Afisi ya Habari
Amerika
H. 1 Rajab 1446 | Na: 03 / 1446 H |
M. Jumatano, 01 Januari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hakuna Tofauti Kati ya Uhalifu wa huko New Orleans na Ukatili Unaofanywa na Umbile la Kizayuni huko Gaza
(Imetafsiriwa)
FBI imefichua utambulisho wa mhusika wa shambulizi la kugonga na gari huko New Orleans, Marekani, ambalo lilisababisha vifo na majeruhi ya makumi ya watu wakati wa sherehe za mwaka mpya. Mshambuliaji huyo alitambuliwa kama askari wa zamani wa Wanamaji. Mamlaka mjini New Orleans ziliripoti vifo vya watu 10 na wengine 30 kujeruhiwa baada ya lori kuingia kwenye umati wa watu. Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba watu kadhaa walipoteza maisha baada ya gari hilo kugonga mkusanyiko wa watu kwenye Barabara ya Bourbon katika Mtaa wa Wafaransa wa New Orleans mnamo siku ya Jumatano. Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya “Israel” ilisema kwamba “Waisraeli” wawili walijeruhiwa katika tukio hilo.
Wakati huo huo ambapo dola ya Kizayuni inawalipua kwa mabomu watu wasio na hatia mjini Gaza kwa kutumia silaha za Marekani na Ulaya, mhalifu huyo mwenye matatizo ya kiakili alitenda jinai yake huko New Orleans. Wakati ulimwengu umekaa kimya kuhusu jinai za umbile la Kizayuni—jinai ambazo zimedumu kwa zaidi ya miezi 15 mfululizo na kutajwa kwa uwongo kuwa ni vitendo vya “kujilinda”—ulimwengu unaoitwa “ulio huru” unalaani uhalifu wa mwanajeshi aliyechanganyikiwa aliyefanya shambulizi hilo la kugong kwa gari, ukimtaja kuwa gaidi. Ikiwa huu sio unafiki, basi ni nini?
Uislamu unaharamisha mauaji ya watu wasio na hatia, huku hadhara ya Kimagharibi na umbile la Kizayuni zikiruhusu. Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Quran:
[مِنْ أَجْلِ ذَلِكَ كَتَبْنَا عَلَى بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا]
“Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.” [5:32]
Historia haina rekodi ya Waislamu kuwahi kumwaga damu za watu wasio na hatia, bila kujali dini au makabila yao. Badala yake, historia inashuhudia ukweli kwamba Waislamu daima wamelinda maisha na heshima ya wengine, hata wakati wa vita. Maagizo yaliyotolewa na Abu Bakr (ra) kwa majeshi yake yalijumuisha yafuatayo:
«لاَ تَقْتُلَنَّ امْرَأَةً وَلاَ صَبِيًّا وَلاَ كَبِيرًا هَرِمًا وَلاَ تَقْطَعَنَّ شَجَرًا مُثْمِرًا وَلاَ تُخَرِّبَنَّ عَامِرًا وَلاَ تَعْقِرَنَّ شَاةً وَلاَ بَعِيرًا إِلاَّ لِمَأْكُلَةٍ وَلاَ تَحْرِقَنَّ نَحْلاً وَلاَ تُفَرِّقَنَّهُ وَلاَ تَغْلُلْ وَلاَ تَجْبُنْ»
“Msiue wanawake au watoto au wazee, wagonjwa. Msikate miti yenye matunda. Msiharibu mahali pa kuishi. Msichinjie kondoo au ngamia isipokuwa kwa chakula. Msiunguze nyuki na wala msiwatawanye. Msiibe ngawira, wala msiwe waoga.”
Haya ni maadili matukufu ya Waislamu hata wakati wa mapigano—basi tafakarini tabia zao wakati wa amani!
Kinyume chake wapiganaji wa Kimagharibi wakiwemo majeshi ya umbile la Kizayuni wamefanya ukatili usio na idadi. Wameua, wameweka njaa, na kutesa raia wa marika yote—watoto, wanawake, na wazee. Tunashuhudia haya leo huko Gaza, kama tulivyo shuhudia nchini Afghanistan, Iraq na Syria. Kwa hivyo, haishangazi kwa askari wa Amerika, aliyezama katika utamaduni huu wa uhalifu, kufanya vitendo kama hivyo. Vile vile si jambo la kushangaza kwa wahalifu wa umbile la Kizayuni kutekeleza mauaji ya kimbari ya kikabila, kwani umbile lao zima limejengwa juu ya mfumo kinyama na wa ubaguzi wa rangi.
Utamaduni wa mauaji na unyanyasaji wa kikatili unaofanywa na umbile la Kizayuni katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina—sambamba na uungaji mkono usio na masharti linaoupata kutoka nchi za Magharibi—unaenda sambamba na utamaduni wa kuwaunga mkono madhalimu katika ardhi za Kiislamu na kuua watu wasio na hatia nchini Afghanistan, Iraq na Syria kwa kutumia silaha za Magharibi. Hii pia inajumuisha kuundwa kwa vikundi vya mamluki kama vile “Blackwater” na “Wagner,” ambavyo ni bidhaa za mashirika ya kijasusi ya Magharibi na havina uhusiano wowote na Uislamu au Waislamu. Vikundi hivi viliibuka tu baada ya uvamizi wa kisasa wa Vita vya Msalaba katika ulimwengu wa Kiislamu. Uhusiano wa Urusi na makundi ya kigaidi yaliyofanya jinai nchini Syria pia umethibitishwa, huku Uislamu na Waislamu wakisalia kuwa hawana hatia na vitendo vyote kama hivyo.
Vitendo vya mwanajeshi huyu ni vya kulaumiwa na kulaaniwa, kama vile jinai za umbile la Kizayuni, linaloungwa mkono na nchi za Magharibi na Marekani, ni za kutisha zaidi na zinazostahili kulaaniwa. Waislamu, pamoja na watu wengine wa dunia, wanapaswa kusimama dhidi ya watawala na taasisi zinazoendeleza jinai kama hizo. Ni lazima wakatae hadhara ya Kimagharibi, ambayo imejengwa juu ya umwagaji damu, na badala yake wapendekeze hadhara tukufu ya Uislamu kama badali bora kwa ajili ya wanadamu. Uislamu ni dini ya amani, usalama na utulivu. Zaidi ya karne 13 za utawala wa Kiislamu katika sehemu kubwa za dunia, idadi ya vifo vinavyosababishwa na utawala wa Kiislamu si sehemu hata ya maisha yaliyopotea katika vita vimoja vya Magharibi-iwe ni wakati wa Vita vya Kwanza au vya Pili vya Dunia.
Hebu sote na tuukumbatie Uislamu kama suluhisho na tuipe mgongo hadhara ambayo haijaleta chochote isipokuwa mateso na taabu kwa wanadamu.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa..” [8:24].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Amerika
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Amerika |
Address & Website Tel: |