Hashr: 14]

Na Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿لَوْ أَنفَقْتَ مَا فِي الأَرْضِ جَمِيعاً مَّا أَلَّفَتْ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلكِنَّ اللّهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ﴾

"Na lau wewe ungeli toa vyote viliomo duniani usingeli weza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha." [Al-Anfal: 63]

Umuhimu wa kumbukumbu ya miaka 100

Umuhimu wa kumbukumbu ya kuvunjwa kwa Khilafah wakati huu ni wa pande mbili, ama upande wa kwanza ni ya kutisha na kufazaisha, kwa sababu kugeuza ukurasa wa mia moja inamaanisha kuwa tumefika karne moja bila utawala wa Uislamu, kwa hivyo tunahofia kwamba kizazi hiki cha Umma wa Kiislamu kisiwe kimeingia katika kundi la watu wa karne. Na watu wa karne ni wale ambao Quran imewalaani kwa kushindwa kusimamisha amri ya Mwenyezi Mungu kwa karne nyingi za nyakati, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿فَلَوْلاَ كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُوْلُواْ بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ الْفَسَادِ فِي الأَرْضِ إِلاَّ قَلِيلاً مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ وَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُواْ مَا أُتْرِفُواْ فِيهِ وَكَانُواْ مُجْرِمِينَ﴾

"Basi mbona hawakuwamo katika watu wa kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanao kataza uharibifu katika nchi, isipo kuwa wachache tu, ambao ndio tulio waokoa? Na walio dhulumu walifuata starehe zao, na wakawa ni wakosefu." [Yunus: 13]

Na Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ مِن قَبْلِكُمْ لَمَّا ظَلَمُواْ وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ وَمَا كَانُواْ لِيُؤْمِنُواْ كَذَلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ﴾.

"Na kwa yakini tumekwisha ziangamiza kaumu za kabla yenu walipo dhulumu, na waliwajia Mitume wao kwa Ishara zilizo wazi; lakini hawakuwa wenye kuamini. Ndio kama hivyo tunavyo walipa watu wakosefu." [Yunus: 13]

Ama upande wa pili, ni kwamba Umma wa Kiislamu umejaribu kila aina ya miundo ya serikali katika kipindi cha miaka 100 iliyopita. Umejaribu ujamaa, ufalme, udikteta, utaifa, Ubaathi, uzalendo, demokrasia, shirikisho, ubunge, urais, na umakundi. Na umejaribu yote katika aina zake zote, usekula kamilifu na uliochanganywa na Uislamu. Halafu baada ya kujaribu miundo hii yote ya serikali ilianguka moja baada ya moja. Mapinduzi ya Kiarabu yalikuwa harusi kubwa zaidi kuletwa mtaani kutoka kwa raia wa Umma wa Kiislamu, hadi wimbo wa "watu wanataka kuangushwa kwa serikali" ukawa ni jinamizi la serikali na dola kuu.

Ndio, Umma imejaribu miundo yote ya serikali isipokuwa kutawala kwa Uislamu safi kama ilivyokuja nao na Bwana wetu Muhammad (saw) na kama walivyoutabikisha Maswahaba wa watukufu bila ya kuongeza au kupunguza.

Kwa sababu hizi mbili, na kwa kupita kwa kumbukumbu ya miaka 100 ya kuvunjwa kwa Khilafah, tunaulingania Umma wa Kiislamu na wanachama wake wote, vikundi, duru, shughuli, haiba, watu wenye nguvu na uthabiti ndani yake, tunawalingania nyote mupate tunu katika mwaka wenu huu na mufanye kazi pamoja na Hizb ut Tahrir chini ya uongozi wa mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Rashtah Mwenyezi Mungu amhifadhi, bila kuchelewa wala kusitasita kukomesha msururu wa misiba na kusimamisha Khilafah Rashida ya kwa njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

"Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume."

#أقيموا_الخلافة

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

 

Mh. Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu