Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  23 Jumada II 1445 Na: H.T.L 1445 / 11
M.  Ijumaa, 05 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Inatoa Rambirambi zake kwa Shahid Sheikh Saleh Al-Arouri na Wenzake
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon uliwasilisha salamu za rambirambi kwa ajili ya shahid Sheikh Saleh Al-Arouri, ambaye hivi karibuni alipoteza maisha katika mji mkuu Beirut. Rambirambi hii ilitolewa katika nyumba ya maombolezi iliyoandaliwa kwa ajili yake na wenzake katika Ukumbi wa Quds katika kambi ya Nahr El-Bared, kaskazini mwa Lebanon.

Akizungumza kwa niaba ya ujumbe huo, mwanachama wa Hizb Sheikh Ahmed Al-Shamali alielekeza hotuba yake katika nukta tatu:

• - Mujahidina mashujaa katika ardhi ya Gaza, ambao wameonyesha udhaifu wa umbile la Kiyahudi. Kwa miaka mingi, Magharibi na watawala vibaraka wamejaribu kulionyesha kama umbile lisiloweza kushindwa na dola isiyoweza kushindwa. Alisisitiza uwezekano wa kuliondoa umbile hilo nyakuzi iwapo utashi na dhamira ya kweli itakuwepo ndani ya Umma na majeshi yake.

• - Kufichuliwa kwa watawala vibaraka baada ya Tofan Al-Aqsa (Kimbunga cha Al-Aqsa), ambapo usaliti na njama zao dhidi ya kadhia tukufu ya Palestina na watu wake yalidhihirika. Ilisisitizwa kuwa wao ndio vikwazo usoni mwa msukosuko wa Umma, ambao hatimaye utaliondoa umbile la Kiyahudi na kuiregesha Palestina yote kwenye ardhi za Uislamu na Waislamu.

• - Umuhimu wa kuhamasisha juhudi na uwezo wa kila mtu kuukusanya Ummah na majeshi yake kuelekea kwenye harakati kubwa inayowaangusha watawala vibaraka wanaosimama kati ya Umma na Palestina. Hatimaye, majeshi ya Umma yanapaswa kusonga mbele ili kuwanusuru watu wa Gaza na kuikomboa ardhi yote iliyobarikiwa ya Palestina.

Taarifa hiyo ilihitimishwa kwa kuwaombea mashahidi na watu wa Gaza na Palestina.

Ujumbe kutoka Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon, pamoja na Kamati ya Matukio katika eneo la kusini, walishiriki katika kutoa rambirambi kwa Mashahidi katika manispaa ya mji wa Sidon.

Zaidi ya hayo, walishiriki katika msafara wa mazishi ya mashahidi katika mji mkuu, Beirut.

Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi hao na awajaalie majeruhi wapone kwa ukamilifu na haraka. Na awape ushindi na afueni watu wa Palestina, Aqsa yake, na Umma wa Kiislamu, aikomboe ardhi na watu. Na rayah (bendera) ya Uislamu inyanyuliwe juu, na Shariah ya Mwenyezi Mungu isimamishwe katika ardhi yake. Na ipeleke ujumbe Wake kwa ulimwengu kupitia wito na jihad.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu