Alhamisi, 09 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  14 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 11 / 1445 H
M.  Alhamisi, 20 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kesi ya Kisiasa Inafichua Uungaji Mkono wa Denmark kwa Uvamizi wa Mauaji ya Halaiki

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 25 Juni, 2024, mimi, Elias Lamrabet, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir / Denmark, nitahudhuria Mahakama ya Jiji la Copenhagen. Afisi ya Mwendesha Mashtaka ya Umma inataka niadhibiwe kwa kifungo gerezani, katika hotuba iliyotolewa mbele ya Ubalozi wa Misri mnamo Mei 2021 wakati wa mauaji ya wakati huko Gaza, kuwataka Waislamu wote kutoa wito kwa majeshi ya Waislamu katika nchi zinazozunguka Palestina kuingilia kijeshi ili kuikomboa Palestina yote na kukomesha uvamizi wa Wazayuni.

Uvamizi huu wa mauaji ulikuja kwa njia ya mauaji ya kikabila, na ugaidi wa kimfumo wa watu halali wa Palestina. Palestina ilichukuliwa kwa nguvu katika dhulma ya kihistoria, na leo hii zaidi kuliko wakati mwingine wowote imedhihirika, pia kwa sehemu za wakaazi wa Kimagharibi, kwamba uvamizi wa umwagaji damu na jinai za Wazayuni zitakomeshwa tu kwa nguvu.

Wito wetu kwa majeshi ya Misri na majeshi mengine ya Waislamu katika eneo hilo ulikuwa mwaka 2021, kama ilivyo leo na umekuwa daima, kwamba ni wajibu wao - wale walio na uwezo wa kijeshi wa kivitendo - kuingilia kati na kukomesha uvamizi haramu wa kigaidi wa Kizayuni, "Israel".

Serikali ya Denmark inaendelea na uungaji mkono wake wa dhati kwa uvamizi wa Kizayuni wa Palestina na mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Gaza, ambayo yameitia hofu kila nafsi adhimu katika sayari hii, na kuwaamsha watu kuona kwamba vima vinavyodaiwa vya dola za Magharibi vimezikwa na maiti hizo za maelfu ya wanawake na watoto chini ya magofu ya Gaza. Haki za binadamu, haki ya kuishi na kujiamulia, haki za wanawake na ustawi wa mtoto - yote haya yanatupwa chini ya tingatinga la Uzayuni na wanasiasa na mamlaka, ambao kwa hivyo wanaonyesha unafiki wao wa hali ya juu na kufichua jinsi gani "vima" hivi kivitendo ni ala tu za kisiasa.

Kuhusu "uhuru wa kuzungumza" unaoimbwa sana miezi ya hivi karibuni imeonyesha kwamba Wazayuni wa Denmark, wanasiasa na vyombo vya habari wanaweza kuunga mkono kwa uhuru na bila matokeo mauaji ya halaiki, ambapo zaidi ya watoto 15,000 wa Kipalestina wameuawa katika kipindi cha chini ya miezi 9 ya miaka 76 ya uvamizi katili, na bado kiu yao ya damu isiyo na hatia haijakwisha. Wakati huo huo, kwa kufunguliwa mashtaka na vitisho vya kufungwa jela, wanajaribu kuwatisha Waislamu ili hata wasizungumze kuhusu ukombozi!

Kwa hivyo serikali ya Denmark kwa hiari inamomonyoa msingi wake wenyewe wa vima kwa madhumuni pekee ya kutoa usaidizi kwa uvamizi wa mauaji ya halaiki.

Hata hivyo, jaribio la vitisho halina matumaini. Hatia ya kusimama upande wa Palestina - upande wa watoto na wanawake, upande wa kaka na dada zetu wanaokandamizwa - daima itakuwa ni medali ya heshima kuvaa kwa fahari.

"Israel" inakabiliwa na maangamizi yake. Ni uvamizi wa kijeshi, na uvamizi wa kijeshi unamalizwa kwa ukombozi wa kijeshi. Ukweli huu angavu, ambao ndio suluhisho pekee la kweli kwa Palestina ambalo Uislamu unaamuru, mimi na Hizb ut Tahrir tutaendelea kuulingania popote pale tulipo.

Hakuna mashtaka yaliyochochewa kisiasa, hakuna tishio au kulazimishwa, yatatuzuia kusema ukweli au kutikisa azma yetu hata kidogo. Bali kinyume chake.

Elias Lamrabet

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu