Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  26 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 015
M.  Jumamosi, 22 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Ujumbe wa Hamas Uliomzuru Muuaji Bashar

«أَلَا وَإِنَّ الإِيمَانَ حِينَ تَقَعُ الْفِتَنُ بِالشَّامِ»
“Jitahidini na Iman, pindi Zitakapotokea Fitna katika Ash-Sham”
(Imerafsiriwa)

Kwa masikitiko makubwa, tulishuhudia ujio wa ujumbe wa Hamas na makundi ya Wapalestina unaoongozwa na Khalil Al-Hayya katika ziara rasmi ambayo ni ya kwanza baada ya Hamas kutangaza mnamo Septemba 15 kwamba itarejesha uhusiano wake na utawala haramu wa Baathi na kurejea kifuani mwa mhalifu Bashar, baada ya mpasuko ambao uliendelea tangu 2012, wakati mkuu wa afisi ya kisiasa ya vuguvugu hilo, Ismail Haniyeh alipohalalisha sababu ya ususiaji huo: "Hatuwezi kuwa upande wa utawala unaoua watu wake, na atakayesimama nasi katika haki, hatutasimama naye katika batili."

Kauli hii kutoka kwa Haniyeh ilikuwa mwanzoni mwa njia ya jinai ya utawala wa dhalimu Bashar ambapo alikuwa bado hajaua Waislamu zaidi ya milioni mbili nchini Syria, na mbwa wake wa kibinadamu walikuwa hawajabaka maelfu ya wanawake wa Kiislamu katika magereza yake, wala hakuwa ameangusha maelfu ya mabomu na kuharibu miji ya Syria, na picha za maelfu ya watu waliouawa chini ya mateso hazikuwa zimevuja kutoka kwa mtu mwenye uhusiano na serikali kwa jina la "Kaisari", na uhalifu mwingine wa kinyama ambao ni mazimwi wa kibinadamu pekee ndio huufanya katika uadui wao kwa Mwenyezi Mungu, na Mtume wake na Waumini, na uhalifu wao ungali unaendelea.

Tunashangaa ni lipi lililobadilika lililoifanya Hamas kubadili mtazamo wake? Na tunawauliza Hamas, kama harakati ya Kiislamu, je, ipi hukmu ya Sharia kwa utawala huu wa kihalifu ulioikiuka heshima yetu, kumwaga damu zetu, kuharibu nyumba zetu na kututelekeza katika ardhi yetu?

Tunawahutubia huku tukiwa na uchungu kwa sababu sivyo tulivyofikiria kuwahusu. Je, hivi ndivyo udugu wa Kiislamu ulivyo?! Je, hii ndio haki ya Muislamu juu ya Muislamu mwengine?! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«الْمُسْلِمُ ‌أَخُو الْمُسْلِمِ، لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يُسْلِمُهُ» “Muislamu ni ndugu yake Muislamu, hamdulumu wala hamsalimishi.” Imepokewa na Al-Bukhari, na kwa mujibu wa Al-Tirmidhi kwa Silsila sahihi ya wapokezi:

«المُسْلِمُ ‌أَخُو المُسْلِمِ، لَا يَخُونُهُ وَلَا يَكْذِبُهُ وَلَا يَخْذُلُهُ» “Muislamu ni ndugu yake Muislamu, hamsaliti wala hamdanganyi, wala hambwagi.” Je, mlilolifanya sio kuwabwaga watu wa Ash-Sham?!

Hatujui nyinyi wenyewe mmechagua vipi kuweka mikono yenu mikononi mwa mhalifu Bashar, anayeendelea kumwaga damu za watu wa Ash-Sham, je hivi ndivyo Uislamu wenu unavyowajibisha kufanya?!

Ndugu wapenzi: Maadui wa Uislamu wanafanya kazi ya kumregesha dhalimu huyu katika eneo katika utekelezaji wa sera zao za jinai dhidi ya Waislamu, na nyinyi mnashiriki katika jinai hii, na hata kuonekana kana kwamba mnamuunga mkono katika jinai zake, basi mtakutana vipi na Mola wenu kwa haya?!

Enyi ndugu zetu: Kinachofaa kwa harakati inayopigania njia ya Mwenyezi Mungu ni kuwa mfuasi wa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Waislamu, na kuwakana maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw), na kinachofaa kwa harakati inayopigania njia ya Mwenyezi Mungu ni kukasirikia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pale yanapokiukwa matukufu yake, na dhalimu Bashar hakuacha tukufu moja la Mwenyezi Mungu ambalo hakulikiuka, basi kwa nini musikasirikie kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu?!

Enyi ndugu zetu: Kuuawa kwenu ni kwamba mlijiweka rehani kwa watawala vibaraka, hivyo maamuzi yenu ya kisiasa yakawa na uhusiano na Qatar na Iran, ambayo inawahadaa kwa fedha chafu za kisiasa wanazonunua nazo wao na mabwana zao mitazamo yenu. Kwa hiyo, hamuwezi kuuelezea Uislamu kwa njia ya kiaminifu, na huwakuwa na utashi wa kweli wa kuchukua mitazamo ambayo Uislamu unaamuru. Mna hakika kwamba ardhi iliyobarikiwa haitakombolewa kutoka kwa Mayahudi isipokuwa kwa msaada wa Umma wa Kiislamu na majeshi yake ili kusimamisha Khilafah na kwenda na majeshi ya Kiislamu hadi Quds, kuikomboa na kuitukuza, basi ni nini kinachokuzuieni hilo?! Je, sio utegemezi wenu kwa watawala vibaraka na pesa zao chafu za kisiasa?!

 Enyi ndugu zetu: Nchi za Ash-Sham ni moja; Bayt al-Maqdis na Aknaf Bayt al-Maqdis (viunga vyake), na adui yetu ni mmoja; umbile la Kiyahudi na kundi la watawala na vibaraka wahalifu wanaotekeleza sera za maadui wa Uislamu, na wajibu wenu ni kuwafanyia uadui wale wanaomfanyia uadui Mwenyezi Mungu, Mtume Wake (saw) na Waislamu.

Enyi ndugu zetu: Tunawapenda sana; kwa hivyo tunakuusieni kumcha Mwenyezi Mungu kwa haki yake, na mtubie kwa ikhlasi, na atakusameheni madhambi yenu, na jueni kwamba ushindi wa Mwenyezi Mungu haupatikani isipokuwa kwa kushikamana na kamba yake yenye nguvu, na kushikamana na Hukmu ya Sharia ambayo inawajibisha kujiwekeni mbali na watawala vibaraka na jinai zao dhidi ya Ummah wenu. Tunakulinganieni mutafakari maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

(وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَتَّخِذُ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَنْدَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّهِ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِلَّهِ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ * إِذْ ‌تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ * وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللَّهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُمْ بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ)

“Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana. Na laiti walio dhulumu wakajua watakapo iona adhabu kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu! Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao. Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.” [Al-Baqara 2:165-167]. Na kauli Yake:

(إِنَّ الَّذِينَ ارْتَدُّوا عَلَى أَدْبَارِهِمْ مِنْ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَى الشَّيْطَانُ سَوَّلَ لَهُمْ وَأَمْلَى لَهُمْ * ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لِلَّذِينَ كَرِهُوا مَا نَزَّلَ اللَّهُ سَنُطِيعُكُمْ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ وَاللَّهُ يَعْلَمُ إِسْرَارَهُمْ * فَكَيْفَ إِذَا تَوَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ * ذَلِكَ بِأَنَّهُمُ اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللَّهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ)

“Kwa hakika wanao rudi nyuma baada ya kwisha wabainikia uwongofu, Shetani huyo amewashawishi na amewaghuri. Hayo ni kwa sababu waliwaambia walio chukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu: Tutakut'iini katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao. Basi itakuwaje Malaika watakapo wafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao! Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyo mchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayo mridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao.” [Muhammad 47:25-28].

Kwa kumalizia: Hotuba yetu inaweza kuwa na ukali fulani kwenu, lakini sio ukali kama maumivu muliyojaza vifuani mwetu na nyoyo za watoto wa Ummah wenu, hususan watu wa Syria, pindi tulipowaona mukipeana mikono na dhalimu Bashar na akitabasamu usoni mwake. Tumekuambieni kwa yale ambayo Uislamu unawaamrisheni, na kwa aya za Mwenyezi Mungu na hikima zilizokuja ndani ya Qur'an Tukufu, tukimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azifungue nyoyo zenu kwenye toba na mregee kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ili muubebe Uislamu kwa uzito na uaminifu, na mutakuwa katika kambi ya Uislamu na Waislamu kukabiliana na maadui wa Uislamu na vibaraka wao kutoka kwa watawala wa madhalimu. Mtegemeeni Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Ambaye Mkononi Mwake umo ushindi peke yake.

Sababu za ushindi haziko mikononi mwa Qatar, Iran, au dhalimu Bashar. Bali, ni kutokana na kutabanni njia za ushindi na kuwakataa wao na uhalifu wao, na kuwashutumu na kufanya kazi ya kuwabadilisha na kuondoa machukizo yao. Basi, muaminini Mwenyezi Mungu naye atakuaminini, na msipofanya hivyo basi toeni ruhusa ya ghadhabu na vita kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu msivyoweza kukabiliana nazo.

Ewe Mwenyezi Mungu, wafanyie wepesi ndugu zetu njia za uongofu na vifungue vifua vyao kwa utiifu wako na nusra ya dini yako, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu