Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  15 Rajab 1445 Na: 1445 H / 15
M.  Jumamosi, 27 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuingizwa kwa Ubadilishaji wa Jinsia kwa Jina la Hadithi ya Sharifa katika Kitabu cha Mafunzo ni Sehemu ya kile kinachoitwa Vita vya Kidemokrasia vya Kimsalaba vya Serikali ya Hasina dhidi ya Uislamu na Waislamu

(Imetafsiriwa)

Jana Januari 23, 2024, kupitia tukio la kufutwa kazi mwalimu mmoja wa Chuo Kikuu cha BRAC kwa kupinga kuingizwa kwa watu waliobadili jinsia (jinsia ya 3 iliyotajwa kwenye kitabu) “Hadithi ya Sharifa” katika darasa la saba kitabu cha “Historia na Sayansi ya Kijamii” cha mtaala mpya, kwa mara nyengine tena msururu wa njama za kuharibu imani na maadili ya kizazi chetu kijacho cha Umma wa Kiislamu umejitokeza. Ingawa, Waziri wa Elimu alijaribu kudanganya suala hilo kwa kulinganisha somo lenye utata la kitabu hicho na idadi ya watu wa Hijra ili kuepusha hasira za umma. Njama hii ya serikali ya kuanzisha “maadili ya kiliberali” ya mkoloni kafiri Magharibi katika ardhi hii ya Kiislamu haikufungika tu kwenye vitabu vya masomo pekee. Wakati huo huo, Wizara ya Ustawi wa Jamii, kwa msaada wa ADB (Benki ya Maendeleo ya Asia), imeandaa sheria iitwayo 'Transgender Rights Protection Act-2023', ambayo inatarajiwa kukamilika kuwa sheria ifikapo mwishoni mwa 2024. Katika barua iliyotumwa na Waziri wa Mambo ya Nje Abdul Momen kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kabla ya uchaguzi, kiapo cha serikali ya Hasina cha vita vya kidemokrasia dhidi ya imani ya Kiislamu kiko wazi. Katika barua hiyo, waziri wa mambo ya nje alimtaja Waziri Mkuu Sheikh Hasina kama 'mpigania demokrasia' (The Daily Star, Bangla, Disemba 08, 2023). Jinsi serikali ya Hasina ilivyojitolea kutekeleza vita vya kilimwengu inathibitishwa na mkutano wa mtu wa kwanza wa nchi hii aliyebadili jinsia (aliyebadilisha jinsia rasmi) na Waziri Mkuu huyo, mwakilishi mkuu wa serikali. (Transgender Ho Chi Min mkutano na Waziri Mkuu, Time News, Agosti 10, 2023).

Ubadilishaji jinsia (Transgenderism) ni sehemu ya jamii inayoitwa LGBTQ, ambayo imekuwa ikitumika tangu miaka ya tisiini kuashiria “jamii ya mashoga” ya zamani. Kwa pamoja, “LGBT” inakusudia “Wasagaji, Mashoga, Wenyejinsia Mbili na Wanaobadili jinsia”, yaani mashoga, watu wa jinsia zote mbili na waliobadili jinsia, wanatokana na kanuni za uhuru wa mtu binafsi na usawa wa kijinsia wa mfumo usiomcha Mungu wa kisekul wa Kimagharibi. Muungano wa kisekula wa BNP pia umetabanni kwa ulaghai maadili haya ya Magharibi katika falsafa yao ya kisiasa chini ya jina la “Taifa la Upinde wa Mvua”, kwa sababu “Upinde wa mvua” ni ishara ya LGBTQ. Lakini Waislamu wanajua kwamba wakati wa Nabii Lut (as) Mwenyezi Mungu (swt) aliangamiza umma wake ambao ulipuuza maonyo ya Lut (as) na kujiingiza katika ushoga. Unaona kwamba jamii ya Kimagharibi na mifumo ya kifamilia ni dhaifu na inakabiliwa na dhana na tabia hizi potofu. Kwa kweli, vibaraka wa tabaka tawala la kisekula la Awami-BNP wamejitolea kuendesha vita vya Magharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu. Hata hivyo, kundi hili tawala la wasaliti kwa njia ya ulaghai lilitumia hisia za Uislamu na Waislamu kukwea madarakani na kulazimisha usekula juu ya jamii na Serikali ikiwa madarakani.

Enyi Watu! Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنْ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَهُمْ مِنْهُمْ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمْ الْفَاسِقُونَ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu." [Surah Aali-Imran:110]. Mwalimu wa Chuo Kikuu cha BRAC Asif Mahtab ni mwana shujaa wa Ummah huu wa Kiislamu ambaye alitumia nafasi yake kufichua vita vya kimsalaba vya kidemokrasia vya serikali ya Hasina na anasifiwa kuwa shujaa na Waislamu wote. Ni ushahidi tosha kwamba Ummah huu wa Kiislamu kamwe haukubali ukafiri kwa kujua; Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «لا تزال طائفة من أمتي ظاهرين على الحق إلى أن تقوم الساعة»“Kipote katika Umma wangu hakitaacha kudhihirisha haki mpaka kitakaposimama Kiyama”. Kukabiliana na vita vya kimsalaba vya kidemokrasia vya Hasina kunahitaji kung'oa sumu ya usekula kutoka kwa jamii na serikali na kusimamisha tena mfumo wa Kiislamu wa Khilafah. Ili kufikia lengo hili, Waislamu wote wanapaswa kuungana katika mapambano ya kifikra na kisiasa chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida.

Enyi Maafisa Wanyoofu wa Majeshi! Mumeshuhudia jinsi maisha ya jamii yaani wanafunzi na walimu yalivyochukua msimamo kwa ajili ya Uislamu. Je, Mwalimu Mahtab si msukumo kwenu aliyepinga kile kilichoitwa kampeni ya kimsalaba ya kidemokrasia ya serikali ya Hasina na kutumia wadhifa wake ipasavyo? Nyinyi muna uwezo wa kijeshi ambao kupitia huo munaweza kung'oa utawala huu wa kisekula akiwemo Hasina. Kwa hiyo, sisi Hizb ut Tahrir tunakuombeni mujitokeze na kuipa Nusrah (nguvu) Hizb ut Tahrir kuiondoa serikali ya Hasina na kuregesha Khilafah. Ambayo kwayo vita vya msalaba vya Magharibi kwa usaidizi wa watawala wao vibaraka dhidi ya Uislamu vitakomeshwa milele, na Uislamu kama mshindi utawaleta wanadamu wote kwenye nuru kutoka kwenye giza la itikadi potofu iliyotungwa na mwanadamu ya usekula.

[الر كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنْ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ]

“Alif Lam Ra. (A.L.R.) Hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha kwako ili uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye muwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifiwa.” [Surah Ibrahim: 1]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu