Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  20 Muharram 1440 Na: 1440/002
M.  Jumapili, 30 Septemba 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Shahada ya Ndugu Annayev Bekentesh Khaidirovitch Kupitia Mikono ya Vibaraka wa Serikali ya Turkmenistan
(Imetafsiriwa)

Vita dhidi ya Uislamu na Waislamu havikufungika pekee kwa dola za kikoloni za Magharibi na Mashariki. Hakuna haja ya kutaja yale ambayo serikali za Amerika, Uingereza na Ufaransa zinayafanya katika vita vyao dhidi ya Uislamu na Waislamu. Urusi inashindana nao, waziri wake wa kigeni, Lavrov, alijigamba katika hotuba yake ya hivi majuzi ya UN mnamo 28/9/2018 kuwa Urusi imefaulu katika kuzuia kusimamishwa kwa Khilafah nchini Syria, ambayo aliisifu kuwa “mandhari hatari” (tafsiri ya gazeti la ‘Russia Today’ ya hotuba yake), lakini watawala wa Waislamu wanafanya kila wawezalo kuthibitisha utiifu wao kwa mabwana zao jijini Moscow na Magharibi, dhihirisho la hivi karibuni ni msako wa kikatili wa serikali ya Turkmenistan dhidi ya walinganizi wa Da’wah, watoto wema wa Uislamu wanaojitolea maisha yao kwa ajili ya Dini yao.

Mnamo 28/9/2018 mtandao wa habari wa Asia ya Kati ulichapisha kipande cha habari kwa anwani: “Serikali ya Turkmenistan Yawakandamiza Waislamu Wanaolingania Utekelezaji wa Sheria ya Kiislamu!”; mnamo 17/8/2018 vibaraka wa huduma za kijasusi za serikali hiyo walimteka nyara kijana wa Kiislamu, mchaMungu na mwema Annayev Bekentesh Khaidirovitch, ambaye alikuwa na umri wa miaka 24, baada ya kuhitimu kutoka katika Chuo Kikuu cha Bashkortostan mnamo 2017, ni mtoto wa kiume wa pekee kwa wazazi wake waliokuwa wakifanya maandalizi ya harusi yake mnamo 24/9 ya mwezi huu; mwili wake ulipatikana mnamo 18/8, kichwa chake kikiwa na majeraha mabaya, mkono wake ukiwa umevunjika, na kulikuwa na ishara ya mateso katika mwili wake na kulikuwa na alama mikononi mwake za kufungwa!

Kabla ya shahidi huyu, Biidhnillah, Annayev Bekentesh Khaidirovitch, huduma za kijasusi ziliwakamata vijana wawili, Kazakov Wiba na Ata Kildi Noor Murad, wao pia wahitimu katika Chuo Kikuu cha Bashkortostan, na wabebaji Da’wah wachangamfu ya kutabikisha sheria ya Kiislamu, walipewa hukumu kali ya vifungo gerezani, miaka 5 na 18 katika gereza la umma.

Kila mmoja na ajue kwamba katu hatutasalimu amri hadi Allah aifanye Dini hii idhihiri au tufe katika njia hii, Ewe Allah kukubali kujitolea kwetu kwa ajili ya ushindi wa Dini hii katika namna ambayo inakuridhisha, Ewe Allah tumiminie subra na uturuzuku ushindi juu ya maadui zako, maadui wa Dini yako, na umimine rehma zako juu ya ndugu yetu na umkubalie pamoja na Mitume, Wakweli, Mashahidi, na hao ndio marafiki wema, na utuunganishe naye katika birika (Hawdh) la Mtume wetu (saw). 

Sisi katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunatoa rambirambi zetu kwa familia, ya shahidi huyu, Biidhnillah, Annayev Bekentesh Khaidirovitch, na kwa wapendwa wake, hususan marafiki zake, na Ummah mzima wa Kiislamu.

Ewe Allah iruzuku familia na wazazi subra, faraja na uwaruzuku kheri katika maombolezi. Ewe Allah itimize ahadi yako kwetu, Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume.

 [إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

“Hakika, Sisi kwa yakini tutawanusuru Mitume wetu na wale walio amini katika maisha haya ya dunia na Siku watakayosimama mashahidi.” [Ghafir: 51]

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu