Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 443
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Vita vya baada ya 9/11 vya Marekani vimesababisha vifo vya zaidi ya milioni 4.5, kwa mujibu wa ripoti kuu mpya kutoka kwa Mradi wa Gharama za Vita katika Chuo Kikuu cha Brown. Takriban vifo milioni 1 kati ya hivyo vilitokana na mapigano ya moja kwa moja katika maeneo ya vita kote Afghanistan, Pakistan, Iraq, Libya, Syria, Somalia, na Yemen, huku milioni 3.5 vilivyobaki ni "vifo visivyo vya moja kwa moja" vilivyotokana na mizozo ya "kuharibiwa kwa uchumi, huduma za umma, na mazingira,” kulingana na ripoti hiyo.
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan alikamatwa kwa kasi na maafisa wa kutuliza ghasia alipokuwa mahakamani kujibu mashtaka ya ufisadi na uchochezi. Wafuasi wa Khan waliingia mabarabarani, wakiteketeza magari, kushambulia kambi za jeshi pamoja na nyumba za baadhi ya makamanda.
Mnamo Jumanne na Jumatano, Mei 9 na 10, 2023, Baghdad ilikuwa mwenyeji wa kongamano lake la kwanza wa kimataifa kuhusu udhibiti wa dawa za kulevya, katika uwepo wa wawakilishi wa nchi nane: Saudi Arabia, Misri, Lebanon, Jordan, Kuwait, Syria, Iran, Uturuki na mabaraza na afisi za Kiarabu na kimataifa. Kama kawaida, mkutano haukutoa suluhisho lolote kwa sababu walitafuta mbali na sababu za jambo hili na kuenea kwake kwa njia ya kutisha.
Risala zilizotolewa na kundi la wabebaji Da’wah zilizoelekezwa kwa Hay’at Tahrir Ash-Sham (HTS) baada ya kuvamia nyumba za wabebaji Dawah na kuwakamata mashababu kadhaa wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria kwa njia ya kishenzi, ukiukaji utukufu, katika mandhari ya kutisha iliyo mbali na maadili ya Uislamu na Waislamu.
Mnamo tarehe 6 Mei 2023, BBC iliripoti kuwa mamia ya wanawake wamegoma kula katika gereza moja la Iraq katika mji mkuu wa Baghdad. Wanapinga kuzuiliwa kwao kwa kuwa sehemu ya kundi la Dola ya Kiislamu, baada ya kile wanachosema kuwa ni kesi zisizo za haki. Kundi hilo linasemekana kujumuisha raia wa kigeni kutoka Urusi, Uturuki, Azerbaijan, Ukraine, Syria, Ufaransa, Ujerumani na Marekani. "Inafikiriwa kuwa takriban watoto 100 pia wanazuiliwa katika kituo hicho".
Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.
Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.
Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.
Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.
Balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Zalmay Khalilzad alinukuu tweet, "Pengine maafa yanaweza kuepukwa, lakini ikiwa tu mambo 2 yatatokea. Mkuu wa Jeshi Munir anahitaji kujiuzulu, na uchaguzi lazima kutangazwa kwa tarehe maalum. Bila ya la kwanza, la pili haliwezekani. Bila hatua hizi mzozo wa kiuchumi, kisiasa na usalama wa Pakistan utazidi kuwa mbaya.” (The Tweet)
Kwa mujibu wa amri ya Rais wa Uzbekistan, uchaguzi wa mapema wa rais ulipangwa kufanyika Julai 9, 2023. Amri hiyo inasema: “Kulingana na Ibara ya 110 na 128 ya Katiba ya Jamhuri ya Uzbekistan na Kifungu cha 66 cha Kanuni za Uchaguzi za Jamhuri ya Uzbekistan, uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Uzbekistan umepangwa kufanyika Julai 9, 2023.”