Alhamisi, 16 Rajab 1446 | 2025/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  2 Jumada I 1443 Na: 1443/05 H
M.  Jumatatu, 06 Disemba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chini ya Mfumo wa Kibepari Mtandao wa Barabara Daima ni Wenye Kukaribisha Maafa

Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir inatuma rambirambi zake kwa wanafamilia na marafiki waliopoteza wapendwa wao kwenye ajali ya mto Enzui baada ya basi kutumbukia ndani ya maji, ambapo hadi kufikia sasa watu 33 wameaga dunia. Kwa majeruhi wa mkasa huu, tunawatakia afueni ya haraka.

Katika maafa kama haya, tunaweka bayana kwamba ajali huingia kwenye mzunguko wa matendo ambayo wanadamu hawawezi kuyazuia. Hata hivyo, Uislamu unaamrisha wanadamu kuwajibika ipasavyo na kuwa makini pindi wanapotenda matendo yao sawasawa wawe ni abiria ama madereva na wengineo. Uislamu aidha, unataka masuala ya usalama wa umma kupewa kipaumbele bali serikali inapaswa kuhakikishia raia wake miundo mbinu imara ili kuweko na usalama wa barabarani kwa raia wote. Isitoshe, serikali inatakikana kuweka mikakati na hatua ya kuhakikisha kuwa magari ya abiria yana vigezo vyote vya kuweko barabarani ili yaweze kutoa huduma bora ya usafiri.

Ajali hii na zile zilizotangulia zinaonesha wazi hali mbovu ya barabara ambazo kwa hakika zipo katika mazingira ya kukaribisha majanga. Kwa sababu ya ufisadi uliosheheni, kila uchao barabara hutiwa viraka na kufanya kutopitika kwa kunyesha tu marasharasha kwani hugeuka kuwa ni mito na mitego ya vifo. Cha kuhuzunisha zaidi, baadhi ya maeneo nchini hadi sasa hayana barabara nzuri huku raia ambao tayari wanasota kwa uchochole wakilimbikiziwa zigo la ushuru. Hii ndio sura halisi ya mfumo muovu wa Kibepari na tawala zake ambazo hazitilii maanani maslahi ya umma. Cha kutamausha, kwenye kung’ang’ania kwao utawala, wanasiasa wa kibepari huzunguka na Helikopta pembe zote za nchi wakifanya kampeni ya kuwinda kura lakini kwa kipindi cha mafuriko wao hubakia tu kuangalia tu runinga raia wanapokufa maji! Hii bila shaka ni hadaa kubwa ya ubepari na watawala wake wanaodharau maisha ya raia masikini.

Sisi katika Hizb ut-Tahrir tunabainisha waziwazi kwamba hali hii mbovu itaendelea kushuhudiwa chini ya mfumo fisidifu wa kibepari unaofadhilisha zaidi maslahi ya wanasiasa zaidi kuliko yale ya raia wa kawaida. Kwa hivyo tunatoa mwito kwa jamii nzima kuunga mkono kazi ya kuleta mabadiliko ya kikweli ya kuondosha mfumo wa kibepari na kuweka mahala pake mfumo safi wa Uislamu. Kwa yakini Uislamu ndio mfumo pekee unaojali maslahi ya umma yakiwemo yale ya usalama wa abiria na hii ni kuwa ni mfumo wenye sifa ya uwajibikaji katika masuala yote yakiwemo suala la usalama barabarani ya yote yanayofungamana na ukaguzi wa magari ya abiria na kutengeza barabara nzuri.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut-Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu