Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  2 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 018
M.  Alhamisi, 05 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chini ya Uongozi wa Watawala Ruwaibadha wa Waarabu na Waislamu, Majeshi na Uwezo wa Kijeshi wa Ummah Yamekuwa kwa ajili ya Maonyesho Tu!
(Imetafsiriwa)

Vyombo vya habari vya kidijitali na satelaiti vinasambaza habari kila mara za mazoezi ya kijeshi ya majeshi makubwa katika miji mikuu ya nchi za Kiislamu, ambapo ujuzi wao, silaha na visasisho vinaonyeshwa. Taarifa hizi za habari huanza kwa kuonyesha jinsi gani majeshi haya hayakosi uzoefu, teknolojia au vifaa vinavyohitajika kwa nchi yoyote kuwa kubwa, kuanzia kwa askari wenye uwezo ambao wamefunzwa kwa ukali. Hakika mwanajeshi wa Pakistan, Bangladesh, Misri na Uturuki alijizolea umaarufu mkubwa kwa medali za dhahabu zinazotolewa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ya kijeshi... Taarifa hizi za habari zinahitimishwa na wataalamu wa masuala ya kijeshi na wachambuzi wa mikakati ambao baadhi yao kutokana na wingi wao wameanza hufanya kazi kama wachambuzi wa kijeshi kwenye chaneli za setilaiti, kana kwamba ni wasanii wa utayarishaji wa maigizo, au wanahabari kwa programu shirikishi. Haya yote ni bila kutaja silaha za kimkakati na makombora ya balestiki, ambayo majeshi haya yanamiliki, kutoka kwa silaha za nyuklia hadi makombora ya balestiki ya masafa ya bara hadi bara.

Katika muktadha huu, tovuti ya Kiarabu ya “Youm7” iliripoti, “Maonyesho ya Kimataifa ya Ndege na Anga ya Misri kwa mwaka 2024 yalizinduliwa, kuanzia Septemba 3-5 huko Alamein, Misri. Maonyesho hayo yanachukuliwa kuwa tukio la kipekee la kimataifa katika nyanja ya ndege na anga, barani Afrika na Mashariki ya Kati. Maonyesho hayo ya angani huanza kwa kushirikisha zaidi ya makampuni na mashirika 300 kutoka kwa watengenezaji wa ndege na tasnia ya anga kote ulimwenguni, wakiwakilisha zaidi ya nchi 100, pamoja na Saudi Arabia. Kipindi kinaonyesha wakati wa hafla mifano tofauti ya ndege za kiraia, za kijeshi na zinazoongozwa. Kamera katika Maonyesho ya Ndege na Anga huko Alamein zilifuatilia uwepo wa gari jipya la kivita la Misri, ambalo lilikuwa limeandikwa “Proudly Made in Egypt.” Ndege za Saudi kutoka mfululizo wa F-15, ndege ya Eurofighter Typhoon, na mfumo wa ulinzi wa kituo kwa kutumia akili bandia na droni zilionyeshwa. Hii ni pamoja na onyesho la uwezo wa hali ya juu katika uwanja wa kubuni, maendeleo, uzalishaji, usaidizi wa kiufundi, matengenezo na sehemu za utengenezaji wa ndege F15 -SA. Waliohudhuria walishuhudia maonyesho kadhaa ya kitaalamu kando ya shughuli za maonyesho, ikiwa ni pamoja na onyesho la anga la pekee la ndege ya Saudia, Eurofighter Typhoon, kupitia onyesho la miondoko kadhaa yenye sifa ya ustadi na usahihi.”

Pamoja na hayo yote, umbile la Kiyahudi limekuwa salama kutokana na uwezo na silaha zote hizi za kijeshi zinazoonyeshwa ndani ya umbali wa pua na mdomo wa Gaza, ambapo dola ya Kiyahudi inawafanyia ukatili watu wake. Hii ni wakati ingekuwa inatosha kuzuia umbile la Kiyahudi kwa kufungua maonyesho kama hayo na kuendesha mafunzo kama haya huko Sinai, kwa mfano, na kutishia kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya umbile la Kiyahudi. Hili pamoja na ukweli kwamba kuliondoa  umbile la Kiyahudi kungetosha kwa jeshi, au hata sehemu ya jeshi, kutoka kwa majeshi yaliyowekwa katika kambi zao katika nchi za Kiarabu na Kiislamu, iwe karibu na mipaka ya umbile hilo ovu, au mbali nalo. Hata hivyo, ikiwa tunajua sababu ya Mayahudi kutoogopa vyombo hivi, ajabu na mshangao umetoweka. Sababu ni usaliti wa watawala wa Waarabu na Waislamu, na uoga na ufisadi wa makamanda wa majeshi hayo. Hili huwezesha umbile la Kiyahudi kuendelea katika uasi wake. Haimkiniki kwamba umbile la Kiyahudi litasimama mpaka liwaondoe kabisa watu wa Gaza, libomoe Al-Masjid Al-Aqsa, na kujenga hekalu lake linalodaiwa.

Enyi Wanyofu katika Majeshi ya Ummah kwa Jumla, na Majeshi ya Nchi zinazoizunguka Palestina, Wenye uwezo zaidi ni Majeshi ya Misri, Jordan, Uturuki na Pakistan! Kwa hakika mnafahamu kwamba uwezo wa majeshi yenu ni zaidi ya kutosha kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na utakatifu wake, na kulipizia kisasi wajane na waliofiwa, dhidi ya Mayahudi na wale wanaowaunga mkono na kuwafuata. Mnajua kwamba kikwazo pekee kilicho katika njia ya kufikia hili ni watawala wenu wa Ruwaibidha (mabwege duni) na uongozi wenu wa kijeshi unaoshirikiana nao. Mnajua kuwa muna uwezo wa kuwaondoa wasaliti hawa katika uongozi wa kijeshi na kisiasa. Kwa hivyo fahamuni kwamba matamanio ya umbile la Kiyahudi na Marekani bwana wake hayatakoma kwa kikomo au faida yoyote. Mtakuwa mumeliwa siku ile “fahali mweupe” alipoliwa, huku mukitazama tu. Je, mnangoja hadi Mayahudi watawale, na umbile lao lienee kati ya Mto Nile na Furat, na wafikie kile wanachokiota na kueneza matamanio yao kwenye runinga, bila uoga au aibu?! Ni lazima murekebishe hali hiyo kabla ya Mwenyezi Mungu (swt) kuwabadilisheni, na muongozwe pamoja na uongozi wenu wa kisiasa na kijeshi ndani ya kina cha Jahannam, baada ya kulaaniwa na Malaika na watu wote. Muna Hizb ut Tahrir, yenye uwezo zaidi, ujuzi zaidi, na yenye fiqhi (sheria) na uongozi wa kisiasa na kijeshi ulioendelea zaidi katika Umma wa Kiislamu. Mkiipatia Nusrah yenu, mtaisimamisha dola yenu, Dola ya Khilafah kwa Njia ya Utume, na mtaziepusha nafsi zenu na moto wa Jahannam, na laana ya watu na Malaika.

[يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا * وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا * رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا]

“Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungeli mt'ii Mwenyezi Mungu, na tungeli mt'ii Mtume! (66) Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia. (67) Mola wetu Mlezi! Wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa. (68)” [Surah Al-Ahzab 66-68]

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu