Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  18 Dhu al-Qi'dah 1441 Na: H 1442/14
M.  Jumanne, 29 Juni 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut-Tahrir Kenya Yatuma Ujumbe Wake kwa Ubalozi wa Pakistan Ukibeba Mwito wa Kusitisha Utowekaji wa Naveed Butt.

Katika mojawapo ya sehemu ya kampeni ya Kiulimwengu kushinikiza serikali ya Pakistan na majenerali wa Kijeshi kumwachia huru Naveed Butt aweze kujumuika na Familia yake. Siku ya Jumane tarehe 29 Juni 2021 Hizb ut-Tahrir Kenya ilituma ujumbe wake katika afisi za ubalozi wa Pakistan Jijini Nairobi.

Ujumbe huo uliongozwa na Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut-Tahrir / Kenya Shabani Mwalimu aliyesuhubiana na:

Yasin Kiwayo - Mkuu wa Kamati ya Mawasiliano ya Hizb ut-Tahrir / Kenya.

Yusuf Gasana - Mwanachama wa Hizb ut-Tahrir / Kenya.

Ujumbe huo ulifika ubalozini majira ya saa nne na dakika thelathini na mbili (10:32 AM)  kwa majira ya Afrika Mashariki ukakutana na kuzungumza na mmoja ya wafanyikazi kwa Jina la Charles ambaye aliahidi kumpa balozi nakala tatu za taarifa kwa vyombo vya Habari kwa lugha tatu; Kiurdu, Kiarabu na Kingereza.

Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir ilio na anwani: “Wito wa Kutaka Kumalizwa kwa Kupotezwa kwa Nguvu kwa Naveed Butt Nchini Pakistan”. Taarifa hiyo ilijumuisha wito wa kukomesha opotezwaji wa kimabavu wa msemaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya Pakistan, Mhandisi Naveed Butt, aliyetekwa nyara zaidi ya miaka tisa na ujasusi wa Pakistan ambaye hadi leo hajulikani alipo. Tokea mwaka wa 2012, tawala zilichokua hatamu nchini Pakistan zimekataa kubaini alipo na hali imefikia kiasi kuwa majasusi wa Pakistan wanawatishia Familia yake kumwangamiza endapo hatositisha amali zake za Kisiasa katika Hizb ut-Tahrir.

Taarifa hiyo ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir pia ilijumuisha wito kwa maafisa watiifu wa ngazi zote za majeshi ya Pakistan, ikisema: Someni ayah zinazoambatana na miito yenye kuyapamba mabega yenu. Kumbukeni mafundisho ya itikadi asili ya kivita ya jeshi lenu…

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir, aidha ilielekeza mwito wake kwa wanadiplomasia wa Pakistan ukiwaambia: “Nyinyi mnawakilisha sura, sifa, historia na hivi sasa watu wa Pakistan ulimwenguni. Kupotezwa kwa nguvu kwa Naveed kunachafua sifa ya haki katika nchi yenu. Kwa hivyo tunakulinganieni mufanye sehemu yenu katika kumaliza aibu hii ambayo serikali imejiletea.” Taarifa hiyo pia ikaeleza mwito kwa kila Muislamu na kila mwanahabari kushiriki kwenye kampeni hii ya kutia shinikizo kwa serikali ya Pakistan. “Tunakulinganieni nyote: njooni mjiunge na kampeni hii kuishinikiza serikali ya Pakistan na majenerali wa jeshi lake kumwachilia huru Naveed Butt na kumunganisha tena na familia yake. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

"Lakini wakiomba kwenu msaada katika Dini basi ni juu yenu kuwasaidia."

[Al-Anfal: 72].

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut-Tahrir Kenya

#MwacheniHuruNaveedButt

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu