Ijumaa, 02 Jumada al-thani 1442 | 2021/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  9 Shawwal 1441 Na: 1441/11
M.  Jumapili, 31 Mei 2020

  Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chini ya Pazia la Ugaidi Polisi Watekeleza Mauaji ya Kinyama

Polisi wamewaua kwa kuwapiga risasi mtu mmoja na watoto wake wawili kwenye uvamizi wa usiku katika kaunti ya Kwale Kusini mwa Pwani ya Kenya. Polisi wanadai kwamba Mohamed Rahma Mapenzi mwenye umri wa 41 anayejulikana pia kwa lakabu ya Spanya, alikuwa gaidi anaye windwa na kwamba ati kwenye uvamizi huo aliwatumia watoto wake kama ngao-binadamu baada ya kuwarushia guruneti maafisa hao! Mke wa Marehemu, bi Mwanahalima Mwachili aliyekuwa na uja uzito wa miezi minane, alipigwa risasi tumboni na mguuni na sasa amelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Msambweni akiwa katika hali mahututi. Hizb ut-Tahrir / Kenya, inatuma rambirambi zake za dhati kwa familia na marafiki wa marehemu na kumuombea majeruhi afueni ya haraka.

Kufuatia kitendo hiki cha kikatili, tunapenda kueleza yafuatayo:

Tangu kupitishwa kwa Mswada wa Kupambana na Ugaidi, ni bayana kuwa polisi mara kwa mara wamekuwa wakiteleza mauaji ya watu nje ya sheria, pasi na uchunguzi wa kina wa mambo, wala amri ya mahakama. Polisi wamekuwa wakituhumiwa kuvamia majumba ya washukiwa, wakiwapandikizia silaha na kuwapiga risasi washukiwa. Vipi polisi waliopokea mafunzo wadai kwamba baba mzazi alitumia watoto wake mwenyewe kama kinga kwake dhidi ya risasi?

Ni wakati sasa kwa raia na hasa jamii ya Kiislamu nchini kuitilia shaka hulka hii ya polisi kwani nchi hii kattu haiwezi kuyafungia macho mauaji haya ya kinyama kwa jina la kupambana na ugaidi. Ama wanasiasa wanaojitokeza wakidai kushutumu ukatili huu, hili kihakika si lolote isipokuwa hufanya hivyo kama mawakala tu wa kiserikali na wa mahusiano ya umma.

Tunaeleza kinaga naga kwamba udhalilishaji na unyanyasaji huu unaoshuhudiwa leo, ni miongoni tu mwa maonevu mengi yanayofanywa dhidi ya Waislamu kote duniani na, kwa yakini kamwe hayatokoma hadi pale Waislamu waregeshe faradhi kubwa iliyo telekezwa ya kufanya kazi kwa lengo moja pekee la kusimamisha tena Khilafah- Ar-Raashidah kwa njia ya Utume katika mojawapo ya nchi nyingi za Waislamu. Utawala huo ndio pekee ulio na uwezo wa kulinda Waislamu na hata wasiokuwa Waislamu dhidi ya unyama wa aina yoyote ile.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu