Jumatatu, 28 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Amerika

H.  6 Rabi' I 1447 Na: 03 / 1447 H
M.  Ijumaa, 29 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ulaghai wa Suluhisho la Dola Mbili kwa Palestina

«لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ»

Muumini hang’atwi kutoka kwenye tundu moja mara mbili.” [Bukhari]

(Imetafsiriwa)

Wito kwa Umma wa Kiislamu

Msiba unaoendelea mjini Gaza, na kwa hakika katika Ardhi yote iliyobarikiwa ya Palestina, unasimama kama kioo kinachoakisi utu, heshima, na kujitolea kwa Umma. Pia unaakisi majeraha makubwa yaliyotokana na kupotea kwa ngao yetu—Khilafah.

Ni kioo kinachofichua unafiki shupavu na undumakuwili wa dola za kikoloni, ambazo uadui wao wa kina dhidi ya Uislamu unawekwa wazi. Sheria na taasisi za kimataifa zimeonyesha umbile lao halisi: ugumba, kutokuwa na umuhimu, na utumwa kwa ajenda za dola hizi.

Gaza pia imefichua, kwa uwazi wa uchungu, usaliti wa watawala katika ulimwengu wa Kiislamu. Badala ya kuilinda Palestina, wamejifungamanisha na mabwana zao wa kikoloni—kuzuia majeshi ya Waislamu, kunyamazisha matakwa ya umma ya kufungua mipaka, na hatimaye kulilinda umbile la Kizayuni huku likiendelea na kampeni yake ya mauaji ya halaiki na utiaji njaa.

Hata hivyo, chini ya hali ngumu hizi zaidi, watu wa Gaza wamesimama kidete, wakikataa kushindwa. Umma mpana zaidi haujanyamaza, ukijifungamanisha na maneno ya Mtume (saw): «مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ وَتَرَاحُمِهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ مَثَلُ الْجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى» “Mfano wa Waumini katika kupendana kwao, kuoneana huruma kwao, na kuoneana upole kwao, ni kama mfano wa mwili pindi kiungo kimoja kinaposhtakia maumivu, mwili mzima huitikia kwa kukosa usingizi na homa.” [Bukhari 6011, Muslim 2586]

Mtego wa Kikoloni wa Suluhisho la Dola Mbili

Katika wakati huu muhimu, dola za kikoloni zinazohusika na kupandikiza ukaliaji wa kimabavu wa Kizayuni kwa mara nyengine tena zinaendeleza kile kinachoitwa “suluhisho” lao – uundaji wa dola ya Palestina sambamba na dola ya Kizayuni. Ufaransa, Uingereza, Australia, na nyengine hivi majuzi zimethibitisha kuunga mkono mpango huu.

Lakini hizi ni dola zile zile ambazo ziliunda, kulipa silaha, kulifadhili, na kulilinda umbile la Kizayuni tangu kuanzishwa kwake. Zinaendelea kulikinga kidiplomasia huku zikisambaza silaha na ufadhili unaowezesha uhalifu wake. Ummah unahitaji kufahamu wazi na usiingie kwenye mtego wa kutapatapa na uchovu katika kukumbatia suluhisho hilo la kikoloni ambalo linatoa tu afueni ya muda, huku umbile la Kizayuni likidumisha unyongaji wake wa ardhi iliyobarikiwa. Mtume (saw) alitukumbusha, «لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ» “Muumini hang’atwi kutoka kwenye tundu moja mara mbili.” [Bukhari 6133]

Itakuwa ni ujinga wa hatari kuamini kwamba wito wao wa suluhisho la dola mbili umetokana na kujali mateso ya Wapalestina. Nia zao ni za kisiasa tu – kutafuta kutuliza hasira ya umma inayokua juu ya kushiriki kwao katika uhalifu wa kivita, huku wakihifadhi maslahi yao ya kimkakati katika eneo hilo. Hizi ni siasa za kisekula kwa kejeli yake: uchafu, ufisadi na unyama mkubwa zaidi.

Kwa nini Suluhisho la Dola Mbili Sio Suluhisho

Mpango wa  dola mbili hauikomboi Palestina; unaimarisha ukaliaji wa kimabavu. Unahalalisha dola ya Kizayuni, kulinda uwepo wake huku ukiunda mamlaka isiyo na nguvu ya Palestina isiyo na ubwana wa kweli – ukiiga hali ilivyo sasa. Chini ya mpangilio kama huo, umbile la Kizayuni litadumisha udhibiti wa mipaka, rasilimali, na matembezi ya watu. Litaendelea kufurahia usaidizi wa kijeshi na kifedha kutoka kwa dola za kikoloni, huku tawala za Kiarabu zikifanya kazi kama wadhamini wa usalama wake. Zaidi ya hayo, unaziruhusu dola za kikoloni na tawala za Kiarabu fursa ya kuosha mikono yao iliyotapakaa damu.

Zaidi ya uhalisia wa siasa za kijiografia, mpango huu unatumikia madhumuni mengine hatari: uhalalishaji wa utamaduni wa kupima uhalisia na hisia ya kushindwa ndani ya Umma. Kwa kushajiisha vizazi vinavyofuatana kukubali ulegezaji msimamo na makubaliano ya kivipande, unawatia moyo maadui wa Uislamu kudai hata zaidi, kutushinda na kupotoa umakinifu kutoka kwenye njia pekee ya kweli ya ukombozi.

Mtazamo Wazi wa Kiislamu

Mwenyezi Mungu (swt) anatukumbusha kwa uwazi tusijilinganishe na wale waliotutoa katika ardhi zetu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاء تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءكُم مِّنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ]

nyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyo kujieni, wakamfukuza Mtume na nyinyi  kutoka majumbani mwenu …” [Al-Mumtahina: 1].

Ummah wetu unapoendelea kuamka, ni lazima tubaki imara na tusiogope, tusikubali kushindwa au kuchukua hatua za kujirudia za kupima uhalisia na kulegeza msimamo ambayo yanaendeleza masaibu, japokuwa huenda yakafanywa kwa nia ya dhati ya kuwapunguzia watu matatizo ya mara moja. Mwenyezi Mungu (swt) anatukumbusha:

[وَلاَ تَلْبِسُواْ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُواْ الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ]

Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua.” [Al-Baqarah: 42],

[وَلاَ تَهِنُوا وَلاَ تَحْزَنُوا وَأَنتُمُ الأَعْلَوْنَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ]

Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini.” [Aal-Imran: 139].

Suluhisho la dola mbili ni Batili. Halitoi ukombozi wala utu. Linaendeleza utiishwaji chini ya amri iliyolazimishwa na ukoloni na lazima likataliwe vikali na Umma. Wajibu wetu si tu kupinga dhulma ya umbile la Kizayuni bali ni kufanya kazi kwa ajili ya ukombozi wa kina wa Palestina. Hilo linahitaji zaidi ya maandamano au mazungumzo—linahitaji kuregeshwa kwa Khilafah kwa njia ya Utume na uhamasishaji wa majeshi ya Waislamu.

Khilafah si dhana kinadharia; ni mfumo uliothibitishwa ambao Waislamu, Wakristo, na Mayahudi waliishi chini yake kwa utulivu, haki, na amani. Ndio mfumo pekee wenye uwezo wa kukomesha ukaliaji kimabavu, kuunganisha Ummah, na kuondoa uwepo wa kikoloni kutoka kwa ardhi zetu.

Suluhisho la serikali mbili ni mtego – ulioundwa ili kuutuliza Ummah huku ukilinda uhai ya mradi wa Kiyahudi wa Kizayuni. Jibu letu lazima liwe wazi na lisiloteteleka: kukataa suluhisho hili la batili na kujitolea kwa njia pekee inayohakikisha ukombozi—kusimamisha Khilafah na kukusanya rasilimali za Ummah ili kuikomboa Palestina yote.

Historia itakumbuka iwapo tulisimama kidete kwenye haki au tulikubali kulegeza msimamo. Mwenyezi Mungu (swt) aujaalie Ummah ubainifu, umoja na ushindi.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Amerika

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Amerika
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu