Jumatano, 12 Ramadan 1446 | 2025/03/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  23 Sha'aban 1446 Na: 1446/07 H
M.  Jumamosi, 22 Februari 2025

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Sudan imekua Jeraha jengine Chungu kwa Umma wa Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 18 Februari 2025, kikosi cha Rapid Support cha Sudan kilifanya mkutano katika jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta (KICC) jijini Nairobi kuzungumza uundaji wa serikali ya umoja ya majimbo yanayodhibitiwa na kikosi hicho nchini Sudan. Utawala nchini Kenya unashikilia kudai kwamba kujihusisha kwake kwenye mazungumzo hayo ni kuimarisha “juhudi za amani nchini Sudan”. Nairobi imetetea uamuzi wake wa kuwa mwenyeji wa kufanya mazungumzo na kikosi cha wapiganaji yanayolenga kusainiwa kwa mkataba wa kisiasa. Maafisa wa Kiutawala wa Sudan wameiona hatua hii kama jaribio la kuanzisha utawala mwengine sambamba na ule wa Khartoum, hatua hii ya Kenya imepelekea kulaumiwa kwake kwa kukiuka ubwana wa Sudan na kujihusisha na matendo ya kiuhasama.

Hizb ut Tahrir / Kenya ingependa kuangazia yafuatayo:

Huku ikiwa maudhui ya mkataba huo wa Kisiasa hayajatolewa kwa umma, lakini kinachotarajiwa ni kueleza mfumo wa kiutawala wa RSF, malengo yake ya kisiasa na mikakati yake ya kuunganisha udhibiti wake kwa majimbo yake. Mkataba huo unalenga kuja na muundo wa kiutawala kwenye maeneo ambayo RSF inayadhibiti. Kiuhakika ni jambo la kuhuzunisha kuiona Nairobi kwa kisingizio cha kutafuta suluhu ya mizozo, inaendelea kucheza dori ya kiuwakala ya kuendeleza mizozo inayopelekea kupotea maisha ya wanadamu!

Uhalisia wa hali ya sasa ya kisiasa nchini Sudan na nchi zengine zinazoendelea kama vile Somalia na DRC ziko hatarini kwa nguvu za nje ambazo, kwa kufuata maslahi ya mataifa makubwa ya Magharibi (Marekani na Uingereza). Inasikitisha leo kushuhudia nchi za Kiafrika na taasisi zake zote kama vile AU na IGAD zikishiriki katika kuunga mkono maslahi na ushawishi wa wakoloni wa Magharibi. Tangu mzozo huo ulipozuka miaka miwili iliyopita, tamko lote la mapatano, kuanza tena kwa mapigano, mazungumzo na mawasiliano ni kati ya pande mbili zilizo na uhusiano na Amerika: uongozi wa Jeshi na uongozi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka.

Nia ya Marekani ni kupunguza mzozo kati ya vibaraka wake na kudhibiti matokeo kwa kugawanya dori kati yao. Hatua yake hii ni kusambaratisha vikosi  pinzani vinavyoegemea upande wa Uingereza na Ulaya ambavyo tangu machafuko yaanze vimekuwa vimelemazwa. Kwa hakika, vibaraka wa Uingereza katika kadhia ya Sudan ni kikosi cha Freedom and Change na vyengineo.

Mizozo na ‘miito ya kutafuta amani’ kote barani Afrika inachangiwa pakubwa na mvutano wa kiubabe wa Kikoloni. Sudan imekuwa ni jeraha jengine baya la Umma wa Kiislamu baada ya kushuhudiwa miongo mitatu ya Waislamu kupigana wao kwa wao nchini Somalia.

Tunahitimisha kwamba kwa vile migogoro yote barani Afrika na Ulimwenguni kwa jumla inapangwa na mataifa yenye uchu wa kikoloni na washirika wao, suluhu za kikweli kamwe hazitofikiwa na mfumo wa Kibepari unaendeleza ukoloni. Kwa hiyo, Afrika inahitaji mfumo mpya wa dunia yaani Uislamu ili kuikomboa kutoka kwa mnyororo wa kikoloni unaoliona bara tajiri la Afrika kama chanzo cha malighafi na soko la bidhaa zao.

Uislamu unamkomboa Mwanadamu kutoka kuwa mtumwa wa mtu mwengine badala yake kumfanya mja wa Muumba wake Mwenyezi Mungu (swt) Kwa maana haya, mfumo wake wa utawala (Al-Khilafah) utafanya kazi kuelekea kuwakomboa walimwengu wote katika nyanja zote za maisha. Hapo ndipo Afrika itakapokombolewa na kuishi kwa heshima na mafanikio.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu