Alhamisi, 13 Ramadan 1446 | 2025/03/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Amerika

H.  7 Ramadan 1446 Na: 09 / 1446 H
M.  Ijumaa, 07 Machi 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Amerika Yala Sanamu Lake Yenyewe!

(Imetafsiriwa)

Katika Arabuni ya kabla ya Uislamu, baadhi ya Waarabu walikuwa wakitengeneza masanamu yao kutokana na tende; walipohisi njaa, wangekula miungu yao! Leo, historia inajirudia yenyewe, lakini kwa umbo gumu zaidi. Mfumo wa Kimagharibi ambao hapo awali uliinyanyua fahamu ya uhuru hadi kwenye hadhi takatifu—uhuru wa fikra, dhamiri, na dini; uhuru wa kuzungumza na kujieleza; uhuru wa kukongamana kwa amani; ushiriki wa kisiasa; ulinzi wa haki za walio wachache; na kukataza utesaji na kutendewa kikatili – sasa unasaliti maadili haya haya yanapokinzana na maslahi ya mabepari na kipote cha watawala.

Katika baadhi ya maeneo ya Ulaya, wanawake wa Kiislamu wamekatazwa kuvaa hijabu shuleni, sehemu za kazi, na baadhi ya maeneo ya umma, licha ya ukweli kwamba, kwa mujibu wa falsafa yao ya kiliberali, huu unapaswa kuzingatiwa kuwa ni uhuru binafsi! Lakini inaonekana kwamba "uhuru" huu unaruhusiwa tu wakati unatumikia ajenda kuu ya kithaqafa na kisiasa.

Leo, tunashuhudia ukinzani mwingine mkubwa nchini Marekani. Wanafunzi wa chuo kikuu walipotoa maoni yao kuhusu chuo kikuu, wakilaani uungaji mkono wake usio na masharti wa mauaji ya halaiki na kuhamishwa kwa watu wa Gaza—kifungu cha sheria kinacholindwa na Katiba ya Marekani—utawala wa Trump, ukiungwa mkono na kipote cha kifedha na kisiasa, uliwatia hatiani wanafunzi hao kuwa wahalifu, ukitishia kuwafukuza kutoka vyuo vikuu, na hata kuwafukuza nchini wanafunzi wa kigeni miongoni mwao!

Matukio ya Gaza yamefichua unafiki wa madai ya nchi za Magharibi ya kudumisha uhuru. Yamethibitisha kwamba uhuru katika mfumo wa kirasilimali si chochote zaidi ya chombo kinachotumiwa ilimradi tu kuwatumikia kipote cha watawala. Lakini unapopingana na maslahi yao, unakanyagwa bila kusita.

Je, sio wakati sasa kwa ulimwengu kuuzingatia tena Uislamu? Tofauti na kauli mbiu tupu, Uislamu hauchukulii uhuru kama neno lisilo na maana bali ni mfumo jumuishi unaomkomboa mwanadamu kutoka katika utumwa wa wanadamu wengine na kuweka haki zinazoegemezwa juu ya uadilifu badala ya maslahi binafsi. Mwanamke mmoja wakati fulani alimsahihisha Umar ibn al-Khattab alipokuwa akiwahutubia watu, na hakumkashifu au kumnyamazisha, ingawa alikuwa Kamanda “Amir” Khalifa.

Badala yake, alikiri kwa unyenyekevu, "Umar amekosea, na mwanamke yuko sahihi." Katika mfano mwingine alitangaza: "Tangu lini mmewafanya watu kuwa watumwa, ilhali mama zao wamewazaa wakiwa huru?"

Uislamu ulitoa haki na majukumu kwa wanadamu kama wanadamu – bila ubaguzi kati ya wanaume na wanawake, au kati ya rangi na makabila. Uislamu kamwe haujakuwahi kulazimisha imani kwa nguvu; Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ] “Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu.” [Al-Baqarah: 256].

Badala yake, Uislamu umeifanya iman kuwa ni uamuzi unaotokana na msingi wa akili na tafakuri: Mwenyezi Mungu asema:

[إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَاخْتِلاَفِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللهُ مِنَ السَّمَاء مِن مَّاء فَأَحْيَا بِهِ الأرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَآبَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخِّرِ بَيْنَ السَّمَاء وَالأَرْضِ لآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ]

Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia.” [Al-Baqarah: 164]

Uislamu ulianzisha utekelezaji wa sheria kwa kuzingatia uchamungu badala ya matamanio ya kibinafsi. Ukafanya kuwa wajib kwa wenye nguvu kuwajali wanyonge; Mtume Muhammad (saw) amesema:

«أَلَا كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» Jueni kila mmoja wenu ni mchungaji, na kila mmoja wenu ataulizwa juu ya aliowachunga.”

Uislamu uliwajibisha watu kusimama kwa ajili ya uadilifu hata pale inapokwenda kinyume na maslahi yao binafsi au ya pamoja, kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاء لِلّهِ وَلَوْ عَلَى أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالأَقْرَبِينَ]

Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu.” [An-Nisa: 135].

Hivyo basi, mujtamaa wa Kiislamu ukawa kielelezo kwa jamii inayotawaliwa na huruma na uadilifu.

Enyi Waislamu zingatieni tena imani yenu—sio kama urithi wa kithaqafa bali kama mfumo mpana unaojenga upya mujamaa juu ya msingi wa “Sharia” sheria ya kiwahyi.

Tunatoa wito kwa umma wa Marekani, wasomi, na watafutao ukweli wote kuvuka upotoshaji wa vyombo vya habari kuhusu Uislamu, ili kuuchunguza Uislamu kwa akili iliyo wazi, isiyo na upendeleo wa kifikra. Pengine, kwa kufanya hivyo, mutapata katika Uislamu njia badali adilifu inayoweza kuokoa ulimwengu kutoka katika utawala wa maslahi finyo ya kibinafsi ambayo yanakanyaga maadili kila yanapokoma kuwa na manufaa.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Amerika

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Amerika
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu