Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari

H.  19 Jumada II 1442 Na:
M.  Jumatatu, 01 Februari 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mfumko wa bei: Tatizo Sugu ndani ya Mfumo Muovu wa Kiuchumi wa Kibepari

Wakenya wa kawaida kwa sasa wanakumbana na hali ngumu ya maisha kufuatia ongezeko kubwa la bei ya bidhaa muhimu kama vile unga wa ngano, sukari, mkate na mafuta ya kupikia. Tatizo hili ambalo limekuwa ni sugu linalowaacha wakenya taabani huku ikizingatiwa kwamba zaidi ya nusu yao wanaishi katika hali ya uchochole. Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir Kenya ingependa kusema yafuatayo:-

Wakati ambapo Umma unakumbana na hali hii ngumu ya kiuchumi, viongozi wamejitia hamnazo wanajihusisha na porojo za kisiasa zisizomnufaisha raia bali ni kugombania tu madaraka ili kuendelea kujitajirisha. Hali hii ya kutamausha inatokamana moja kwa moja na usimamizi duni wa kiuchumi wa serikali. Taifa la Kenya kama lilivyo taifa lolote linaloshikilia  mfumo wa kibepari unaoruhusu uchukuaji wa mikopo iliosheheni riba hali inayolazimu serikali kutumia njia ya utozwaji mkubwa wa ushuru  karibu katika kila huduma na bidhaa ili kugharamia madeni.

Mfumko wa bei huwa ni tatizo la mara kwa mara ndani ya mfumo wa Kibepari uliochukua mfumo wa pesa za makaratasi sizokuwa na faida halisi kwani haiwezi kubadilishwa kwa kitu chochote chenye kushikika. Thamani yake huchukuliwa tu kutoka kwa ugavi na mahitaji tu. Ukosefu huu wa thamani yenye faida hufanya pesa za makaratasi kukosa thamani ya kudumu hivyo hushuka na kupanda, hali inayowafanya wale walio na ukiritimba juu yake kuweza kuchapisha pesa zaidi wakati wowote ule. Kwa hatua hiyo wao ndio wa kwanza kujipatia mtaji mkubwa wa pesa zisokuwa za halali kwao, seuze kusababisha mfumko mkubwa wa bei ambao hakuna ukuaji wowote wa mapato. Ifahamike kwamba katika mfumo wa Kibepari suala la mfumko wa bei pamoja na muundo wa kisarafu ni silaha zinazotumiwa kudhibiti usambazwaji wa bidhaa na huduma.

Uislamu una sera imara ya kisarafu iliosimama juu ya msingi wa kisarafu za chuma zilizo na thamani yenye kushikika. Hapa ndio huja ule mfumo wa Dhahabu na Fedha kama thamani mbadala ya sarafu, mfumo huu hufanya usambaswaji wa sarafu kuwa imara wakati wowote hivyo mawakala wenye uchu wa kupapia mali wa sekta za fedha kutoweza kuhujumu usambazwaji wake kwa mapato ya muda mfupi. Kwa kuegemea mfumo wa dhahabu na fedha, tatizo la mfumko wa bei huwa dogo ama kukosekanwa kabisa ndani ya mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu. Zaidi ya haya, Mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu huzingatia zaidi mikakati na sera za  kuufanya uchumi ni wenye kukua kwa kasi, hii ni kwa kupitia utumiaji mzuri wa mali ghafi katika kuunda viwanda vitakavyoajiri watu wengi. Twasema kutekelezwa kwa mfumo wa Kiuchumi ndani ya dola ya Khilafah kutahakikishia raia chakula cha kutosha pamoja na kutatua tatizo la kupanda kwa gharama za maisha.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

 Hizb ut- Tahrir in Kenya 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu