Jumamosi, 14 Muharram 1446 | 2024/07/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  22 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 12 / 1445 H
M.  Ijumaa, 28 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hakuna Uamuzi wa Kisiasa wa Mahakama Utakaositisha Wito wa: “Israel” Lazima Iondolewe na Palestina Yote Ikombolewe

(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumanne tarehe 25/6/2024, nilihukumiwa kifungo cha nje siku 60 katika Mahakama ya Jiji la Copenhagen kwa kutoa wito wa ukombozi wa Palestina. Jaji anayeendesha kesi aliamua wakati wa kutoa hukumu kwamba hotuba yangu ya 2021 katika suala hilo haikuelekezwa kwa Mayahudi kama kundi la kidini, lakini alitoa wito wa kuondolewa kwa umbile haramu la Kizayuni linaloitwa “Israel” kupitia uingiliaji wa kijeshi. Wito huu ulitangazwa na mahakama ya jiji kuwa sio halali!

Hivyo basi hukumu hiyo inaharamisha moja kwa moja wito wa ukombozi wa Palestina, bila madai ya chuki dhidi ya Mayahudi kama pazi nyembamba inayojulikana sana, na bila hata kufafanua ni uhalifu gani niliodaiwa kuuchochea.

Ikiunganishwa na makubaliano mapya ya Bunge juu ya kupambana na “chuki dhidi ya Mayahudi”, ambayo pia inaharamisha upinzani dhidi ya umbile la kigaidi la Kizayuni liitwalo “Israel”, sehemu ya chini iliyooza inakanyagwa kutokana mfumo wa sheria nchini Denmark.

Wakati huo huo, uvamizi wa Kizayuni wa Palestina unaendelea kutekeleza mauaji ya halaiki mbele ya macho ya walimwengu, wakifadhiliwa na dola za Magharibi - na dola ndogo kama Denmark, ambazo zinachangia mauaji ya halaiki ya watoto wa Gaza kwa kutuma sehemu za silaha kwa ndege za kivita umbile hilo la kigaidi.

Kwa kuwafanya wapinzani wa uwepo kwa “Israeli” kuwa ni haramu, dola ya Denmark inayounga mkono mauaji ya halaiki inakamilisha ushiriki wake katika uhalifu wake.

Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Denmark, tunatoa wito kwa kila mtu mwenye maadili kuendeleza upinzani dhidi ya uungaji mkono wa serikali ya Denmark kwa mauaji ya halaiki. Hasa tunawalingania ndugu na dada zetu Waislamu kuendeleza wito huo kwa azma na ushupavu mkubwa zaidi na kufanya kazi kwa ajili ya kuondolewa kikamilifu uvamizi huo na ukombozi wa Palestina kupitia majeshi ya ulimwengu wa Kiislamu.

Kimya na maridhiani sio chaguo.

Elias Lamrabet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu