Afisi ya Habari
Kenya
H. 30 Shawwal 1442 | Na: 1442/12 H |
M. Ijumaa, 11 Juni 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kusomwa kwa Bajeti: Adhabu ya Kila Mwaka ya Serikali Dhidi ya Raia wa Kawaida
Alhamisi Tarehe 10, Juni 2021 Waziri wa Fedha Ukur Yattani alisoma bajeti ya mwaka 2021/2021 ya Shilingi trilioni 3.632. Bajeti hii ambayo ndiyo kubwa zaidi kuwahi kusomwa katika historia ya Kenya ina nakisi ya shilingi trilioni 1.2. Kima cha shilingi trilioni 1.97 cha bajeti hii kinatarajiwa kukusanywa kupitia utozwaji ushuru huku kiwango cha shilingi trilioni 1.63 kikichukuliwa kutoka mikopo na ruzuku. Mamlaka ya mapato ya Kenya inatazamia kukusanya shilingi bilioni 835 huku kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ikitarajiwa shilingi bilioni 472.9 na ushuru wa uzalishaji katika bidhaa ukikisiwa kuwa kiwango cha bilioni 241.
Harakati ya Hizb ut-Tahrir Kenya ingependa kutaja yafuatayo;-
Bajeti hii inawasilishwa katika kipindi ambacho raia wa kawaida wamejawa na wasiwasi juu ya mkopo kutoka kwa shirika la Fedha duniani IMF wa jumla ya kitita cha shilingi bilioni 255 uliochukuliwa na Nairobi kwa lengo la kupunguza nakisi ya sasa ya fedha. Hatua hii imeilazimu serikali ya Kenya katika miaka ya hivi karibu itumie zaidi ya nusu ya ushuru kulipia mikopo yake. Ni wazi kwamba bajeti ya mwaka wa 2021/2022 kama zilivyo bajeti zozote zile ndani ya serikali za Kibepari humaanisha kuadhibu mamilioni ya Wakenya ili kuingiza mikono yao zaidi mifukoni huku tayari wakikabiliana na mfumko wa bei uliofanya bei za bidhaa msingi kama vile unga wa ngano na mafuta ya kupikia kupanda maradufu zaidi. Kwa uhakika haya ndio matunda ya mfumo muovu wa kirasilimali unaofanya mfumo wa fedha wa riba ndio msingi wa kupeleka uchumi wake hali inayopelekea mirundiko na mizigo ya madeni huku ukiongeza kiwango cha kulipia deni. Ni bayana kwamba Bajeti zinazochorwa kwa misingi ya IMF na Benki ya dunia huletea taifa maafa zaidi ya kiuchumi bali kulifanya kuwa mateka wa kiuchumi.
Tofauti na Uislamu ambapo ukusanywaji wa ushuru hauzingatiwi kuwa mapato yenye kuendelea, bajeti za kirasilimali hufanya mzigo wote wa matumizi yake kuegemea zaidi utozwaji mkubwa wa ushuru huku nakisi yake ikifidiwa na madeni na ruzuku. Na kwa muktadha huu ndio twasema kuwa taarifa za bajeti za kirasilimali hujumuisha vifungu vinavyoletea raia ugumu zaidi wa kiuchumi bali vikijumuisha matumizi ya kifahari na tarakimu kubwa ambapo huishia kuwapa wanasiasa uwezo wa kupora mabilioni ya pesa.
Dola ya Khilafah ambayo kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu SWT kusimama kwake ni kwenye kukurubia siku hadi siku, haitopoteza wakati katika zoezi la uhusiano mwema kusoma bajeti za kila mwaka hii ni kwa kuwa mapato na matumizi yake tayari yapo, kwani yamekwisha elezwa na sheria za Mwenyezi Mungu. Khilafah haitotoza ushuru kwenye mishahara ya watu (PAYE) ama ushuru wa kimapato kwani ina vyanzo maalum vya kupata mapato ya umma ikiwemo rasilimali asili kama vile madini ambapo zitaweza kutumiwa kuweza kukimu mahitaji ya raia pasina kuumiza watu katika ushuru. Kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kusimamishwa Khilafah ndio kutakapokomboa walimwengu kutokana na dhulma za kitawala na umasikini uliozagaa.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut-Tahrir
Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |