Jumatatu, 28 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Amerika

H.  26 Rabi' II 1447 Na: 04 / 1447 H
M.  Jumamosi, 18 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji ya Halaiki na Unafiki - Jinsi Washington Inavyokaidi Watu Wake Wenyewe

(Imetafsiriwa)

Utawala wa sasa wa Marekani, unaoongozwa na Donald Trump, unafuata njia ya vibaraka wake miongoni mwa watawala dhalimu wa ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu - wale ambao wanapuuza viwango vya rai jumla ya umma, wanatawala kwa udikteta kamili, na kupuuza itikadi na maadili ya Umma.

Licha ya kura za maoni za hivi majuzi za Marekani kuonyesha kupungua kwa kasi kwa uungaji mkono wa umma kwa kulipatia umbile la Kizayuni silaha kwa ajili ya mauaji ya halaiki huko Gaza, na kuongezeka kwa wito wa kuzuia misaada ya kijeshi ya Marekani, Trump alijigamba katika hotuba yake kwa Knesset kuhusu matumizi ya silaha za Kimarekani. Alisema, “Tunatengeneza silaha bora zaidi duniani, na tunazo nyingi zaidi, na nyingi tumezipeana kwa ‘Israeli.’ Kusema kweli, Benjamin [Netanyahu] alikuwa akinipigia simu sana – ‘Je, unaweza kupata silaha hii, na silaha ile,’ na baadhi yazo hata sikuwa nimezisikia kabla.” Aliongeza, “Lakini tulikuwa tunazipata hapa, sawa?” Trump alisifu ufanisi wa umbile la Kizayuni katika kupeleka silaha hizi na akasema, “Israel imejifunza jinsi ya kuzitumia vizuri.” (Al Jazeera)

Moja ya viashiria vikubwa vya kutoidhinishwa na umma vilitokana na kura ya maoni ya Gallup iliyoonyesha kuwa ni asilimia 32 pekee ya Wamarekani wanaounga mkono operesheni za kijeshi za ‘Israel’ mjini Gaza, huku 60% wakipinga. Utafiti wa Kituo cha Utafiti cha Pew uligundua kuwa 33% ya watu wazima wa Marekani wanaamini Washington inatoa misaada ya kijeshi ya kupindukia kwa ‘Israel’, huku 35% wanafikiri misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina haitoshi. Vile vile, kura ya maoni ya Quinnipiac ilifichua kuwa 60% ya wapiga kura wa Marekani wanapinga kutuma msaada wa ziada wa kijeshi kwa ‘Israel’.

Matokeo haya yanasisitiza kwamba sera ya utawala haiakisi maoni ya wapiga kura wa Marekani, na kufichua tofauti kubwa kati ya sera rasmi na rai jumla ya umma. Hata ndani ya vyama vikuu vya kisiasa, uungaji mkono kwa umbile la Kizayuni unapungua. Miongoni mwa Democrats, 75% wanapinga kutuma msaada wa ziada wa kijeshi; kati ya watu huru, 66% wanashiriki maoni hayo; na hata miongoni mwa Republicans – waungaji mkono imara wa jadi – ni 56% pekee wanaopendelea usaidizi zaidi wa kijeshi.

Takwimu hizi zinaonyesha mabadiliko makubwa katika mitazamo ya Wamarekani kwa ‘Israel’ na kuongezeka kwa matakwa ya kuzuia msaada wa kijeshi wa Marekani, ikisukumwa na wasiwasi juu ya kuongezeka kwa ghasia na athari zake mbaya kwa watu wa Palestina, Ardhi Iliyobarikiwa.

Msimamo jumla wa ulimwengu wa Magharibi - unaoitwa “ulimwengu huru” - katika kuunga mkono jinai za umbile la Kizayuni mjini Gaza, kwa kulipatia silaha, fedha, na habari za kisiasa na vyombo vya habari ili kuhalalisha ukatili wake, unadhihirisha zaidi unafiki wa hadhara ya Kimagharibi. Kukusanyika kwao katika kongamano la Sharm El-Sheikh kusherehekea “ushindi” juu ya watoto, wanawake, wazee, na uharibifu wa hospitali, shule, na misikiti inafichua umbile halisi la hdhara iliyojengwa kwa karne nyingi za unyonyaji na ukandamizaji - ambayo inaendelea kuhubiri uhuru, haki za binadamu, na kujitawala huku ikiyasaliti maadili hayo kwa vitendo.

Kwa hiyo ni wajibu kwa walimwengu - hasa watu wa ulimwengu wa Kiislamu - kufanya kazi kuelekea kuubadilisha mfumo wa kibepari wa kisekula, ambao misingi yake ya kinyonyaji imeleta taabu na ufisadi kwa wanadamu, kwa mfumo wa Kiislamu unaoongozwa na wahyi. Tofauti na ubepari, ambao hubadilika na kuwa udikteta unaohudumia kipote cha watu wa juu kifedha waliojikita mizizi, Uislamu unatoa mfumo wa haki na wa kimaadili unaoakisi matakwa ya watu na kuyalinda maslahi yao ya kweli chini ya mwongozo wa Mwenyezi Mungu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Amerika

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Amerika
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu