Jumapili, 27 Dhu al-Qi'dah 1443 | 2022/06/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  1 Rajab 1442 Na: 1442 H / 022
M.  Jumamosi, 13 Februari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Afisi kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Yazindua Kampeni kwa Anwani:

"Juu ya Karne Moja ya Kuvunjwa kwa Khilafah… Isimamisheni Enyi Waislamu"

(Imetafsiriwa)

Huu hapa tena umerudi mwezi wa Rajab al-Khair kwetu kutukumbusha kuwa msiba wa kuvunjwa kwa Khilafah ungali unaendelea haujamalizika bado. Mpaka sasa, Waislamu bado hawajairudisha dola ambayo Mtume wao aliwaachia. Tangu mhalifu Mustafa Kemal alipoivunja Khilafah Uthmani mnamo 1342 Hijria sawia na 1924 M, Umma wa Kiislamu umegeuka makaa ya misiba yanayoizunguka pande zote.

Na katika mwaka huu, kumbukumbu ya kuvunjwa kwa Khilafah inafungua ukurasa wake wa 100, na hivyo kukamilisha karne ambayo Ummah wa Kiislamu umenyimwa kuishi chini ya kivuli cha sheria yake tukufu. Bali yule mhakiki wa miongo hii kumi anajua ukali wa mateso ambayo Ummah wa Kiislamu umeishi ndani yake wakati wote huo; Mateso ya kuendelea, yaliyotiwa alama na misiba mfululizo, ambayo Umma wa Kiislamu haukuwahi kuyashuhudia hapo awali.

Kwa hivyo, na chini ya uongozi wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata bin Khalil Abu Al-Rashta, Mwenyezi Mungu amhifadhi, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, ikisaidiwa na mashababu wote wa Hizb ut Tahrir kote ulimwenguni, imezindua kampeni ya kiulimwengu ambayo kwayo watoto wa Ummah wa Kiislamu wanaamshwa ili kufanya kazi na Hizb katika harakati zake za kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Vilevile, Hizb ut-Tahrir inaamsha katika kipindi chote cha kampeni hii, haswa ari ya watu wenye nguvu na uwezo katika Umma wa Kiislamu, ikiwakumbusha juu ya jukumu lao na kuwalingania kuinusuru, kwa hivyo waunganishe mikono yao na mkononi mwake ili kuipa izza Dini hiI ya Mwenyezi Mungu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Kama ambavyo Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir pia inatoa wito kwa vyombo vyote vya habari, miongoni mwa wanahabari na mbinu za utangazaji, haswa Waislamu, kuwa watetezi wa kheri na hivyo kushiriki kuangazia shughuli za kampeni hii, ili waweze hisa ya kheri katika kazi kurudisha Khilafah ambayo Ummah wa Kiislamu unaitamani.

Na kwa hivyo, kwa jina la Mwenyezi Mungu na juu ya baraka ya Mwenyezi Mungu tunazindua kampeni hii: "Juu ya Karne Moja ya Kuvunjwa kwa Khilafah... Isimamisheni Enyi Waislamu," tukimtegemea Mwenyezi Mungu atuafikie kusimama kwa Dini Yake na kuinuka kwa Ummah wake.

Mh. Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu