Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  14 Rabi' I 1445 Na: 1445 H / 07
M.  Ijumaa, 29 Septemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Inatoa wito kwa Raia wenye Ufahamu na Watu wenye Ushawishi: Jiungeni na Kongamano la Mtandaoni lenye Kichwa "Njia ya Kutokea - Kutoka kwa Mshiko wa Dhalimu Hasina na Mkoloni Marekani" na Jitokezeni Kutekeleza Miongozo

(Imetafsiriwa)

Siasa na uchumi wa nchi zinapitia shida ambayo tayari imegeuka kuwa mgogoro mkubwa. Mateso ya watu yamepitiliza. Kwa sababu ya kuongezeka kwa bei ya bidhaa watu wa kawaida wanajitahidi kununua hata chakula msingi kama mayai na mkate. Katika janga la dengue, kila mtu anapita siku zake kwa uoga na hofu pamoja na familia, jamaa na watoto wao. Hakuna kipimo madhubuti cha kuua mbu, na hakuna vifaa vizuri vya matibabu. Biashara, chanzo kikuu cha chumo na riziki ya watu, inapitia mporomoko mkali, huku mabepari wachache wakiunda milima ya utajiri. Uporaji mkubwa unaendelea kwa jina la Mradi wa Mikubwa. Benki za nchi zinaporwa katika mchakato wa kuendelea, na kwa jina la malipo ya umeme, sherehe ya uporaji inaendelea katika sekta ya umeme. Uchumi wa nchi unakabiliwa na kufilisika kutokana na shinikizo la malipo ya mkopo wa riba wa kigeni na mgogoro wa akiba.

Wakati watu wa nchi wanapokuwa katika hali kama hiyo, ni kipi kincho endelea katika uwanja wa kisiasa? Kama muonavyo, maafisa wa ngazi za juu kutoka Ulaya na Marekani wanazuru Bangladesh mara kwa mara. Makundi ya Awam-BNP yameshughulishwa na kufanya mikutano na vyajio pamoja na maafisa wa nchi hizi za wakoloni. Walakini, wanadai kwamba wanafanya siasa kwa ajili ya watu. Hatuoni umakini wao hata kwa uchache katika kutatua shida yoyote ya watu, badala yake umakini wao uko katika kusalia madarakani au kupata mamlaka kupitia kuwahudumia wakoloni hawa. Kwa kutumia fursa hii, wakoloni wanaendelea na ajenda zao kufikia maslahi yao ya kiuchumi na ya siasa za kijiografia. Ingawa hutumia demokrasia, utawala wa sheria, na haki za binadamu kuficha ajenda na nia zao kinyama, lakini mnajua na mumeona jinsi walivyo angamiza nchi kama Iraq, Afghanistan na Pakistan kwa jina la maneno haya matamu.

Enyi watu, katika hatua hii muhimu ya nchi, kongamano hili limeandaliwa kwa madhumuni ya kuonyesha ulisia wa kweli wa nchi hii na kuwasilisha mwongozo wa njia ya kutoka katika uhalisia huu. Tunatoa wito kwenu kushiriki katika kongamano hili la mtandaoni lenye kichwa "Njia ya Kutokea - Kutoka kwa Mshiko wa Dhalimu Hasina na Mkoloni Marekani" litakalo peperushwa na Al Waqiyah TV na jitokezeni kutekeleza njia ya kutokea.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. [Surah Al-Anfal: 24]

Wakati na Tarehe ya Kupeperuswa Kongamano:   07:00 pm; Jumamosi, 30 Septemba, 2023

Tovuti ya Upeperushaji: ALWAQIYAH.TV - https://youtu.be/w0ztfSvVrnU

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu