Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  20 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 029
M.  Jumatatu, 23 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Nchini Urusi, Wanawake wa Kiislamu Waliojistiri Wanakamatwa na Kufanyiwa Ukatili!
(Imetafsiriwa)

Mnamo Septemba 18, 2024, vyombo vya habari vya Urusi viliripoti uvamizi na ukamataji huko Tatarstan unaohusisha kina dada wanne Waislamu wanaotuhumiwa kuwa wa Hizb ut Tahrir. Wanakabiliwa na vifungo vya jela kwa zaidi ya miaka kumi chini ya Kifungu cha 205/5 cha sheria ya Shirikisho la Urusi. Kina dada hao, Leysan Sadykova (Лейсан Садыкова), Aliya Vaisova (Алия Ваисова), Alsina Khairullina (Альсина Хайруллина), na Albina Vali Akhmetova (Альбина Валиахметова), waliletwa kwa njia ya kuhujumiwa hadi Mahakama ya Vakhitovsky huko Kazan, kana kwamba walikuwa ni wahalifu hatari, mikono yao ikiwa imefungwa pingu na chini ya ulinzi wa vikosi maalum vya usalama vya Urusi.

Vyombo vya usalama vilipuuza ombi la upande wa utetezi la kuzuiliwa nyumbani, vikitaja kuwa wanawake hao ni mama wa watoto wadogo na sababu zingine muhimu. Hata hivyo, vyombo vya usalama vilisisitiza kuwaweka kizuizini na kuwafunga kutokana na madai yao ya ugawanyaaji na usambazaji wa fikra zinazotokana na itikadi ya mfumo wa kimataifa wa Khilafah tangu Machi 2019-miaka mitano iliyopita. Vyombo vya usalama vilifahamu shughuli zao tangu wakati huo, lakini havikuwakamata hadi sasa.

Hii inaashiria kwamba kukamatwa kwao, kwa mujibu wa sheria hii, kunamaanisha kuwa hawana tishio lolote kwa jamii, na si kutokana na shughuli zao katika shirika linaloitwa la “kigaidi”. Badala yake, ni kwa sababu Urusi inatawaliwa na fikra sawa na zama za KGB wakati wa Usovieti, ambapo dhamira yao ilikuwa kuwatia hofu Waislamu hasa, na jamii kwa jumla.

Vyombo vya usalama sio tu vimewatenganisha watoto na wazazi wao kwa kuwafunga kwa muda mrefu chini ya shtaka la kuwa katika Hizb ut Tahrir - kama ilivyokuwa kwa Emir Vali Akhmetov, ambaye amefungwa tangu 2016 na ni baba wa watoto wawili - lakini sasa wamemkamata mkewe, Albina Vali Akhmetova, akiwaacha watoto wao wawili bila wazazi. Hii inafanywa ili kuwatia hofu Waislamu na jamii kwa jumla.

Watawala wa nchi za Waislamu na mashirika yanayodumisha uhusiano na Urusi lazima waishinikize Urusi iwaachilie wanawake hao wa Kiislamu wasio na hatia, wasafi au kukata mafungamano yao nayo. Ikiwa mahusiano yao na Urusi ni muhimu zaidi kuliko machozi ya wanawake hawa na watoto wao, basi tunamuomba Mwenyezi Mungu awadhalilishe madhalimu hawa na washirika wao duniani na Akhera kwa uhalifu huu wa kinyama.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ]

“Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa” [Al-Buruj:8].

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu