Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  30 Dhu al-Hijjah 1439 Na: 1439/033
M.  Jumatatu, 10 Septemba 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Jinamizi la “Harusi ya Demokrasia”

 (Imetafsiriwa)

George W. Bush alidai kuwa serikali ya Saddam Hussein ilimiliki silaha za maangamivu makubwa, hivyo basi kuwa tishio kwa amani ya ulimwengu. Hiki kilikuwa ni kisingizio chake cha kuiangamiza Iraq na kuikalia mnamo 2003 katika “Oparesheni Uhuru wa Iraq”. Licha ya ripoti kadhaa kutoka kwa timu za wachunguzi, na Baraza la Usalama la UM kukataa kutoa ruhusa ya kushambuliwa Iraq, lakini, Amerika, kwa kiu yake iliyopitiliza ya kutaka kuudhibiti ulimwengu kupitia sera katili ya kikauboi ya kukoloni watu na mataifa, haikutilia maanani “umuhimu wa kanuni ya kimataifa”, wala upinzani jumla wa kiulimwengu uliolipuka dhidi ya mpango wake wa kuishambulia Iraq. Pindi majeshi ya Amerika yalipofeli”, baada ya kuivamia, kupata hizo silaha zilizodaiwa kuwa “silaha za maangamivu makubwa”, George Bush alidai kuwa “ulimwengu uko salama zaidi kwa kukosekana Saddam Hussein”, na kwamba Amerika itaifanya Iraq kuwa mfano wa bustani la demokrasia na ufanisi. Haya ndiyo maumbile ya kila mvamizi muovu. Hutoa ahadi nzuri za urongo za ufanisi na hali nzuri za watu waliokaliwa, huku silaha zake zikitona damu, na ndege zake ovu zikinyesha kwa makombora na mabomu maangamivu juu ya vichwa vya watu, huku kampuni zake zikifuja mali zao.   

Ili kufinika uhalifu huu, Amerika, kupitia mwakilishi wake, Paul Bremer, ililazimisha katiba mbovu, ambayo ilidai ingeasisi Iraq ya kidemokrasia. Ili kutekeleza ajenda yake, Amerika ilitumia wanasiasa wachache wenye njaa ya utawala wanaoshindana wao kwa wao kuthibitisha utiifu wao kwa mvamizi Amerika, ambaye badali yake, huwapa makombo kutokana na “keki ya utawala” ili kushindana kwa ajili yake pamoja na magengi yao na vibaraka wao. Watu waliodhulumiwa, wakati huo huo, humalizwa kwa moto wa mivutano ya kindani, na kuathirika na hali mbaya za kimaisha kwa kukosekana viwango vya chini vya maisha bora, katika nchi ambayo imebarikiwa na rasilimali nyingi za kiuchumi na utajiri, iwe ni katika mafuta, kilimo au maji. Licha ya yote haya, baada ya ahadi ya urongo ya kila serikali kupotea, watu walisinywa na kukataa kushiriki katika uchaguzi wa ubunge mwezi Mei iliyopita (ripoti zilizo nakiliwa kwamba kiwango cha ushiriki hakikuzidi asilimia 19% ya wapiga kura), mijini na mashambani kuliripuka kwa hasira ya kutaka maisha bora na kuliondoa tabaka la wanasiasa fisadi.

Miaka kumi na tano baada ya “harusi ya kidemokrasia” ya Amerika (ambayo serikali ya Iran ilishiriki katika kuilazimisha), ile iliyoitwa demokrasia haikufaulu katika kuwadanganya watu. Waligundua ufisadi wa tabaka la wanasiasa ulioingia Baghdad kupitia vifaru vya Amerika, na kugundua kuwa “mchezo wa kidemokrasia” si chengine isipokuwa ni mangati. Katika wakati ambapo watu wanakosa maji, umeme na fursa za kazi, vyama vya kisiasa vinang’ang’ania utawala na vimefeli, miezi minne baada ya uchaguzi, kukutana na kumchagua raisi wa bunge, hivyo basi kuvuruga mchakato wa kisiasa wa kuunda serikali nyengine ya kijambazi.

Enyi watu wa ardhi ya Iraq:

Mumeuona ufisadi wa serikali iliyooza iliyo lazimishwa na Amerika, kwa ushirika wa Iran, na mumeona wazi wazi jinamizi la ile inayoitwa demokrasia, na uhadaifu wa tabaka la wanasiasa dhidi yenu. Tunawaalika kutawaliwa kwa sheria ya Mola wenu, na kukata ushawishi wa Amerika na mikono yake yote nchini Iraq, na kuikomboa Iraq kutokana na uovu wake na uovu wa vibaraka wake. Izza yenu na hadhi yenu iko pekee kupitia kuishi kwa kumtii Mola wenu, aliye wakirimu kwa Dini hii tukufu na kuwafanya Ummah bora ulioletwa kwa wanadamu.

  أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُون وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴿

“Je, wao wanataka hukmu za kijahiliya? Na ni nani mbora zaidi katika kuhukumu kuliko Allah kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma’ida: 50]

Dkt. Osman Bakhach

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu