Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
H. 25 Rajab 1446 | Na: 1446 / 11 |
M. Jumamosi, 25 Januari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuondolewa kwa Umbile la Kiyahudi ndio Suluhisho Pekee, Sio Suluhisho la Dola Mbili, Safadi
(Imetafsiriwa)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi, wakati wa kushiriki kwake katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos mnamo Jumatano, 22/01/2025, alisema kuwa mbinu yoyote ya baadaye ya Gaza lazima iegemee juu ya umoja wa Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi na lengo la kufikia amani tu kwa msingi wa suluhisho la dola mbili. Alisema: “Katika muktadha wa suluhisho la kisiasa, serikali ya Palestina ndiyo pekee inayoshikilia uamuzi wa amani na vita, na hakupaswi kuwe na makundi ya kisilaha nje yake.”
Katika taarifa yake ya baadaye, alisisitiza ulazima wa kusitisha kuenea kwa hatari kwa umbile la Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi, akionya “mlipuko wa hali katika eneo hilo kutokana na kuendelea kwa sera za serikali (ya Israeli) yenye misimamo mikali dhidi ya Wapalestina na ukiukaji wake unaoendelea katika maeneo ya Palestina.”
Na kwa kujibu matamshi haya ya mara kwa mara na kurudiwa kwake mara kwa mara kila Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Jordan anapokabidhiwa kipaza sauti ili azungumze—kana kwamba kifaa cha kunakili sauti kimewekwa kooni mwake pamoja na semi hizi, kiasi kwamba imewakera umma kwa ujumla pamoja na kipote cha wasomi kwa sababu ya upuuzi wake, migongano, na kujitenga na uhalisia – yanapuuzwa na kila mtu isipokuwa wale wanaofuata njia ya utawala ya utiifu na kujisalimisha kwa maadui wote wa Ummah. Kwa hivyo, tunafafanua yafuatayo:
Kinachojulikana kama suluhisho la kisiasa, yaani suluhisho la dola mbili, sio tu kwamba limeharamishwa kidini bali pia ni usaliti wa kufedhehesha na kujisalimisha—sio tu kwa umbile la Kiyahudi, bali kwa dola zote za kikoloni, huku Amerika ikiwa mstari wa mbele. Zaidi ya hayo, ni wazo potofu lisilo na uhalisia wowote wa kweli, kwani umbile la Kiyahudi linafanya kazi ya kunyakua Ukingo wa Magharibi kufuatia vita vyake vya mauaji ya halaiki huko Gaza. Wakati huo huo, Amerika inaliwezesha kufanya hivyo, na Trump, pamoja na timu yake ya misimamo mikali inayounga mkono umbile la Kiyahudi, wanapuuza waziwazi hata dhana ya kuunda dola bandia kwa Wapalestina.
Ama watu wa Umma wa Kiislamu, hususan wale walio jirani na Palestina, hivi sasa wanatazamia kwa hamu kuanguka kwa tawala za utumishi na utiifu. Haya yanajiri baada ya kushuhudia uthabiti na ushindi usio na kifani wa watu wenye fahari wa Gaza, ambao umeacha alama isiyofutika nyoyoni na akilini mwao—kuishinda mashini ya vita vya kimataifa mikononi mwa Mayahudi waoga. Imejikita katika Aqidah yao kwamba jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu na kulitokomeza umbile la Kiyahudi ndiyo suluhisho pekee la halali na la kweli kwa kadhia ya Palestina.
Madai yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan kwamba, ndani ya muundo wa suluhisho la kisiasa, “serikali ya Palestina” ndiyo pekee inayoshikilia uamuzi wa amani na vita, na kutokuwa na nafasi kwa makundi yenye silaha nje yake, sio tu ni upuuzi na kujitenga na uhalisia lakini pia halina msingi kabisa. Hakuna kitu kinachoitwa serikali au mamlaka ya Palestina; bali, kuna chombo cha ukandamizaji kwa watu wa Palestina ambacho kinafanya kazi ili kuhakikisha usalama wa umbile la Kiyahudi kwa baraka za Amerika na Ulaya. Wakati huo huo, uwepo wa mujahidina, ambao hutikisa misingi ya usalama wa umbile la Kiyahudi, ndio uhalisia wa kweli ulio uwanjani. Wao ndio ambao wamepata usikivu wa ulimwengu kupitia mafanikio yao huko Gaza. Kauli hii haiakisi chochote ila uwiano wa utawala wa Jordan na hatua za Mamlaka ya Palestina yenye khiyana, ambayo dori yake imekuwa kuua wapiganaji wa upinzani badala ya kulaani uchochezi huu, ambapo vyombo vya usalama vya Mamlaka ya Palestina vinaua watu wake wenyewe.
Je, Safadi na utawala wake hawaelewi athari za kile anachotahadharisha kuhusiana na “mlipuko wa hali katika eneo” kutokana na kushadidi mauaji na mauaji ya halaiki ya umbile la Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi mara baada ya mapigano huko Gaza kukoma? Hii inaashiria dhamira ya umbile la Kiyahudi ya kunyakua Ukingo wa Magharibi, pamoja na hatari zinazofuata kwa Jordan, kama vile kuhamishwa kwa lazima au kwa khiyari kwa Wapalestina katika ardhi yake, kwa kisingizio cha utawala mpya wa Amerika, kulingana na balagha yao ya kisiasa. Je, yeye haelewi hili na kuutayarisha utawala wake kwa mapambano ya kweli ya kijeshi ili kuling'oa umbile hili, hasa pamoja na watu wanaounga mkono wenye shauku ya jihad na kufa shahidi, badala ya kusujudu kichwa chake kila mara umbile la Kiyahudi linaposonga mbele zaidi na matamanio yake?
Labda wanapaswa kuwasikiliza wale waliowatangulia katika njia ya kujisalimisha kutoka miongoni mwa maafisa wa utawala huo, kama vile Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na balozi wa kwanza wa Jordan katika umbile la Kiyahudi, Marwan Muasher. Baada ya kuapishwa kwa Trump, Muasher alisema kuwa kuhusu hatima ya kadhia ya Palestina chini ya utawala mpya wa Trump, kuwepo kwa timu ya Marekani yenye msimamo mkali wa kisiasa na kidini kunaongeza hofu juu ya kutokuwepo kwa nia yoyote ya kweli ya kufikia suluhisho la haki kwa kadhia ya Palestina. Muasher pia alikuwa amesema katika taarifa zilizochapishwa miaka miwili iliyopita: “Wakati umefika wa kutambua kile ambacho kimekuwa dhahiri kwa miaka michache: suluhisho la dola mbili la kumaliza mzozo wa Palestina na ‘Israel’ limekufa na haliwezi kufufuliwa. Kadri jumuiya ya kimataifa inapong'ang'ania zaidi suluhisho hili lisilowezekana, ndivyo kadri shimo inavyojichimbia yenyewe.” Je, utawala huo sasa umefikia mahali hauwezi kufanya lolote ila kubangaiza siku chache zaidi kabla ya kuipeleka nchi na watu wake kwenye maangamivu?
Hatimaye,
[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَن كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ]
“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf:37]. Suluhisho pekee la kadhia ya Palestina linatokana na kuhamasishwa kwa majeshi ya Ummah ili kuling'oa umbile la Kiyahudi kutoka Palestina yote na kuiregesha kwenye kumbatio la Ummah chini ya kivuli cha Khilafah Rashida, ambayo misingi yake inawekwa huku uungwaji mkono wake maarufu ukienea katika ardhi za Waislamu. Utambuzi huu umewezekana baada ya Mwenyezi Mungu kuuwezesha Ummah kushuhudia kwamba suluhisho kama hilo linawezekana, kufuatia miezi 15 ya mapigano ya kishujaa ya mujahidina huko Gaza. Licha ya muungano wa ukafiri, ukoloni, na tawala tiifu zinazokula njama dhidi ya Gaza, vita vijavyo havitashuhudia nguvu ile ile ya usaliti na kutiishwa. Damu ya Umma sasa inachemka kwa hasira kwa kiburi cha Mayahudi, uungwaji mkono wa Marekani kwao, na kuungwa mkono na wakoloni makafiri, sambamba na ushirikiano wa watawala vibaraka wao. Watawala hawa hawajafichuliwa tu kwa watu wao bali sasa wanangojea siku ambayo wao pia wataanguka—kama vile wengine waliowatangulia walivyoanguka, kama madikteta wa ulimwengu wa Kiarabu. Na dhalimu wa Ash-Sham hayuko mbali na kukutana na hatima hiyo hiyo.
[الَّذِينَ آمَنُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ الطَّاغُوتِ فَقَاتِلُوا أَوْلِيَاءَ الشَّيْطَانِ إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفاً]
“Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapiana katika njia ya upotofu. Basi piganeni na marafiki wa Shet'ani. Hakika hila za Shet'ani ni dhaifu”. [An-Nisa:76]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: http://www.hizb-jordan.org/ |
E-Mail: info@hizb-jordan.org |